msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Hivi karibuni mmebuni utaratibu wa hovyo wa kuajiri walimu kimya kimya kupitia mawasiliano ya simu za mkononi.
Huu utaratibu sio rafiki hasa katika zama hizi za maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo utapeli wa mitandaoni umeongezeka, hivyo matapeli wanaweza kutumia mwanya huo kutapeli watu kwa kujifanya ni maafisa kutoka wizara yenu.
Utaratibu wa kuajiri kwa kupigia watu simu si tu umegubikwa na utapeli bali pia una kiuka sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma. Sababu Kwa mujibu wa sera hii ajira zote za Serikali zinatakiwa kutangazwa hadharani ili kila mtu mwenye sifa zinazo takiwa kwenye ajira husika aombe.
Kwa hivyo kwenye ajira 6000 zilizotangazwa na mheshimiwa Rais Samia suluhu tunaomba mchakato wake uwe wa wazi ambapo katika hatua ya kwanza ni ajira zitangazwe watu waombe, kisha mchakato wa kuchambua wenye sifa ufanyike na baadae majina yatangazwe hadharani sio kupigiana simu kimya kimya.