kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,732
Wazungu ni watu wa ajabu sana,ok fine sisi ni maskini kwanini wao kila kukicha wanamiminika kuja afrika kutafuta fursa za uwekezaji? Kwanini wanatumia kila aina ya mbinu kutufanya sisi kushindwa kufanya mambo yetu wenyewe mpaka wao wawepo?.Wao wenyewe ndio wanatupiganisha sisi kwa sisi,wanatufanya tushabikie mambo yao ilihali tukiacha kufanya kazi kwa bidii.Ebu tujiulize nini mantiki ya hoja hii? Hivi inaingia kabisa akilini kwamba sisi ni maskini wale ni matajiri alafu wale ambao ni matajiri wanatutumia sisi ambao ni maskini ili wao waendelee kuwa matajiri alafu wanakuja kutuambia ninyi ni maskini sana kwa hiyo tufanyeje sasa?.Ndio maana tunaanza kulaumiana sisi kwa sisi alafu wao wanafurahi kwelix2 na kutuona sisi ni mazuzu na ujinga uliokithiri,maana kama tungelikuwa welevu tungeliwakataa ili tutumie fursa wanazitumia wao hapa Afrika/Tanzania ili nasi siku moja tuwekwe kwenye rekodi zao.Kwa mtizamo wangu si kweli kwamba sisi ni maskini bali wao ni maskini ndio maana kila kukicha wanakuja kuchukua mali zetu ili wao wawe matajiri.
Kwa mtazamo wako wao sio masikini, chukulia mfano nchi za kiarabu wenzetu sio masikini wanajivunia kwa mafuta waloyonayo na wao wanajitahidi kuyatumia ili kujikwamua kiuchumi wao ndo wanapanga bei ya kuuza mafuta yao lakini kwetu tuna Tanzanite haipo duniani kote isipokuwa Tanzania lakini usione ajabu bei wanapanga wanunuzi badala ya muuzaji pia tuangalie kwenye madini kama Dhahabu wenzetu South Africa, Botswana wanatumia vizuri dhahabu yao lakini sisi tunagawa Bure unategemea nini hapo. Sisi tuna utajiri wa mali na Rasilimali lakini ni masikini wa fikra na hii inachangiwa na Ubinafsi uliopo sasa miongozi mwa viongozi tulionao.