Takwimu za Umasikini; Tanzania tunaonewa au ni kweli?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimetembelea mtandao [ame=http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_percentage_of_population_living_in_poverty]List of countries by percentage of population living in poverty - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]
nikitaka kujua nchi ambazo wananchi wake wengi wanaishi katika umasikini wa zaidi wa kipato. Ukweli ni kuwa nimeshangazwa sana kuona nchi yetu ni nchi masikini zaidi kuliko zote zilizowekwa hapo.

Viongozi wetu kila siku wanajisifu kwa maendeleo yaliyopatikana tangu tupate uhuru! Katika takwimu nilizopata Tanzania ni ya mwisho i.e watu wengi zaidi wanaishi katika umasikini mkubwa kuliko nchi za DR Congo, Burundi, Chad nazote unazozijua wewe. Cha kushangaza zaidi ni kuwa Viongozi wetu ndo watumiaji wazuri wa fedha za umma na ndo wanaotoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji na kuruhusu raslimiali zetu ziporwe mbele ya macho yetu.

Yawezekana katika mtandao huu tumeonewa, naomba wenye takwimu mbadala watoe ili tujue uhalisia wa mambo kama kweli tu masikini sana au wanatuonea tu.
 
Back
Top Bottom