Mambo Aliyofanya Rais
Katika suala zima la kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme, Rais alihusika katika mambo manne. Kwanza, katika kuamua TANESCO itumie mitambo ya kukodi kuzalisha umeme na Serikali igharamie ukodishaji huo. Suala hilo lilikuwa lazima liamuliwe na yeye kwa sababu lilikuwa linahitaji Serikali kugharamia ukodishaji. Kama si hivyo lisingefikishwa kwake kwani ni jambo ambalo lingekuwa juu ya TANESCO kuamua kukodisha na kulipia. Gharama hizo hazikuwa zimepangwa katika bajeti ya serikali hivyo ilikuwa ni lazima kupata idhini ya Rais ya kutafuta hizo pesa na kuzitumia kwa ajili hiyo.
Pili, Rais alihusika katika kuzungumza na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuwaomba wakubali sehemu ya pesa waliyopanga kuipa Tanzania kama msaada kutokana na mpango wa msamaha wa madeni itumike kugharamia ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme. Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond (ambayo baadae ikawa Dowans) na matumizi mengine ya dharura za umeme. Matumizi hayo mengine yalijumuisha pia ununuzi wa mitambo ya aina ya Watsilla ya kuzalisha megawati 100 za umeme pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Mitambo hiyo imeshanunuliwa, kufungwa na tayari inazalisha umeme.
Tatu, Rais alihusika katika vikao vya Baraza la Mawaziri vilivyojadili matatizo ya upungufu mkubwa wa umeme nchini na kuamua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo. Moja ya hatua zilizoamuliwa kuchukuliwa, ni hii ya kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Katika vikao hivyo vya Baraza la Mawaziri alitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika zoezi zima la kupata makampuni au watu watakaotoa huduma hiyo. Hususan, Rais alisisitiza kuwa pamoja na udharura uliokuwepo Kanuni na Sheria ya Ununuzi wa Umma zizingatiwe.
Nne, Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 milioni na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumuomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo. Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wafanye mambo mawili. Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond. Isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hukuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake. Pili aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe. Maagizo hayo ya Rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo. Lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.
watanzania wakipata uhuru wa kuongea, wanautumia vibaya. Siyo uungwana hata kidogo kumuita rais wetu 'idiot'. Kamwe siwezi kukubaliana na utovu huu wa nidhamu uliokithiri. Rais ni 'head of state' ndiyo 'baba' yetu. Sasa wewe unaweza ukamuita baba yako mzazi 'idiot'? HAPANA, tusifikishwe huko. Kinachotakiwa katika 'blog' hii ni hoja zenye mantiki kwa faida ya nchi yetu na siyo matusi yasiyo na tija.
Ni kweli JK ana mapungufu, kwani yeye ni binadamu kama sisi. Lakini pamoja na mapungufu hayo JK 'has this country at heart". Hana utajiri, ni 'mlalahoi' mwenzetu; hana makuu. JK ni mchukia rushwa na ufisadi, hana uroho wa kujilimbikizia mali. Amefananafana na Mwalimu Nyerere kwa upande wa tabia na kuipenda nchi yake na watu wake.
Lakini ni kweli tamko hilo la IKulu kuhusu Richmond lina kasoro. Hakukuwa na sababu ya kutoa tamko hilo. Maelezo hayo yangeweza kutolewa katika namna nyingine lakini siyo kutolewa na IKULU. Kwa maoni yangu kuna kasoro na mapungufu mengi kuhusiana na baadhi ya watendaji wa IKULU. Tukumbuke IKULU ni 'taasisi' nyeti. Inapaswa iwe na watu makini na waadilifu. Sina hakika sana kama kweli baadhi ya watu ndani ya IKULU ni makini na waadilifu kwa kiwango cha kutotiliwa shaka. Sina hakika na hili, kama kweli baadhi wanaipenda nchi na ni watendaji wazuri.
Suala hili la Richmond lisipofanyiwa kazi kwa umakini linaweza likaigawa nchi yetu. Mjadala ndani ya Bunge kwa hakika haukuwa mzuri kwa umoja wetu. Nina hofu ya kitakachotokea mjadala huu ukianza tena na kuendelea zaidi.
This is stupid & wrong move
sasa msemaji wa ikulu ni nani? Luhanjo, salva au wale ma mediocres wengine?
Ikulu imekuwa kama chaka la incompetents...yaani media wanaset Agenda halafu wao wanafuata
hiii issue as far as i know uchunguzi haujakamilika nau liko mikononi mwa vyombo vya sheria sasa whats this kujibizana na media...sometimes i dont understand those ******...tangu juzi naona wanatoa statements kila kukicha
why pick a fight wanajua clearly they cant win? Just wehn tunataka kujua kwa nini miradi ya Milleium Challenge Account ina delay wao wanataka kufufua mambo ambayo yatawatoa from main agenda ya kuwahudumia wananchi
sasa sijui nani kawaambia kuwa its better kujibizana kuhusu mambo haya..ukweli ni kuwa wakishatoa statement next week nzima wataandamwa mpaka mwiki mbili...sasa wakishatoa hii whats next? watajibu na Meremeta ? then baada ya hiyo watajibu na kwa nini kamati ya mauaji ya Mwembechai haijaundwa mpaka leo?
hawa jamaa wanatia kinyaa sana
I guess the only person than can save JK's presidency ni Mama Salma maana husikii wao kujibizana na media..huu ni mtego na i am not sure they will get themselves out of it
Yaani this thing is simple na nashangaa kwanini wanatumia nguvu nyingi na kuita wahariri,kupoteza muda na kutusumbua tu.
Ndiyo Jk hausiki nani anahusika sasa,kwanini wasimtaje jina?na kama walipuuzia maagizo ya Mkulu walichukuliwa hatua gani?
Navyojua Rais ana uwezo wa kutengua uteuzi wa mtu yeyote,alifanya aliutenguza uteuzi wa balali(usanii flani).Hata hili linawezekana kabisa na afanye sana.
Hili suala la RDC ni siasa za maji taka ambazo wamezipiika wao wenyewe.tatizo ni uwaziri mkuu na hawana lolote.Tokea six alipokosa U-PM basi imekuwa vuru vuru mechi tu..
sasa watamalizana wao kwa wao na mie naona tuangalie 2010..tunampa nani Nchi,Je tunaamua kumsuport Mkwere au tunaunganisha nguvu na kuchagua Chaguo La Mungu.
.............................. Watendaji wa IKULU wawe makini sana na masuala nyeti kama haya.
Mwenyewe nikadhani labda huwa nachelewa kuangalia Tv. Alifuta utaratibu wake wa kuongea na Taifa kila mwisho wa mwezi? Sababu ni nini hasa?Nuilidhani mwisho wa mwezi uliopita mukulu mwenye we angeliongelea hili kwa undani kwenye hotuba zake za kila mwisho wa mweZi.... oh! hivi zilifutwa vile eh????
Hata najua ndugu yangu!!! Mi nimeona tu hotuba zimeota mbawa!!!Alifuta utaratibu wake wa kuongea na Taifa kila mwisho wa mwezi? Sababu ni nini hasa?
Hata najua ndugu yangu!!! Mi nimeona tu hotuba zimeota mbawa!!!