Tamaa ya fedha kupita kiasi; is it worth it?

Tamaa ya fedha kupita kiasi; is it worth it?

sahihi kabisa. zamani baba yangu alikuwa anafanya biashara ya ubia na wenzake, wakamjeuka baba, wakakimbia na hela zote. Mzee akarudi kwenye umasikini.

Huwezi amini wale wababa waliomtapeli dingi wameshafariki na wengine walijiua kalafu hata na watoto wao wakageuka kama vichaa wengine wezi majambazi, ndoa zao zikavunjika wengine

Kuna mda nakaa najiuliza, so what? walifanya hayo yote na dhuluma, halafu ikawaje?
What goes around comes around
 
Pole sana , Hali itakua mbaya Zaid miaka ijayo...si unaona hata machawa wa ccm unafikiri kwanini ni machawa ..wengine wako tayar hata kufirwa ili wapare pesa ..
Kuna mmoja alifirwa ili apate elfu 90 tu.
Duh elf 90 alikuwa shida gan huyo maku.
 
Nisinukuliwe vibaya, ni kwa nia ya kuchokoza mada ili tujue ni kwanini ufalme wa pesa unazidi kuwa mkubwa duniani na Tanzania kwa ujumla.

Nitazungumzia Tanzania kwa sababu ndo ninaishi, huko duniani kwengine siwezi ku-draw conclusion sababu sijaishi.

Aisee, yaani sasa kila mtu hapa Tanzania anachowaza ni ufalme wa fedha! Kila kitu anachokifanyika, ajenda yake kupata fedha zaidi!

Kiongozi mwanasiasa anapewa nafasi fulani, siku yake ya kwanza ofisini, anaanza kuwaza atafanya mitikasi gani ili aanze kupata fedha kwa kutumia hiyo nafasi aliyonayo. Na akianza kupata hizo fedha, akili yake inachangamka anaanza kuwaza, atapataje fedha nyingine zaidi ya hizo anazozipata. Na endapo yeye kupata fedha zaidi, kunahusisha kumkanyaga mwenzake mguuni, basi yupo radhi amkanyage mara 100, ili aendelee kupata fedha zaidi.

Naenda kwa muuza bucha leo kununua maini, ananiambia bei ni 15,000 wakati jana ilikuwa ni 14,000 na najua bei ni 14,000. Namuambia nipe gram 500 ananipimia gram 460, namuambia, 'mbona haijatimia?' anasonya kwa kukasirika, anairudisha kwenye mzani na kuongeza gram 40, ili zitimie gram 500. Nakaa najiuliza, hii shida yote nini? Najijibu: Anataka kukupunja wewe, apunje na wengine 100, ili atengeneze fedha zaidi!

Huko makazini ndo kabisa. Yaani vikao kila siku mwenyekiti akiitisha AOB, wajumbe wakianza kuongea basi malalamiko yao ni kuhusu wao kupata pesa au kupunjwa pesa, au kufikiria kupewa pesa fulani. Yaani ni kupata pesa zaidi.

Tamaa ya pesa inatia kichefuchefu kwa sababu kuna mambo yanafanyika kwa ajenda ya tamaa ya fedha nyingi, yamejeuka kuwa machukizo kwa jamii. Huduma hazitolewina zikitolewa ni kwa ubora wa chini, dhulma, wizi, utapeli, mauaji... etc

Naomba kuuliza: Hivi huu ulafi wa fedha utaisha lini? Kwa nini watu wawe na mentality ya fedha kwanza, na fedha zaidi kwa gharama yeyote?

Kwa sababu unakuta mtu anakurusha fedha, au anakudhulumu haki yako, halafu mwisho wa siku unakuta anaandamwa na matatizo makubwa kiasi kwamba hata hizo fedha nyingi kwake hazina maana.

Tamaa ya kupata mahela mengi hata kwa njia haramu; does it worth it?

Tujadili.

Financial freedom ni muhimu

Pole sana , Hali itakua mbaya Zaid miaka ijayo...si unaona hata machawa wa ccm unafikiri kwanini ni machawa ..wengine wako tayar hata kufirwa ili wapare pesa ..
Kuna mmoja alifirwa ili apate elfu 90 tu.

Acha basi mkuuu 90 ikamtoa mtu rindaa aiseee

Mkuu acha utani basi, 90k mtu anakunjwa?

Kariri tu kuwa hakuna pesa nyingi kwa mkupuo zinazotoka kwa Mungu. Ukipata ufurahiye mapesa, chungulia tu ulimwengu wa roho ila uwe tayari kwa masharti.

Maandiko yamesema "fedha ni jawabu la mambo yote"

Mimi nani niende kinyume na maandiko?

Kwenye mambo yako ya kifedha usiambatane na mtu mwenye usongo sana na pesa

Kuna hawa viongozi wanao kula Nauri Sijui huwa wana waza nini

CCM inahusika vipi hapo

Afya njema / amani ya nafsi na moyo, chakula na pesa ndiyo mahangaiko yetu hapa duniani. Mengine ni ziada tu

What goes around comes around
kuna kitu wanadamu wanaita FINANCIAL FREEDOM.
kama jina lako tuu mtoa mada inaonyesha unatoa mikopo. sasa sijui ni una force au hujui dunis.





anywah hali hata sio kama mnavyoeleza na imeathiriwa na mazingira. ukikaa na watu flani usi generalize dunia au nchi nzima inafanya hayo.

asilimia 30 ya watanzania hata hawajui hela ni nini. wako vijijini wana kula kuolewa kuzaa na kufa.



anyway majibu yenu yote yapo hapa.


Dini rasmi inaitwa the Omnitheistic Singularity jina la Mungu na kitabu kikuu ni Omnipotent Singularity. Imeandaliwa na IIT
 
Hata kwa kukanyaga miguu ya wengine? Maana hoja yangu ndo ipo hapo.

Kwa hiyo seeking financial freedom ndo iwe kali mpaka kupata hela hata pale ambapo hujapanda?

Na kingine: hicho unachosema ni 'financial freedom,' ni jambo gani haswa?

Ukiwa na Milioni 500 au bilioni 1, hiyo ndo maana ya financial freedom?
Kuna member uku alicomment kwenye uzi flan iv akasema kama unataka kuelewa maana ya financial freedom kamsikilize mwakasege YouTube 2008, namimi nakusihi tena kamsikilize yule baba..#salute sana kwa yule member ase sijui ni nani
 
Kuna member uku alicomment kwenye uzi flan iv akasema kama unataka kuelewa maana ya financial freedom kamsikilize mwakasege YouTube 2008, namimi nakusihi tena kamsikilize yule baba..#salute sana kwa yule member ase sijui ni nani
Hata bila kumsikiliza, financial freedom ni subjective concept. Mtu unaweza kuwa na akiba ya 1 billion ukadhani upo financially free halafu linatokea tatizo la ugonjwa kwenye familia ambalo ndani ya mwaka mmoja au miwili likamaliza akiba yote uliyonayo. Ndo maana huwa nasema, financial freedom ni concept ambayo inaweza kubadilika muda wowote na hauwezi kuipima kwa pesa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom