TAMISEMI: Acheni kuajiri kimya kimya, mchakato wa ajira 6000 za walimu ufanyike kwa uwazi

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Hivi karibuni mmebuni utaratibu wa hovyo wa kuajiri walimu kimya kimya kupitia mawasiliano ya simu za mkononi.

Huu utaratibu sio rafiki hasa katika zama hizi za maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo utapeli wa mitandaoni umeongezeka, hivyo matapeli wanaweza kutumia mwanya huo kutapeli watu kwa kujifanya ni maafisa kutoka wizara yenu.

Utaratibu wa kuajiri kwa kupigia watu simu si tu umegubikwa na utapeli bali pia una kiuka sera ya menejimenti na ajira katika utumishi wa umma. Sababu Kwa mujibu wa sera hii ajira zote za Serikali zinatakiwa kutangazwa hadharani ili kila mtu mwenye sifa zinazo takiwa kwenye ajira husika aombe.

Kwa hivyo kwenye ajira 6000 zilizotangazwa na mheshimiwa Rais Samia suluhu tunaomba mchakato wake uwe wa wazi ambapo katika hatua ya kwanza ni ajira zitangazwe watu waombe, kisha mchakato wa kuchambua wenye sifa ufanyike na baadae majina yatangazwe hadharani sio kupigiana simu kimya kimya.
 
Wangeajiri kwa kufuata miaka wanachuo waliohitimu,hiyo biashara ya mifumo wizi mtupu.
Kuna wanachuo 2015/16/17/18/19/20 nakuendelea.
Siyo unaajiri 2020 unamwacha wa 2015.NOT fair
Hili nalo neno ila sasa wanaajiri kulingana na uhitaji kwa mfano wanahitaji walimu wa physics lakini kwenye intake ya 2015 hawapo kwanini wasichukue tu na wa 2020?
 
Hili nalo neno ila sasa wanaajiri kulingana na uhitaji kwa mfano wanahitaji walimu wa physics lakini kwenye intake ya 2015 hawapo kwanini wasichukue tu na wa 2020?
Nayo wazingatie miaka waliyohitimu
 
Wangeajiri kwa kufuata miaka wanachuo waliohitimu,hiyo biashara ya mifumo wizi mtupu.
Kuna wanachuo 2015/16/17/18/19/20 nakuendelea.
Siyo unaajiri 2020 unamwacha wa 2015.NOT fair
Good , Ila wacompasate na zile ajira walizo ajiri wasukuma wengi ili kujipendekeza kwa mkulu. Hii nayo imechangia Jafo atumbuliwe tamisemi.
 
Kumbuka Magu alipotangaza ajiza za walimu elf13 waliomba watu zaidi ya laki2 wenye sifa na wako kwenye kanzidata,wakatoa ajira elf7 kwamba wataongeza wengine kufikia elf13,nafikri ndo hiyo elf6 aliyosema mama hivyo hiyo namba wataichomoa tu pale kwa uelewa wangu watu watajulishwa kwa simu na kupitia tovuti ya ajira na tamisemi
 
Kweli tumefeli kama nchi..., Taifa lenye mamilioni ya wananchi wasio na ajira tunagombania ajira 6000?
 
kumbuka magu alipotangaza ajiza za walimu elf13 waliomba watu zaidi ya laki2 wenye sifa na wako kwenye kanzidata,wakatoa ajira elf7 kwamba wataongeza wengine kufikia elf13,nafikri ndo hiyo elf6 aliyosema mama hivyo hiyo namba wataichomoa tu pale kwa uelewa wangu watu watajulishwa kwa simu na kupitia tovuti ya ajira na tamisemi
Njia nzuri ni kuruhusu maombi mapya maana ukisema watumie kanzi data ya tangu mwaka jana December hadi leo kati kati hapa kuna waombaji wamefariki na wengine hawana nia ya kuajiriwa tena serikalini lakini kuruhusu kupokea maombi upya ni fursa ya kutambua uwepo wa waombaji na watu wenye commitment ya kuajiriwa kuliko kutumia kanzi data kupangia mtu kazi kumbe alishafariki zamani au hana nia na hiyo kazi tena
 
Kweli tumefeli kama nchi..., Taifa lenye mabilioni ya wanancho wasio na ajira tunagombania ajira 6000?
Jiwe ndiye alitufikisha hapa kwa sera zake mbovu na kuthamini sana maendeleo ya vitu kuliko maendeleo ya watu
 
Back
Top Bottom