BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Tamko kuhusu Chenge lasubiri Sekretarieti ya Maadili
Gloria Tesha
Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00
Gloria Tesha
Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00
Sektarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kutoa tamko kuhusu mwenendo wa maadili ya Andrew Chenge kama mtumishi wa umma, kutokana na madai kuwa anamiliki akaunti nje ya nchi yenye thamani ya Sh bilioni moja.
Kamishna wa Sektretarieti hiyo, Jaji Stephen Ihema, aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kwamba wanasubiri uchunguzi unaoendelea dhidi yake ukamilike ndipo watoe kauli kulingana na tamko lake la mali anazomiliki kama alivyowasilisha katika chombo hicho. Sisi tuna matamko yake kama kiongozi wa umma; hatuwezi kuyasemea sasa hivi, ngoja uchunguzi unaofanywa sasa ukamilike, alisema Jaji Ihema wakati akijibu maswali ya waandishi hao.
Jaji Ihema alikuwa akizungumza baada ya uzinduzi wa ofisi ya Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi Dar es Salaam, akijibu maswali yao kuhusu nini msimamo wa chombo hicho cha maadili kwa kiongozi huyo kutokana na kashfa dhidi yake.
Chenge, ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, anatuhumiwa kuhusika katika rushwa ya dola za Marekani milioni 12 zilizolipwa na kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada Tanzania. Anatuhumiwa kula rushwa kutoka kwa Shailesh Vithlani ambaye pia anatuhumiwa kuwa kinara katika ununuzi wa rada hiyo, jambo lililosababisha ajiuzulu uwaziri wa Miundombinu, mwaka jana.