Binafsi sipendagi kudaiwa,ila kunawakati mambo huwa juu chini,hupelekea mtu kuonekana si mwaminifu
Kiuhalisia hakuna mtu anae penda kila kukicha kuamshwa na sms ya deni au taarifa ya kitisho kutoka kwa yule anae mdai.
Kiafya pia ni nzuri kwani hutakaa unenepe kabsa na kuwa nyama uzembe na hata kuhatarisha maisha kwa kuwa na magonjwa ya moyo kama presha.
Binafsi nimeshawahi kudaiwa na kudai pia,ila katika kudaiwa ni hali ambayo huwa ni mbaya sana pale inapofikia kupelekana mahakamani na sehemu zingine,achana na madeni madogo ya kwa mangi na kwenye bar ya mzee fulani,
Kuna haya madeni ya kuanzia 1m+
Kwa kweli kichwa huwa kinawaka moto .
Tujitahidi kulipa palipo na nafasi ya kufanya hivyo ,pia wadeni wetu wawe wanajua hali kuwa si nzuri kwa sasa kwani tulio wengi mambo ya meshabadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma,tusijisifu kwa kutokulipa ila tujitahidi kulipa tunapopata nafasi ya kufanya ivo.
Kila la kheri katika kupambana na changamoto za awamu hii.
Sent using
Jamii Forums mobile app