Tamisemi huyo mkurugenzi wa Pangani ni mpigaji na wasaidizi wake asiachwe kabisa, mpaka leo ajira mpya hawajalipwa pesa za kujikimu

Amie whitney

Member
May 21, 2023
78
183
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Isaya Mbenje na Watendaji walio chini yake kujitafakari juu ya mwenendo wa utendaji kazi wao kutokana na kushindwa kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri hiyo ikiwemo kutumia Tsh. bilioni 1 yote waliyopewa wajenge Shule ya Pangani Halisi bila kukamilisha ujenzi huku wakiomba wapewe tena Tsh. milion 700.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo alipotembelea miradi ya Shule Wilayani Pangani akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Zainab Abdallah, ambapo Ndejembi ameonesha kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Pangani Halisi iliyogharimu kiasi cha TSh. bilioni moja, Shule ya Sekondari Masiaka inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP inayogharimu Tsh. milioni 585 na Shule ya Msingi Bushiri iliyogharimu Tsh. milioni 440 ikijengwa kupitia mradi wa BOOST ambapo hata hivyo DED hakumkuta Pangani kwakuwa yupo likizo.

Amesema mwaka jana kabla DC wa sasa Zainab hajahamishiwa Pangani, Halmshauri hiyo ilipewa Tsh. bilioni 1 kujenga Shule ya Pangani Halisi lakini hela imeisha yote na mradi haujaisha ambapo wamejenga madarasa matano na magofu ambayo hayaeleweki na bado wameomba tena wapewe Tsh milioni 700 ili wakamilishe “Wamepewa Tsh. milioni 470 ya Shule ya Sekondari Jumaa Aweso mwaka jana, wamekamilisha madarasa manne tu”

“Mkurugenzi wa Halmashauri na Wasaidizi wake wajitafakari, hawamsaidii Rais katika ngazi ya huku chini kuna kukosekana kwa umakini na kujali kwasababu hatuwezi kuja tukakuta hali ya aina hii, bilioni imekatika hapa hatuwezi kumchekea Mtu ambaye anachezea pesa ya umma”

“Fedha nyingi Mh. Rais kaleta, Mh. Mbunge kazipambania kwa Wananchi wake wa eneo hili ziweze kufika lakini kwenye utekelezaji mambo gongana, Mna Mbunge mzuri ambaye ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso mna DC mzuri Zainab Abdallah lakini Halmashauri haina Kiongozi (DED)”
#MillardAyoUPDATES
 
Back
Top Bottom