Samahani wandugu,
Mi huwa nashangaa, hivi hawa watu wanaoamini (wanaosema) kuwa Slaa katumwa na kanisa/katoliki ina maana huwa wanaamini kweli au wanataka tu kuchafua hali ya hewa? Hebu tujifunze kuchagua maadui jamani.
Kwa haraka bila hata kufanya uchunguzi wa kina, shida yetu kubwa ni umasikini wa kujitakia, viongozi wasio na utu, (Bila kutujali wanyonge na dini zetu) maamuzi yasiyofaa ya viongozi, kudanganywa mara nyingi sana viongozi wetu, mifumo ya uongozi ambayo haisukumi kuwajibika viongozi. Watu wenye uchu jamani hawana dini, hata angekuwa shehe au padri, alhaji au askofu, wakishaanza tu uchu na wizi, basi sio mwenzenu tenaaaaa.
Kuna ile hadithi ya fisi wawili na sungura:
Hapo zamani fisi wawili waiokota pande la mkate mkubwa wakakubaliana wagawane. Basi mmoja wao akaumega ule mkate ila ukaonekana umezidi kidogo upande mmoja, ili kupata muafaka watatue vipi tatizo la kugawiana bila kuoneana wakamwita sungura aje awasaidie, basi sungura akawasikiliza weeeeeee, akavichukua vile vipande viwili akauliza kipi kikubwa? Wakajibu wote hicho mkono wa kushoto, Sungura akangata kile kipande kikubwa kikapungua, akauliza tena sasa je vimekuwa sawa au kipi kikubwa? Wakajibu kwa pamoja kabisa, hicho mkono wa kulia, Sungura akakingata kile kipande kikubwa kikapungua, basi ndo ikawa hivyo, kila kipande kikingatwa kinapungua zaidi, inabidi kungwatwe kingine ili kikaribie kile kidogo.
Hatimaye vikabaki vitonge viwili ambavyo havilingani vilevile, ndio wale jamaa wakapata fahamu wakamuambia sungura awaache wajiamulie mambo yao wenyewe,
Jamani hawa wanaokuwa huko juu haijalishi ni wa dini gani, hawafai kuwaamini na mali yetu, tupange sisi, hata tukipunjana kidogo, si neno kama akishiba mmoja.
Alivyokuwa Mkapa na Nyerere tulilalamika sana, anapendelea wakristu, wakiwa Mwinyi na Kikwete wanapendelea waislamu, bora tuwafunge wote/yeyote anayekuja ashindwe kufanya nje ya tunayomtuma.