Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,112
TAKUKURU mkoa wa Shinyanga katika ufatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi, manao tarehe 29/06/2020 majira ya saa tatu usiku mtaa wa Mwasele B nyumbani kwa Joseph Jonas Tasia ilikamata doti mia sita za vitenge zenye nembo ya Chama cha Mapinduzi na vya kawaida vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria kuwa vilikuwa vinaandaliwa kutumika kufanya ushawishi kwa wapiga kura.
Aidha uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Joseph Jonas Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa magari madogo tax hana duka la vitenge wala hafanyi biashara ya vitenge.
Katika mahojiano na TAKUKURU Joseph Jonas alishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusiana na mzigo huo wa vitenge na hata risiti za manunuzi ya vitenge hivyo hazikujitosheleza.