TAKUKURU mmenidhalilisha na kunisingizia

TAKUKURU mmenidhalilisha na kunisingizia

Wakipatikana watu 100 tu waliotumiwa huo ujumbe, wakapeleka kesi ya madai, kila mmoja akadai Shs. 100,000,000 kama fidia kutoka kwa kampuni za simu na TAKUKURU, hapo watashtuka. Kwanza watashindwa kesi, pili wataacha ufisadi huo!

Tuzinduke. Haki zetu zinapokwa kila siku. Wadau JF mnauweza mkakati huu? Wanasheria wapo wa kushindania kesi hii!

In legal terminology, this is a TORT! (Definition: Definitions)

Nadhani tutaweza kuanzia hapo. Kabla ya kuchukua hatua, ULIZA, JIFUNZE, TAFAKARI!

Mwana wa Haki
 
sijawahi kuona upuuzi kama ule.....mfano mdogo ni wakati wa kura za maoni juzijuzi.....yaani huwezi kutenganisha rushwa na maisha yetu ya kila siku ,ndiyo system at work!!!!!!yaani ni kama vile umwambie mtu aishi bila pumzi....mnacheza kwelikweli.....ITS JUST IMPOSSIBLE..HUWEZI KWENDA KINYUME NA MFUMO....mfano mwingine mdogo ..pamoja na Kandoro kufunga ofisi za ardhi za manispaa zote Dar es Salaam,na kuwahamisha wafanyakazi wote na kuwaleta wapya wengine kwa sababu ya rushwa....leo zimefunguliwa...sasa ukienda kichwakichwa ukitarajia huduma bila chochote thubutu!!!!! hakiyamungu hupati huduma bila kueleweka!!!haya yamenikuta just two weeks ago..ukisema uwakamatishe sometimes ni wastage of time ,muda hakuna,siyo mkazi wa hapo,hivyo gharama zitaongezeka nk...na hivyo hutakiwi kushangaa,MAMBO yanatakiwa yaende fasta,kazi ya siku moja imeshakaa miezi miwili,unafanyaje???....JIBU HUU NI MFUMO KAMA DAMU NA MISHIPA MWILINI,...MSIANZIE KWENYE MATAWI,MNGECHEKI NA MIZIZI YENYEWE IKOJE??.....na hii mnaijua....anyway endeleeni kututumia meseji sometimes simu zetu nazo zinakaa idle muda mrefu.....
 
Mlisajiri number zenu za simu koooote Bongo sasa tunalalamika nini jamani?Tanzania yetu ni zaidi ya tuijuavyo....Huo usajiri wa manumber mie sijui kama utafaualu lengo lake ambalo mpaka leo silijui maana Bongo kwanza watu hatuna hata resident card(Vipande kenya wanaita) halafu tusajiri minumber,kazi kweeeeeli
 
Nawashauri TAKUKURU kama chombo cha uchunguzi kitayarishe master list ya simu za watoaji na wapokeaji wa rushwa; halafu wawatumie hao. Nimeshangaa mimi kwa raha zangu niko baa napata moja baridi moja moto na familia, mara message hiyo, kuisoma nkuta ujumbe huo toka TAKUKURU, nikashangaa na nikawakemea washindwe na walegee.
 
Tatizo kubwa hapa ni kampuni za simu kuruhusu kampeni/matangazo mbalimbali kupelekwa kwa wateja wao - sijui ni uroho wa pesa? kwani mauzo ya airtime hayawatoshi? Inakera mno. Hata wenyewe kampuni za simu mara nyingi husambaza meseji za kuchosha.
 
Kaka sema tu nikuunganishe na mwanasheria wangu gerald hongoli akusaie kudai fidia za kuchafuliwa jina.
msg yenu mliyonitumia leo kwenye simu yangu yangu ya mkononi imenidhalilisha na kunisononesha sana kwa kuwa mmenisingizia kuwa mimi ni mtoaji na mpokeaji wa rushwa, na mtanibangoja nikutafutie mwanasheria wa kukusaidia kwa kweli hii meseji ni ya kijinga sana na imeudhalilisha utu wangu kwani sijawahi kuyatenda yote hayo mawili, kupokea na kutoa rushwa.
Naomba muache mara moja kusambaza kwa watu msio wafahamu huo ujumbe wenu.
Kama mko katika harakati ya kukemea na kuzuia rushwa, jaribuni kutumia maneno ya kiungwana na yaliyo polite, ambayo hayasingii mtu, wala kumuharibia credibility yake kwenye society.
Naamini mmenielewa na kosa hilo hamtolirudia kwa mtu mwingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom