Tamko la Kamati Kuu ya Chadema: Jan 31 Jan, 2011

Tamko la Kamati Kuu ya Chadema: Jan 31 Jan, 2011

Tunawaombeeni kila la kheri ila msigombane na polisi tu. Tuko pamoja na nyie kinadharia lakini sio kiitikadi (kwani siwaungi mkono Chadema ila napinga ufisadi). Sifikirii kama Chadema wamefikiria vizuri katika kukawakatalia CUF hiyo itazidi kuwamaliza badala ya kuwajenga kwani wamegubikwa na tuhuma za kwamba ni chama chenye udini (hasa ndugu zangu wakristo)!!! Wangeliwaruhusu CUF na ikisha baadae wakaharibu kwa kuonyesha upambe dhidi ya CCM then CUF ingelikufa kifo cha mende. Hivi nadhani Chadema ndio wanajiandalia kaburi lao karibuni hakuna mtu atawaunga mkono isipokuwa wanacham ka wa chadema tu.

huo ni ujanja ccm na usalama wa Taifa kutugawa kidini ili Check bob Jk aendelee kutula kilaiiiiiiiiiiiini! tumia akili we mlevi wa dini
 
Ama!!! Kumbe kuna watu waliomba kuchaguliwa ili wakaiunge mkono CHADEMA bungeni?! Mi nilidhani wabunge waadilifu wataunganishwa na hoja za kuwatetea watanzania bungeni? Kumbe ikiwa CUF watapeleka muswada kuwa mafisadi wote wafilisiwe itabidi CHADEMA wasiuunge mkono na vise-versa?! Wabongo bado tuna kazi.

acha kupotosha umma elevuka,mlevi wa dini wewe! kutumia hicho kimodem iwe tabu kwetu eee
 
Vita vya panzi ( CDM + CUF ) ni furaha ya kunguru ( CCM ). Kwa mtindo huu hawa jamaa watatawala nchi maisha. Well done CDM kwa kutoa maamuzi ya kuisaidia CCM

Nyie ccm na cuf acha kujichanganya,walishagwanyika kitambo hawa, muafaka ulikuwa kati ya ccm na cuf,sio upinzani tayari huo ulikuwa boge la mgawanyiko.
 
Je, Makubaliano ya CCM na CUF yako wazi ( MOU) - waweke hapa tusome wote. Hamad anatembelea Benz - ataweza kusema ufisdi kwa nguvu zote! tusiwe wanafiki - nchi inaitaji watu jasiri kwa sasa na CDM waongeze pressure kwa serikali kila jambo linalogusa maisha ya watanzania.
 
Kurunzi, points nzuri! Lakini mimi ni mpenzi wa Chadema ila kijaribu kufanya siasa kivingine. Ushirikiano na vyama vingine vya upinzani si muungano wa vyama. Wengi wa wachangiaji wanamtizamo wa TANU + ASP = CCM. la! Ni makubaliano ya ku-support misimamo. Hakuna siri zinazouzwa TLP, UDP, NCCR au hata CUF. Ni uhusiano wa kusupport misimamo huku bara. Nikupe mfano Ujerumani kuna vyama vinavyokinzana kwenye siasa za kitaifa lakini vikaungana kwenye siasa katika majimbo. Nadhani tunapaswa kujifunza demokrasia ya vyama vingi
Ndugu ZED, Wewe hujajibu swali langu, umetupa mfano wa Ungereza kwa kutaja vyama viwili. Swali langu liko palepale. Hapa tuna Ccm na CUF walioungana upande mmoja, halafu tunataka CHADEMA iungane na CUF!! Naomba unipe muungano wa aina hiyo Uingereza... Chama tawala kimeungana na chama kingine, wakati huohuo chama kikuu cha upinzani bungeni kimeungana na hicho chama cha pili!! Ndo maana pale juu nimekuuliza ktk mfano wa Uingereza unaotupa chama cha tatu kiko wapi?! sababu hapa tuna chama tawala(ccm), chama kilichoungana na chama tawala kuunda serikali(cuf) na chama cha upinzani(Chadema). Ili mfano wa Uingereza ufae kwetu tuwekee hapa vyama vitatu vya huko vilivyo na ushirikiano mnaoshauri hapa.. kumbuka hakuna anayesema cuf + chadema ni sawa na Tanu + Asp iliyoleta ccm!
 
acha kupotosha umma elevuka,mlevi wa dini wewe! kutumia hicho kimodem iwe tabu kwetu eee
Hee!! kaka/dada, kumbe hapo nimeshataja dini tayari??? Ngoja nirudie kusoma post zangu zote, nikikuta dini I promise you, nitakuomba msamaha hapahapa... usikonde ndugu..sawa eeh?!
 
Hee!! kaka/dada, kumbe hapo nimeshataja dini tayari??? Ngoja nirudie kusoma post zangu zote, nikikuta dini I promise you, nitakuomba msamaha hapahapa... usikonde ndugu..sawa eeh?!

Msomi kabisaa alafu unapotosha ukweli
 

1. Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya.
Kamati Kuu imezingatia na kupongeza juhudi za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pamoja na wadau mbalimbali wa demokrasia nchini za kudai Katiba Mpya. Aidha, Kamati Kuu imejadili na kutafakari kwa kina maoni ya wadau mbalimbali juu ya mchakato unaofaa katika kupata Katiba Mpya, na kuzingatia kuwa njia sahihi ni ile itakayowashirikisha wananchi kikamilifu na kwa dhati bila kujali tofaui zao za kisiasa, dini, umri, elimu, kabila wala jinsia zao. Kamati Kuu imezingatia pia kwamba Tume ya Rais sio njia sahihi itakayowezesha upatikanaji wa Katiba Mpya yenye kuzingatia utashi, matakwa na mahitaji ya wananchi wa Tanzania. Hivyo basi:

  1. Kamati Kuu imepinga utaratibu wa kuunda Tume ya Rais katika uundaji wa Katiba Mpya
  2. Kamati Kuu imeunga mkono utaratibu wa kutumia Bunge katika kutengeneza na kusimamia mchakato utakaoletekeza upatikanaji wa Katiba Mpya
  3. Kamati Kuu imeipongeza Sekretariati yake kwa kumwagiza Mheshimiwa John Mnyika kuandaa na kuwakilisha Hoja Binafsi inayolitaka Bunge kuandaa sheria itakayoweka utaratibu na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya
  4. Kamati Kuu imewahimiza na kuwaomba wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunga mkono Hoja Binafsi ya Mheshimiwa Mnyika kwa maslahi ya Taifa.

================================​


Siamini kuwa kamati kuu ya CHADEMA ni dumbers kama walivyo viongozi wa sekretari yake hivi sasa. Siamini kuwa wao wanaamini kuwa wabunge 47 wao wanaweza kuwalazimisha zaidi ya wabunge 270 kuwafuata.

Kutokana na mazingira waliyoyajenga mara baada ya ushindi wa viti 47 sioni uwezekano wa wao kuungwa mkono ama na wanaCCM wala vyama vingine kama ilivyokuwa hapo kabla ambapo walifaidika sana na mahusiano kiasi waliyoyajenga na baadhi ya wabunge wa CCM lakini hata hivyo hakuna wakati ambao waliweza kuwalazimu wabunge hao kuwaunga mkono katika hoja yao isipokuwa pale tu inapotokea kuwa hoja hiyo inalenga kundi moja la CCM dhidi ya kundi linguine kitu ambacho sikioni kwa sasa.

Zaidi aina ya siasa za migongano ambazo vinara wa sasa wa chama hicho wamezikumbatia sioni uwezekano wa kuweza kujenga mahusiano ya kuwezesha ushirikiano na wabunge wa CCM walio wengi ingawa nina shaka kuwa yawezekana wanategemea kufaidika na yale makubaliano ya Freeman Mbowe na Edward Lowassa ambayo waliyafikia miaka ile kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM wa 2005.

Sioni uwezekano wa hoja za ghadhabu na chuki za Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Joseph Selasini, Godbless Lema, Wenje na zile za kishabiki za John Mnyika na Halima Mdee zinaweza kuwashawishi ama wabunge wa CUF au hata robo ya wabunge wa CCM kuwaunga mkono hoja yao. Simuoni Zitto Kabwe wanayemtenga kuwa mstari wa mbele katika siasa za kishabiki na kinazi kama hizi na wala simuoni Makamu Mwenyekiti wao Mzee Arfi waliyemtelekeza tangia alipoaanza kuugua mara baada ya uchaguzi kutumia busara zake kuwalainisha wabunge wa vyama vingine.

Ama yawezekana kuwa wanaamini kuwa kutumia live coverage ya vipindi vya bunge kutawasaidia kujijenga zaidi kwa wananchi na kuwachonganisha CCM na vyama vingine kwa wananchi. Hivyo basi kwao wao haya yote ni masuala ya kujenga umaarufu kwa wao kama wanasiasa na chama chao kuliko umakini wa kujenga nchi na kutetea maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Katika hali hii nathubutu kukubaliana na mawazo ya baadhi ya watu kuwa ni wazi Chadema ya sasa kimekuwa chama cha kutumia kila kitu kujipatia umaarufu na kusahau ile kauli mbiu iliyowasadia kwa kiasi fulani ya MASLAHI YA TAIFA KWANZA, vyama baadae. Misimamo yao na mikakati yao kisiasa hivi sasa sioni chembe ya nia ya kuweka mbele MASALAHI YA TAIFA KWANZA, na chama baadae. Kwa CHADEMA ya sasa, hizi ni enzi za CHAMA KWANZA, Taifa baadae…
 
Hii imetulia kweli, kilichobaki ni utekelezaji.
 
@mgalanjuka nyie mlio na hiyo bajeti kubwa mbona hatuyaoni hayo maendeleo yenu?

Ah nimesahau kumbe yapo mengi tu kama vile:
(1) kuenea kwa malaya na wafanyabiashara ya ukahaba.
(2) kuenea kwa mauwaji ya kutisha. Kwa mfano, jana mwananyamala wameoneka watoto 10 (kumi) wameuliwa na wakaingizwa ktk shimo moja.
(3) kuenea kwa foleni za barabarani,vyuoni,ktk maduka ya kununua luku. N.k.
(4) kuendelea kwa mgao wa umeme ktk kila kona za mijini na vijijini.
(5) kuenea kwa ukosefu wa chakula na njaa ktk miji kama vile arusha ambako serikali inawagawia chakula cha msaada wananchi wa huko, pia njaa ktk mikoa ya dodoma,morogoro n.k.
(6)kuenea kwa ujambazi nchi nzima. Kwa mfano wale walioteka mabasi ya abiria,kuteka makanisa kwa risasi,kuteka miji kama vile mwanza n.k.
(7)....
(8)....
......endeleza orodha maana ni ndefu.

Kitu kimoja ni muhimu kujua kua pamoja na hali ngumu ya maisha ya zanzibar lkn si rahisi kumkuta mzanzibari halisi akifanya biashara ya ukahaba kama watanganyika. Ukipita maeneo ya m/mala A mchana malaya wanakuvuta mkono.

@ Geza ulole mavazi kila mtu anayake, haikatazwi kinachokatazwa ni mavazi specific ya chama fulani ambacho si kile kilichoandaa hayo maandamano. Weye ukija na misalaba yako hukatazwi. Kama unaopa nikabu,kibaraghashia n.k. Itakua huna akili.
 
Kwa watanzania wote wapenda amani na maendeleo ya nchi yetu, nawaombeni tuikimbie CCM na CUF maana ndani yake kuna hila na nia mbaya isiyoitakia na kuwatakia mema wananchi wa Tzl, walichokifanya Z'bar ni cha kiaibu!
Hongereni sana kamati kuu ya Makamanda, tupo nanyi mpaka kitakapoeleweka!!
Sio wazee tena, sisi ni vijana tuliokubali kufa kwa ajili ya watoto wetu wa sasa na si kwa ajli ya kesho tu!! Tupo tayari kwenda na wazee wenye busara na hekima kama ya mzee wetu Martin Luther, na Mandera na tutawaheshimu na kuzitii busara zao lakini wakumbuke kuwa wanatembea na hatari iwapo watajaribu kuleta mahusiano ya CCM na CUF katika kazi yetu, kazi tuliyo nayo ni ngumu sana inahtaji moyo na juhudi ili kuweza kufikia mwisho wenye mafanikio. Jambo la kwanza tuanze kujenga mori wa mapambano ndani ya akili na ufahamu wa kutafuta haki na Maendeleo ya nchi yetu ndani ya jeshi letu la nchi, lakin pia hatushindwi kuwatoa kwanza endapo wataonekana kutupinga coz tuko nao mitaani so wao hawtatushinda, Tunisia walichokifanya ni fundisho ata kwa kikwete ata km bado akijatimia kwake, LAKINI wahenga wetu walikutwa na hayo ndo mana wakaseme UKIONA MWENZIO ANNYOLEWA NAWE ANZA KULOWANISHA NYWELE ZAKO maana baada ya yeye na zamu yako! Kikwete, alikuwa ananyolewa Mtunis, Mmisiri akatia maji, sa ivi ananyolewa, sasa nadhani wewe usitie maji tena wewe ingia ivo ivo kwa kinyozi maana muda huna tena muda wa kuloweka izo nywele zako, ukzingatia kwanza nia dredi, Kinyozi tayari kashaingia TZ, Wachafuuu wote tunawanyoa mtake mstakeeeeeeee!!!!!! si na uchafu, apo atuna huruma, Tanzania yetu ni safi, Kikwete na wenzio acheni kututia aibu kwa uchafu wenu! Tafuteni jinsi ya kuuficha huo uchafu wenu wa DOWANS kabla hatujaingia bungeni na sio kuuficha uvunguni bali mkaoge kabisa la sivyo bado OMO inawahusu na dodoki la gunia!!, la sivyo tutawaaibisha bure, na nadhani mkikosa akili ya kusolve hii mapema, nawaahikikshia elf 2na 15 hata fom hamtapta, mana mnaenda kufa! DOWANS na ndg yake na Ricmoond hawawaachi mkiishi Tz hii! POLENI SANA!!!!! bt ni ujinga wenu mi nawambia!!!!
 
sio KAFU ni CUF, CUF wana mbunge mmoja tu bara!


mkuu ... kweli wewe unatokea uru kishumundu..... humu jamvini tunatumia impliedly terms.... KAFU=CUF..., jeykey=mheshimiwa..., CDM=CHADEMA..., sisiem=CCM.......

sawa mkuu....usiogope
 
Hurusiwi kuvaa nguo za chama chengine zaidi ya zile za cuf. Kama unashida ya maandamano njoo la kama unashida ya kuvaa magwanda ya wafungwa subiri maandamano ya chadema keshatangaza padri slaa mda si mrefu.
Mwite majina yote utakayo ila habari ni kuwa Chama chako kimetoswa.full stop.:laugh:
 
Niliona tangazo TBC kuwa maandamano ni ya kupinga kuongezeka kwa gharama za umeme na gesi. Baadae nikaona tangazo jingine source nyingine ikisema Chadema inaandaa maandamano kupinga malipo ya DOWANS. At the same time from diffferent source nikasikia CUF nao wanaandaa maandamano kupinga malipo ya DOWANs. I really support every move on these issues and I would wisely suggest a coordination CUF, CHADEMA,Vijana CCM,....if possible. Any segmented movement will not yield any frutful results.
 
kumbe chadema sasa wanamtambua chitanda. tumeua watu wetu bure
 
Hivi hawa cuf why wanapenda huku na huku? wakijifungua mtoto watampa nani?
ccm au cdm? Hata mlete propaganda gani'hatudanganyiki ng'o.
 
Back
Top Bottom