Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Jana wakati jeshi la Tanzania linatoa hoja tofauti pamoja na kujibu maswali ya waandishi wa habari kutokana na milipuko ya mabomu yaliyotokea kule G/Mboto na kuadhiri maisha ya Watanzania, nilimsikia mkaguzi mkuu wa JWTZ Brigedia-Jenerali Leonard Mndeme alitoa sababu tofauti ambazo zinaweza kuchangia kulipuka kwa mabomo yale, lakini pia hakujaribu kugusia pia kama kunaweza kukawa na uwezekano wa hali ya maisha duni kwa wanajeshi wa Tanzania ambayo sio kitu cha kuficha hata sisi wananchi tunaona hali ya polisi pamoja na wanajeshi ilivyo, je haipelekei kwa jeshi hilo kwanjia fulani wakajitokeza wanajeshi ambao kwa lugha ya kijeshi mnasema kutokua na nidhamu wakahusika kwa njia moja au nyingine kulihujumu jeshi hilo kwa kutokukidhi maslahi ya wanajeshi au kikundi fulani jeshini hapo? Nawasilisha hoja.