Kwakuwa imeandikwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa...lakini mbona naona wamejaza siasa kwa wingi sana?
Nimeona tukumbushie tu tulikotoka..
Soma kwa makini hii Taarifa ya Mhe. Pinda kuhusu suala la Richmond utabaini jinsi gani Serikali inavyojikanganya na kujaribu kutapatapa kupotosha ukweli ili kulinda wale waliohusika moja kwa moja na ufisadi huu. Haiyamkiniki kwa Mhe. Rais akatoa matamko ambayo mahudhui yake yamejaa hadaa tupu. Hivi hana uchungu na fedha za watanzania zinazopotea kulipa gharama za utekelezaji wa mikataba hewa pamoja na kulipia watendaji wake wabovu ambao wamelifikisha Taifa hapa tulipo na bado wanaendekea kututia matatizoni akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali yake?
http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdfhttp://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdfhttp://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdf
Nashukuru kwa kutuletea tukumbushie za siku zilizopita: Ila kuna kitu kinachosumbua hapa. Riport ya richmond president alipewa? Je ilisemaje na president aliamua nini?
Je Richmnd waliiambia serikali kama mdau mkuu kuwa tunaiuza tenda?
Wizara ya nishati na madini kwanini walisaini mkataba bila ya kumhusisha preident? au hizi baraka za mkataba alizitoa president. Basi kama baraka zilitolewa na presida then mzigo wa kwake na analijua fika uozo wote.
Heri ya ya mimi mfa maji.
Katika kuweka record sawa.. Karamagi hakuhusika na kuingia kwa Richmond. Aliyekuwa waziri wa nishati wakati huo alikuwa Msabah na aliachishwa ngazi kwa scandal ya Richmond.
Kama sikosei Karamagi tunamkuta ktk swala zito la mkataba wa Buzwagi, kitu ambacho sielewi ni kwa sababu gani aliachishwa Uwaziri ikiwa mradi huo huo bado umekamatwa na Barricks kwa mpini wa mkataba ule ule feki uliotiwa sahihi mjini London Hotelini..