Leo katika Gazeti la Majira nimekutana na Repoti hii.
UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).
Ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012 iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kutoka Geneva, nchini Uswisi, ilisema idadi ya watu waliohamia Ulaya kutoka nchi maskini sana (LDCs) iliongezeka.
Ongezeko hilo ni kutoka watu milioni 19 mwaka 2000 hadi milioni 27 mwaka 2010, sawa na asilimia 3.3 ya wakazi wote wa nchi hizo.
Kwa mujibu wa ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012, iliyotolewa na UNCTAD, ilisema nchi maskini sana duniani zinatoa asilimia moja ya wahamiaji duniani kote.
Imesema wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs, wanaishi katika nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ngambo kwenda katika nchi zao, kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011, kutoka dola bilioni 3.5 hadi bilioni 27.
Mwaka 2011, kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada milioni 3.2 na kutoka Kenya milioni 2.5, ilisema taarifa hiyo.
Fedha zilizotumwa kwenda LDCs, zilikuwa mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI).
Nchi maskini zilizotajwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar na Malawi.
Nyingine ni Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Tanzania, Zambia, Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste, Yemen, Caribbean, Haiti,
Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu
My Take!
Hivi nchi hii tujiringanishe na Kenya tu ambao hawapo miongoni mwa nchi masikini walichotushinda ni nini kwa upande wa Rasilimali, Hapa naona viongozi waliopo madarakani wanacho cha kujibu kwa nini Tanzania kwa wingi wa Rasilimali tulizonazo bado ni Masikini, Hii ni aibu kubwa sana jamani.