BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,365
- 8,097
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania imewataka viongozi 658 waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki, kufanya maandalizi ya uhakiki huo.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Novemba 2, 2022 na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumzia kuhusiana na shughuli hiyo.
“Viongozi watakaohakikiwa ni baadhi ya mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na wengine wa kada mbalimbali,” Amesema viongozi hao wataohakikiwa ni kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam, Lindi, Njombe, Dodoma, Tanga, Geita, Mwanza, Tabora na Iringa.
Amesema wananchi wenye taarifa muhimu kuhusiana na raslimali na madeni ya viongozi pia wanaombwa kutoa ushirikiano ili kufanikisha jukumu hili.
Aidha, amesema sektarieti inatoa rai kwa wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi na mamlaka nyingine katika maeneo mbalimbali kutoa ushirikiano.