Tamko la Chadema: Rais asiteue wajumbe hadi sheria irekebishwe

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akiongea na waandishi wa habari leo John Mnyika amemshauri rais asianze kuitumia hiyo sheria hadi sheria hiyo ibadilishwe.
 
Hivi kama asingesaini na badala yake akasubiri kufanya marekebisho ni maslahi gani ya Taifa ambayo yangehatarishwa? Tuna imani gani na Rais(mwenye rekodi ya kutoaminika hata ndani ya chama chake wakiwamo washirika wake wa karibu) juu ya kutounda tume au kufanya ghiliba baada ya kusaini sheria hii?
 
Nyie Mgwanda msituletee sarakasi zenu za kikatuni hapa. Hivi kulikuwa na ugumu gani ya kutoa haya madukuduku yenu pale kwenye sebule za magogoni? Au mlilewa zile kahawa za Brazil na kashata za Kuwait mlizokunywa na mkulu? Hapo hesabuni imeshakula kwenu na hakuna chochote mtakachoongea kitakachosikilizwa na Magamba.
 
Akiongea na waandishi wa habari leo John Mnyika amemshauri rais asianze kuitumia hiyo sheria hadi sheria hiyo ibadilishwe.

Kama hilo ndilo tamko kali tulilolisubilia, basi CDM imeshindwa katika medani za siasa za nchi hii. CCM imeshinda vita bila hata kutupa risasi moja.
 
Nadhani ni rahisi kuifanyia marekebisho sheria kuliko mswada. Mara nyingi "option" ya pili ya kutosaini mswada huwa haitumiki sana na watawala walio wengi.
 
Kama hilo ndilo tamko kali tulilolisubilia, basi CDM imeshindwa katika medani za siasa za nchi hii. CCM imeshinda vita bila hata kutupa risasi moja.

Unaweza kufafanua zaidi kauli yako? Kwani wewe ulitaka watoe tamko lipi? Nakushauri usome vizuri nini kiliwapeleka CDM ikulu.
 
Akiongea na waandishi wa habari leo John Mnyika amemshauri rais asianze kuitumia hiyo sheria hadi sheria hiyo ibadilishwe.

mnataka kibadilishwe kitu gani?
hilo suala si rahisi namna hiyo, kubadili lazima mrudi bungeni na mtu wa CDM atoe hilo pendekezo. Je kwa uwingi wenu litapitishwa?
mf. mdogo ni huo kwamba Rais asishiriki, na pia uwingi wa CCM bungeni utaathiri mwenendo wa maandalizi ya katiba hivi mnategemea JK atakubali? au CCM watakubali maana mnaongelea kwamba wawaachie dola nyie.
 
kwa mantiki nyepesi tu nilitegemea John Mnyika angemuuliza Mheshimiwa Rais kwamba nini kitafuata endapo atasaini sheria na chadema wangepata jibu palepale Ikulu. Huku ni kutafuta tu umaarufu wakati chadema ilikwenda Ikulu na timu nzito wakiwemo maprofesa wawili.
 
Hivi kama asingesaini na badala yake akasubiri kufanya marekebisho ni maslahi gani ya Taifa ambayo yangehatarishwa? Tuna imani gani na Rais(mwenye rekodi ya kutoaminika hata ndani ya chama chake wakiwamo washirika wake wa karibu) juu ya kutounda tume au kufanya ghiliba baada ya kusaini sheria hii?
Mkuu Ben shauriana na viongozi wa CDM watafakari kwa umakini kinachotokea,haya matamko si makubaliano waliyosaini! Mpaka sasa sijielewi kabisa! tumeanguka vibaya ingawa vyombo vingi vya habari vimetusaidia kutosemea sana aina ya makubaliano tuliyosaini! Tumelikoroga sasa tulinywe.nakuhakikishia kuchomoka hapa hadi kueleweka inahitajika siasa ya kipekee sana.mpaka leo na hilo tamko la CDM ndio wanazidi kuchanganya watu.mimi mwenyewe nimemsia mheshimiwa Mbowe akihojiwa na BBC mara baada ya kikao hakusema wamekubaliana asisaini ule muswada! Naona kama mnasita kusema ukweli mkuu tumedharirika vibaya mno na vile viji paragraph viwili vya kihuni! Mkuu ile aibu ya mwaka!
 
tukiwaambia ugonjwa wa kulalamika ni wa viongozi wote mtasema ni wa ccm tu. Mnyika analalamika mtaani wakati alipata fursa ya kuonana na rais mwenye majibu hayo kisha tutaambiwa JK hapokei ushauri wakati hakushauriwa kuhusu kusaini au kutosaini muswada kuwa sheria
 
Hili sio tamko la chadema ni tamko la Mnyika. tamko la chadema ni lile alitamka Mbowe leo
 
Hivi kama asingesaini na badala yake akasubiri kufanya marekebisho ni maslahi gani ya Taifa ambayo yangehatarishwa? Tuna imani gani na Rais(mwenye rekodi ya kutoaminika hata ndani ya chama chake wakiwamo washirika wake wa karibu) juu ya kutounda tume au kufanya ghiliba baada ya kusaini sheria hii?

Hapo ni ingekuwa ni kulivunjia heshima Bunge lilimpokelea huo mswada au saini na lilimuwekeakea muda maalum wa kuwa amesha usaini. Kumbuka kuwa Bunge ni Mhimili wa Serikali kama Ilivyo Rais na Mahakama.
 
pengine kusaini au kutosaini haikuwa moja ya agenda iliyowapeleka akina Mnyika Ikulu ndio maana Rais kasaini
 
hoja za chadema hazikuwa za kuzuia sheria hoja ilikuwa kupata maoni baada ya sheria kwa sababu hiyo maoni yao yatajumuishwa wakati wa mchakato wa kutoa maoni
 
hakuna anayeshangilia kusainiwa kwa sheria hiyo bali tunakataa kutuletea maswali mepesi hapa kwa majibu magumu ambayo chadema wangeyapata Ikulu
 
Back
Top Bottom