TAKUKURU: Nassari na wenzie hawakuleta Ushahidi bali Taarifa, tunampa onyo kuongelea taarifa za uchunguzi hadharani

TAKUKURU wamesema wameshangazwa na Wabunge Nassari na Lema kuongea na waandishi baada ya kuwapa ushahidi, na walicholeta Lema na Nassari sio ushahidi ni taarifa na wanaifanyia kazi

Katika ushahidi kuna mambo mengi na wanaangalia matakwa ya kisheria, ushahidi una relevance na possibility
Sheria inataka mtoa taarifa alindwe lakini Nassari na wenzake walifanya watu kuwafahamu kwa kuongea na waandishi wa habari

Pia ametoa Onyo kwa Nassari wasiwe wanaishinikiza chombo hicho na kukiweka kwenye malumbano ya kisiasa

Amemshangaa Nassari kuuliza kwa nini hawajaupeleka ushahidi huo mahakamani mpaka sasa na kusema wao wanaongozwa na sheria ya mwenendo wa mashtaka na wakishamaliza uchunguzi watatathimini matokeo waliyoyapata na wakijiridhisha walichopewa kinakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria watafikisha katika hatua nyingine ya mwenendo wa mashtaka ya jinai na watapeleka mashataka kwa mwendesha mashataka mkuu wa serikali na ataandaa mashataka dhidi ya washtakiwa kama wapo

Uchunguzi unaweza kugundua walichopeleka ni kosa ama sio kosa, inawezekana kuna matukio yanafanyika na watu wanadhani ni makosa kumbe ni 'moral wrongs' tu amabayo yanahitaji utaratibu mwingine wa kuwashukulikia

Amemshauri Nassari kukoma mara moja kugeuza mchakato huo wa kisheria kuwa malumbano ya kisiasa

Wanamuonya Nassari asiongee na vyombo vya habari juu ya sakata la tuhuma za rushwa.
1. Kwa nini wasimuite ofisini wakamkataza jambo hilo?
2. Kwa nini na wao wanatumia vyombo vya habari kumuonya Nasari, huku wakimkataza Nasarri ambaye aliekuwa anautaarifu umma ya kinachojiri asitumie vyombo vya habari?
3. Je ukali wa maneno yaliyotumika yalistahili kwenye tukio hilo?
4. Ni wazi jambo likifika mahakamani si ruhusa tena kulijadili nje ya mahakama isipokuwa kwa kutoa mrejesho tu, je ni sawa hata takukuru pia?
5. Je nini hekima ya Taasisi kama taasisi inaposhuhulika na mtu ambaye hekima zake zinatia mashaka.
 
Nadhani maelezo ya takukuru yamezingatia vigezo vya kisheria kabsa wala hakuna siasa ila ni tafsiri potofu za wachache wenye mtazamo hasi juu ya taasisi hiyo nyeti. Takukuru piga kazi kwa mjibu wa sheria
 
Ushahidi kisheria ni ule unaokuwa umekubaliwa na hakimu au jaji.Kabla ya hapo zinakuwa ni porojo tu au maelezo .Nassari haelewi ushahidi ni kitu gani.Alichopeleka ni maelezo ya tuhuma sio ushahidi.Takukuru wako sahihi.Walichopokea ni maelezo tu ya tuhuma
Maelezo yote ni ushahidi. Isipokuwa kuna ushahidi ambao ni wa kweli na ambao si wakweli.
 
Sawa wasishinikizwe ili uchunguzi uchukue miaka 50 ili kizazi hiki kisiwepo wakati hatua zinachukuliwa.
kwa hiyo wewe unadhani wameteuliwa kukutetea wewe au kuitetea serikali? yaani kesi ya ngedere unapeleka kwa nyani? nashukuru nassari katimiza wajibu wake hayo mengine ayaache wasije kumbadilishia kibao
 
Yah Takukuru wapo sahihi...ushahidi is a matter of relevancy, probability, and admissibility... Na haya yote ni kwa mujibu was sheria ya ushahidi na ile ya mwenendo wa makosa ya jinai etc
 
kiukweli nasari kaharibu,alitaakiwa akimbize mwizi kimya kmya ila hii ya kukaa mbele ya camera sio nzuri ,ilitakiwa iwe hatua ya mwisho kabisa

lakini pia Takukuru nao wanaharibu pia kutoonyesha hata nia ya kushughulikia jambo hili
 
Ushahidi kisheria ni ule unaokuwa umekubaliwa na hakimu au jaji.Kabla ya hapo zinakuwa ni porojo tu au maelezo .Nassari haelewi ushahidi ni kitu gani.Alichopeleka ni maelezo ya tuhuma sio ushahidi.Takukuru wako sahihi.Walichopokea ni maelezo tu ya tuhuma
Sasa wao ni nani kusema haufai, si wapeleke huko mahakamani , ili mahakama ituambie!!.. watu tuwaone kwa sura zao na sauti zao wakiahidi vitu, halafu gafla iwe haina mashiko.. hv yule rwakatare wa chadema si alisumbuliwa sana na kesi ya ugaida kwa ajili ya video clip tu.!?? Tofauti ni nn!? Kwa nn wasipelekwe mbele ili wenyewe wakajibu
 
Ushahidi kisheria ni ule unaokuwa umekubaliwa na hakimu au jaji.Kabla ya hapo zinakuwa ni porojo tu au maelezo .Nassari haelewi ushahidi ni kitu gani.Alichopeleka ni maelezo ya tuhuma sio ushahidi.Takukuru wako sahihi.Walichopokea ni maelezo tu ya tuhuma

mmh sijakuelewaa...hata kidogo je wale police waliochukuliwa videos wakiomba rushwaa na kuchukuliwa hatua mara mojaa na kufungwaa jela kisheria maana yake ni nini..? au una maana nyingine ya kisheria ambayo unamaanisha sheri ni kitu kidogooooo kama mchangaa hiviii ili kusudi ukiitee "ki-sheria" acha porojoo
 
Wanamuonya Nassari asiongee na vyombo vya habari juu ya sakata la tuhuma za rushwa.
1. Kwa nini wasimuite ofisini wakamkataza jambo hilo?
2. Kwa nini na wao wanatumia vyombo vya habari kumuonya Nasari, huku wakimkataza Nasarri ambaye aliekuwa anautaarifu umma ya kinachojiri asitumie vyombo vya habari?
3. Je ukali wa maneno yaliyotumika yalistahili kwenye tukio hilo?
4. Ni wazi jambo likifika mahakamani si ruhusa tena kulijadili nje ya mahakama isipokuwa kwa kutoa mrejesho tu, je ni sawa hata takukuru pia?
5. Je nini hekima ya Taasisi kama taasisi inaposhuhulika na mtu ambaye hekima zake zinatia mashaka.

jibu ni kwamba....uhuru wa taasisi nyingi apa nchi hautambuliki vizuri au haupo kabisaaa
 
hamna kitu kama hicho,kuliko ushirikiane na chombo cha dola fanya ushirikiano na chombo kimoja wapo nyumbani kwako unaweza kupata afya boraa...maana mtu unajitaidi kufanya usafi ktk serikali yako ktk chombo iko cha dola lakini ndo wanakuchafua...sasa bora kipi apo??
 
mmh sijakuelewaa...hata kidogo je wale police waliochukuliwa videos wakiomba rushwaa na kuchukuliwa hatua mara mojaa na kufungwaa jela kisheria maana yake ni nini..? au una maana nyingine ya kisheria ambayo unamaanisha sheri ni kitu kidogooooo kama mchangaa hiviii ili kusudi ukiitee "ki-sheria" acha porojoo
Zile tuhuma ziichambuliwa kitaalamu zikaonekana sio feki zikachukuliwa Kama ushahidi wakafukuzwa. Je unamjua aliyepiga ile video ilibaki siri kati Ya takukuru na yeye. Nassari alitakiwa apeleke kimya kimya kwa kuzingatia sheria. Hajazingatia sheria ndio maana kaonywa hivi anavyojianika hao wala rushwa anaowatuhumu wakimkodia majambazi wakamtwanga risasi kwa hasira ya kuanikwa atalaumu takukuru au polisi wakati yeye mwenyewe kwa hiari yake anaijianika mazingira hatarishi kwa Maisha yake? Mlowola kamweleza kwa polite language lakini ni hatari tena kubwa yeye kujianika kwamba ndie muhusika aliyewachomea utambi. Hana akili bwege kabisa.
 
Hana namba zake za simu hadi atafute kiki mbele ya kamera?? Eti kwa siri hivi ile CCTV footage ya watu wakichukua mabilioni kwenye magunia pale stanbic kipindi cha sakata la IPTL mliifanyia kazi gani ?? Ila je ingeonyeshwa hadharani unafkiri wasingejiuzuru??? Shame on u eti kisiri mnazaa taifa la waoga mbona Rais alimtaja double agent wenu mliempandikiza ACACIA!!
 
Hata Azam; sio wabobezi wa haya mambo lakini kwenye taarifa yao ya habari, hawakukurupuka kuita hiyo kitu ushahidi kama clouds; walisema Nassari awasilisha taarifa ya tuhuma za rushwa.
 
Hata Azam; sio wabobezi wa haya mambo lakini kwenye taarifa yao ya habari, hawakukurupuka kuita hiyo kitu ushahidi kama clouds; walisema Nassari awasilisha taarifa ya tuhuma za rushwa.
Vyombo vya habari makini vilitakiwa kuripoti kuwa Nassari awasilisha taarifa ya tuhuma za rushwa. Nikwambie mashirika makubwa ya habari duniani hayaajiri Waandishi watanzania wengi sababu wako below standards hawa analyize wanareport Kama mabwege . Alichowasilisha Nassari sio ushahidi ni taarifa za tuhuma.
 
Back
Top Bottom