Takwimu: Zijue nchi masikini Duniani

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,429
2,000

Leo katika Gazeti la Majira nimekutana na Repoti hii.
UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).

Ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012 iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kutoka Geneva, nchini Uswisi, ilisema idadi ya watu waliohamia Ulaya kutoka nchi maskini sana (LDCs) iliongezeka.

Ongezeko hilo ni kutoka watu milioni 19 mwaka 2000 hadi milioni 27 mwaka 2010, sawa na asilimia 3.3 ya wakazi wote wa nchi hizo.

Kwa mujibu wa ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012, iliyotolewa na UNCTAD, ilisema nchi maskini sana duniani zinatoa asilimia moja ya wahamiaji duniani kote.

Imesema wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs, wanaishi katika nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).

"Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng'ambo kwenda katika nchi zao, kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011, kutoka dola bilioni 3.5 hadi bilioni 27.

"Mwaka 2011, kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada milioni 3.2 na kutoka Kenya milioni 2.5," ilisema taarifa hiyo.

Fedha zilizotumwa kwenda LDCs, zilikuwa mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI).

Nchi maskini zilizotajwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar na Malawi.

Nyingine ni Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Tanzania, Zambia, Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste, Yemen, Caribbean, Haiti,
Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu

My Take!
Hivi nchi hii tujiringanishe na Kenya tu ambao hawapo miongoni mwa nchi masikini walichotushinda ni nini kwa upande wa Rasilimali, Hapa naona viongozi waliopo madarakani wanacho cha kujibu kwa nini Tanzania kwa wingi wa Rasilimali tulizonazo bado ni Masikini, Hii ni aibu kubwa sana jamani.

=======================

Watu wameng'ngania takwimu za miaka 20 iliyopita .. Tanzania nchi ya tatu kwa umasikini Duniani mara Tanzania nchi ya kwanza kwa umasikini Duniani. Angalia Orodha ya Nchi masikini kutoka katika macho ya watu wanaoijua Dunia. Tanzania haimo kwanye orodha ya nchi 25 masikini zaidi Duniani.. Hii maana yake imependa sana katika miaka ya hivi karibuni kutoka nafasi ya 3 hadi nafasi ya 26! Aidha kwa kasi tuliyonayo tunaendelea kuzivuta nyuma nchi mbali mbali na kwenda juu zaidi. Aidha Tanzania inatajwa kuwa moja kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi. Nchi Tajiri zaidi Duniani ni Qatar!

https://fbcdn-sphotos-e-a.akamaihd....0x720/1001011_545338152168858_129569371_n.jpg

======================

Nimejiuliza hili swali nimekosa jibu, kwanini jirani zetu hapa KENYA wameweza kutoka katika hili kundi lakini sisi TANZANIA tumeshindwa ilihali sisi tuna fursa nyingi kuliko wao?!!,

ZIKO WAPI NCHI MASKINI SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo wao ni kama ifuatavyo.

Africa (33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;

Asia (9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste na Yemen;
Caribbean (1): Haiti;

Pacific (5): Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.
Mchoro 1 – Nchi 48 za kundi la LDCs

Imetolewa na UNCTAD
--
Kutengeneza list ya LDCs
List ya LDCs inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo (CDP).
Katika mapitio ya hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:

1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)

2. Kigezo cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na kuandika

3. Kigezo cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na umbali.

source: haki ngowi blog
 
Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,429
2,000
Juzi Zitto Kabwe aliulizwa hili swali kwanini sisi ni masikini, akajibu ni Kwasababu viongozi wetu wamechagua tuwe masikini.
Lakini Zitto na wewe si kiongozi mwenye dhamana ya jimbo?!, unapimaje umasikini wa wananchi katika jimbo lako!
 
Last edited by a moderator:

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,364
2,000
Tanzania ndio masikini wa mwisho kabisa duniani kwakuwa rasilimali tulizonazo haziendani na mahala tulipo.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Leo katika Gazeti la Majira nimekutana na Repoti hii.
UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).

Ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012 iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kutoka Geneva, nchini Uswisi, ilisema idadi ya watu waliohamia Ulaya kutoka nchi maskini sana (LDCs) iliongezeka.

Ongezeko hilo ni kutoka watu milioni 19 mwaka 2000 hadi milioni 27 mwaka 2010, sawa na asilimia 3.3 ya wakazi wote wa nchi hizo.

Kwa mujibu wa ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012, iliyotolewa na UNCTAD, ilisema nchi maskini sana duniani zinatoa asilimia moja ya wahamiaji duniani kote.

Imesema wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs, wanaishi katika nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).

“Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda katika nchi zao, kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011, kutoka dola bilioni 3.5 hadi bilioni 27.

“Mwaka 2011, kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada milioni 3.2 na kutoka Kenya milioni 2.5,” ilisema taarifa hiyo.

Fedha zilizotumwa kwenda LDCs, zilikuwa mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI).

Nchi maskini zilizotajwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar na Malawi.

Nyingine ni Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Tanzania, Zambia, Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste, Yemen, Caribbean, Haiti,
Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu

My Take!
Hivi nchi hii tujiringanishe na Kenya tu ambao hawapo miongoni mwa nchi masikini walichotushinda ni nini kwa upande wa Rasilimali, Hapa naona viongozi waliopo madarakani wanacho cha kujibu kwa nini Tanzania kwa wingi wa Rasilimali tulizonazo bado ni Masikini, Hii ni aibu kubwa sana jamani.
 
Savannah

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
239
0
Tuna umaskini wa viongozi. Tuiondoe CCM 2015 na hatutawa tena kwenye orodha ya inchi maskini.
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,054
2,000
Tuna umaskini wa viongozi. Tuiondoe CCM 2015 na hatutawa tena kwenye orodha ya inchi maskini.
iacheni sisiem ipumuwe,iko kwenye mpango mkakati na upepuzi yakinifu wa kuiondoa nchi kwenye hiyo orodha tuendelee kuiamini na kuichagua kila chaguzi
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,071
2,000
inatia hasira sana,rasilimali zote hizi,vizazi vijavyo aviwez kutusamehe kwa ili,hii takuwa laana si bure,shame
 
kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
2,883
2,000
iacheni sisiem ipumuwe,iko kwenye mpango mkakati na upepuzi yakinifu wa kuiondoa nchi kwenye hiyo orodha tuendelee kuiamini na kuichagua kila chaguzi

HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! MARIRE HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,530
2,000
NAPE,LE MUTUZ,RITZ mmeiona hii report?uchumi wetu huanza saa 2 asbh na kufungwa saa 10jioni!hakuna kulima,bank,usafiri
 
MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,050
1,225
Ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee miaka 50 ya uhuru oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee 2015 ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,304
2,000
Haiwezekani Tanzania kuwa masikini kuna wasomi wengi sana...
 
manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,069
2,000
Ningeshangaa kama isingekuwa kwenye hii nafasi,Kweli kuna aliekuwa na mtazamo tofauti na matokeo haya jamani?
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,054
2,000
Haiwezekani Tanzania kuwa masikini kuna wasomi wengi sana...

ritz kweli we kiza kama ilivyo ccm ,wasomi ndio wanaotuibia karume hakuwa msomi ila alileta maendeleo znz.sasa mwangalie yule mpare profesa maghembe amesaidia nini nchi hii?wewe mwenyewe usomi wako badala ufanye kazi unashinda jf unaandika upuuzi tu
 
Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,458
2,000
Nchi ni maskini ila viongozi wetu ni matajiri mpaka hela zimewazidi wameficha uswiss
 
pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,584
1,500
:laser::target:.......... Alah kumbe.... Tanzania ni nchi yenye madini ambayo hayapatikani duniani kote.... Tanzanite, almasi, dhahabu, makaa ya mawe, gasi, mafuta, mbuga za wanyama, mito, mlima mrefu kuliko yote barani africa kilimanjaro vingine ongezea wewe.......................:majani7: :fencing: :A S 100: :cheer2:
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom