TAKUKURU: Nassari na wenzie hawakuleta Ushahidi bali Taarifa, tunampa onyo kuongelea taarifa za uchunguzi hadharani

Hii ni miongoni mwa taasisi zinazofuja pesa na sijawahi kuona mantiki ya uwepo wake. Hali kadhalika bunge...
Huwezi ona kwasababu wewe siyo mzalendo wa kweli maana bila pccb maendeleo 0 ni sawa kuweka maji kwenye gunia na uadilifu huu wa sasa usingekuwepo maana watumishi wa umma na sekta binafsi wangeendelea kupiga dili tu sasa hali shwari.
 
Aisee baada ya kumsikia yule jaji mwili ulisisimka ndo nikajua kama kweli faru john kesha shika mihimili yote yaani jaji naye mweupe kabisa kichwani au naye anatumikia tumbo na si taaluma
Mimi sishangai hata wenyewe walisema kuhusu hatua kuchukuliwa wana uhakika hazitachukuliwa. Ndiyo maana msemaji wa hicho chama kinachojiita cha kuzuia rushwa ameita press conference kumfurahisha mkuu lazima atetee chakula chake ili asichukue hatua zozote.
 
Kiukweli mkubwa kaumbuka sana,na usemi ule wa Zito kabwe kuwa tumewapa washamba na malimbukeni ni kweli.walidhani wapo gizani na gia zote za kusema madiwani wanafurahishwa na utendaji wa mkubwa kumbe pesa ya rushwa ilikua inatembezwa pamoja na ahadi kemkem.kiukweli mkubwa amejidhalilisha napenda kuwapa hongera hao vijana akina Nasari kwa kua wamejaribu kukomesha cheap politics za mkubwa
Mimi nashauri Nasari aweke zote YouTube kwani kwanza hao wazuiaji rushwa wenyewe hawatafanya chochote ili wananchi tujue inatosha sana.
 
Huwezi ona kwasababu wewe siyo mzalendo wa kweli maana bila pccb maendeleo 0 ni sawa kuweka maji kwenye gunia na uadilifu huu wa sasa usingekuwepo maana watumishi wa umma na sekta binafsi wangeendelea kupiga dili tu sasa hali shwari.

Naomba uwe unachukua muda kusoma na kutafakari kilichoandikwa kabla ya kuanza kuanfika.

Kwanza, natilia shaka uelewa wako wa uzalendo. Nikikuuliza hiyo PCCB imeanzishwa awamu hii ya tano au ilikuwepo toka awali?

Kwa mujibu wa maelezo yako, unasema uadilifu na kupiga deal sasa hivi na haya maendeleo ni kutokana na PCCB...sasa walikua wapi awamu zilizopita? Unaweza kunipa mafanikio 2 tu ya PCCB? Maendeleo kwako ni pamoja na kusema Moral wrongs kabla hata haujafanya uchunguzi?
Tofautisha uzalendo na kukaa kimya bila kuhoji mambo kwa hofu.
 
Yes kwasababu limetendwa na x, that's y ni moral wrong, lingekua limetendwa na y, habari ungeikuta FrontPage, Director wa Takukuru kaibwatukia mwenyewe..... aibu kwa law enforcement agencies za Tanzania.....Aibu...

Must consider attitude of the law enforcer (intention to prosecute).
 
TAKUKURU wamesema wameshangazwa na Wabunge Nassari na Lema kuongea na waandishi baada ya kuwapa ushahidi, na walicholeta Lema na Nassari sio ushahidi ni taarifa na wanaifanyia kazi

Katika ushahidi kuna mambo mengi na wanaangalia matakwa ya kisheria, ushahidi una relevance na possibility
Sheria inataka mtoa taarifa alindwe lakini Nassari na wenzake walifanya watu kuwafahamu kwa kuongea na waandishi wa habari

Pia ametoa Onyo kwa Nassari wasiwe wanaishinikiza chombo hicho na kukiweka kwenye malumbano ya kisiasa

Amemshangaa Nassari kuuliza kwa nini hawajaupeleka ushahidi huo mahakamani mpaka sasa na kusema wao wanaongozwa na sheria ya mwenendo wa mashtaka na wakishamaliza uchunguzi watatathimini matokeo waliyoyapata na wakijiridhisha walichopewa kinakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria watafikisha katika hatua nyingine ya mwenendo wa mashtaka ya jinai na watapeleka mashataka kwa mwendesha mashataka mkuu wa serikali na ataandaa mashataka dhidi ya washtakiwa kama wapo

Uchunguzi unaweza kugundua walichopeleka ni kosa ama sio kosa, inawezekana kuna matukio yanafanyika na watu wanadhani ni makosa kumbe ni 'moral wrongs' tu amabayo yanahitaji utaratibu mwingine wa kuwashukulikia

Amemshauri Nassari kukoma mara moja kugeuza mchakato huo wa kisheria kuwa malumbano ya kisiasa



Dawa ya Mlowola ni moja tu ni kwa Nassari kumwaga video zote mitandaoni ili wananchi wajue wazi PCCB ni tawi la CCM na halina nia ya kupambana na rushwa
 
Back
Top Bottom