Takwimu za Silicon Valley, San Francisco ,USA zimenishtua sana! Mnafanya nini USA?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kwa kweli nimebahatika kufika Silicon Valley huko San Francisco Marekani, kwa wale wasioelewa Silicon Valley ndiyo mama wa modern economy yaani hapa ndipo kilichopo Chuo Kikuu cha Stanford na waasisi wa Kampuni kubwa Duniani kama Google, Yahoo, Hewlet -Packard, Cisco n.k wote ni wahitimu wa Stanford vile vile Silicon Valley ni makao Makuu ya Kampuni ya Apple inc. na Facebook!

Sasa kilichonistua zaidi na kunifanya hata niandike haya ninayoandika ni Takwimu nilizozikuta Silicon Valley ina wakazi takribani milioni tatu (3 000 000) na kwamba theluthi moja (1/3) ya wakazi wake wamezaliwa nje ya Marekani, na Silicon Valley ni sehemu pekee yenye Waafrika weusi wachache klk sehemu nyingine yoyote ile nchini Marekani na ni asilimia 2.5 (2.5%) tu ya wakazi wote wakati asilimia 31 (31%) ni Waasia na asilimia 26 (26%) ni Walatino yaani watu wenye asili ya Bara la Marekani Kusini!

Sasa hizi Takwimu kwa kweli zimenishtua sana hata na kujiuliza watu weusi wote waliozaliwa Afrika na Marekani mnafanya nini Marekani? Kweli uwakilishi wetu Silicon Valley ni 2.5 %?
Hapo ndipo nilipoona kwamba future ya mtu Afrika bado sana kwa maana Silicon Valley ndipo muelekeo wa Uchumi wa Dunia ulipo sasa kama Waafrika tunawawakilishi wa asilimia 2.5 hii inasemanje kuhusu vipaumbele vyetu?
 
Kama ni makao makuu ya makampuni mengi ya teknolojia absi hakuna haja ya kila mtu kuwako huko.Teknolojia inaruhusu ufanyaji kazi hiyohiyo mahali popote.
 
USA baby

upload_2016-1-22_14-24-48.png
upload_2016-1-22_14-24-48.png upload_2016-1-22_14-24-48.png upload_2016-1-22_14-24-48.png
 
Silicon Valley hakuna hata vibarua vya kukatia ng'ombe majani huko tukaongezee % angalau ifike 20% ya weusi?
 
Nafikiri most of companies at silicon valley wanaprefer graduates wa stanford na sio vyuo vinavyotoa african american engineers kwa wingi kama south Carolina ..kuchezea code napo ni Tatzo wengi wa rangi yetu uengineer tunaoupenda ni kama mechanics na so on
 
Inataka shule zaidi math na science, kama sio kusoma Berkeley au Stanford ambapo serikali haina msaada kwa blacks au kama fedha hakuna huwezi fika huko
 
Back
Top Bottom