TAKUKURU yawafikisha sita mahakamani kwa uhujumu Uchumi

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, leo Jumatano Novemba 20, imewakamata na kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara sita wakiwamo raia wa kigeni kutoka nchini China kujibu mashtaka ya Rushwa na uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi), Wli Mfuru amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani kuwa ni You Hattao, Zhang Zhi Xin wote raia wa China, wengine ni John Mnyele, Loncolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro, ambao wote ni watanzania.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa saba.

Amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU na Jeshi la Polisi umebaini kuwa kampuni ya SHIN UP iliyopo Visoga-Kibaha imejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na uhujumu uchumi na hivyo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh Bilioni 1.2.

Fungua kiambatanisho kusoma habari kamili
 

Attachments

  • PRESS RELEASE SHIN UP Pg 1.pdf
    292.4 KB · Views: 2
  • PRESS RELEASE SHIN UP Pg 2.pdf
    365.7 KB · Views: 1
  • PRESS RELEASE SHIN UP Pg 3.pdf
    194.8 KB · Views: 1
Juzi waziri wa kilimo alisema kulitokea udanganyifu na ufisadi mkubwa ktk manunuzi ya korosho uliofanywa na serikali msimu uliopita.
Hakuna aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa sababu wahusika ni wafanyakazi wa serikali.
 
Back
Top Bottom