Yaliyojiri kwenye uzinduzi wa TAKUKURU wa kampeni ya kupambana na rushwa barabarani (UTATU)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,875
IMG-20191031-WA0011.jpg

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) leo inazindua Kampeni ya kupunguza ama kutokomeza kabisa rushwa Barabarani.

Kampeni hii ina malengo mahususi manne, ikiwa kila lengo linatakiwa kutekelezwa na kila mdau kwa nafasi yake:

* Kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa wasimamizi wa sheria za barabarani

* Kuandaa mkakati wa kuzuia vitendo vya rushwa barabarani

* Kushirikisha Umma kuzuia vitendo vya rushwa barabarani

* Matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani ambapo uazinduliwa Mfumo wa (Mobile App) utakaozinduliwa pamoja na Kampeni hii ya UTATU, utapakuliwa kutoka Play Store au App Store ya simu ya mkononi kisha mtu ataweza kupiga picha za video, mnato au sauti na kuzituma TAKUKURU.

UTATU inamaanisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wadau

Uzinduzi unafanyika Katika viwanja vya Manazi mmoja Dar Es Salaam kuanzia saa tatu kamili Asubuhi. Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Zaidi somab

Karibuni.

Kauli Mbiu: Kwa Usalama wetu, Kataa Rushwa barabarani.

======

UPDATES:
IMG_20191101_091400_9.jpg

09:00hrs: Maandamano kutoka Ofisi za Kikosi cha Usalama Barabarani hadi Viwanja vya Mnazi. Watu wanazidi kuwasili

0933hrs: Anawasili Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika ambaye ndo Mgeni rasmi aliyemuwakilisha Waziri Mkuu Majaliwa. Na sasa anapokea Maandamano.
IMG_20191101_094043_8.jpg

09:42hrs: Baada ya maandamano kupokelewa, sasa unaimbwa wimbo wa taifa

0946hrs: Maombi yanaendelea kutoka kwa viongozi wa Madhehebu Mbali mbali. Aliyewakilisha dini ya Kikristo, kanukuu kitabu kutoka kitabu cha kutoka. Kutoka 23:8 Usipokee rushwa, maana rushwa huwapofusha wakuu na kupotosha mambo ya wenye haki.

1000hrs: Baada ya Kikundi cha tabasamu, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Mjema, anawasilisha salamu za Mkuu wa Mkoa Dar ambaye hajaweza kufika.

Baada ya Salaamu Mjema anawakaribisha Wageni wote katika Wilaya ya Ilala na Dar. anaongeza Kwamba katika kipindi cha mwezi mmoja viongozi wa Ilala Wamezunguka kata 39 na mitaa 159 ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kushughulikia maswala ya Rushwa. Club za kupinga rushwa 602. Kinondoni 252 zipo Temeke 171 Ilala 179.
IMG_20191101_100309_2.jpg

1010hrs: Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bi. Sabina Seja.

Baada ya salaam anaanza kwa kutambulisha meza kuu.

Seja anasema;

Lengo la hii kampeni ni kuwashilikisha Polisi, Wadau na TAKUKURU. Lengo kuu iliwa kuzuia rushwa barabarani kwa ushirikiano bila kumnyoshea mtu yoyote Kidole.

Ajali barabarani zinasababishwa na Miundo mbinu mibovu, sheria mbovu, uzembe nk.

Tutafurahi endapo kila mdau atashiriki. Tuliamua kutengeneza mfumo wa takukuru App mtu akaweka kwenye simu yake. Mfumo umetengenezwa na Wakala wa Serikali Mtandao.
IMG_20191101_101148_9.jpg

Tunanshukuru Mkuu wa Polisi, wakala wa Serikali na wote waliohusika katika kampeni hii.

Tukio hili la uzinduzi limekutanisha wadau kutoka sekta ya umma binafsi, kiraia, vyombo vya habari, wananchi nk.

Vitendo vya rushwa vinafanya watu kupindisha barua. Mtu anaingiza gari bovu barabarani akikamatwa anaanza kujitetea ili atoe rushwa. Lakini mwisho wa siku linaweza garimu maisha.

Wamiliki wa vyombo vya barabarani hawatoi mikataba hivyo kufanya dereva awe na mawazo awapo barabarani. Vipo vyanzo vingi. Wazo hili lilianza mwaka 2018 na leo tunazindua. Asanteni sana.

1026hrs: Mkuu wa Polisi Simon Sirro anaongea.

Napongeza juhudi za Rais wa awamu ya tano katika kupambana na Rushwa. Kila kukicha tunafanya ubunifu ili kuunga mkono juhudi hizi.

Novemba 2017 ndo Mchakato huu ulianza tukaona bila huu utatu mtakatifu hatuwezi fika popote. Tukaona tukifanya kazi pamoja tutaweza punguza rushwa na ajali. Sasa tunazindua, kinachofuata ni vitendo. Hili ni jukumu letu kwa pamoja.

Ajali zimepungua kwa 57%. Vijana wetu kule barabarani wakifanya ndivyo sivyo tumekuwa tukichukua hatua. Nawashukuru wadau welevu wanaotupa taarifa.

Swala la tehema ni muhimu sana. Hii inasaidia kupunguza rushwa.

Nitumie fursa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael. Francis Michael

1038hrs: Mshehereshaji anamuomba Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum. Aje kusalimia Kabla ya Michael. Sheikh anaongea na kuomba msamaha kwa kufika kwa kuchelewa. Anasema.

Vitabu vitukufu Quran amewazungumzia wayahudi mabingwa wa kura rushwa. Waliweza kuwasaliti manabii na mitume mbali mbali. Rushwa ni Jambo la haramu. Rushwa ni dhuruma. Mtume Mohamad mwenye kura rushwa na mwenye kutoa rushwa na yule mpambe wa katikati wote ni motoni

Asiwepo mtoaji, mpokeaji na mtu wa katikati. Wasipokuwepo rushwa haitakuwepo.

1044hrs: Watu wanaburudika na Msanii Mrisho Mpoto.

1054hrs: Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael. Anasema

Kazi yangu ni ndogo, kukukaribisha mgeni rasmi kutuzindulia hii kampeni ya Utatu, lakini kabla ya kuzindua

Baada ya Salaam namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutukutanisha leo.

Nakushukuru Mgeni rasmi kwa kuweza kukubali Mwaliko wetu na wote walioitikia wito wa Mwaliko wetu.

Nawashukuru Wote waliofanikisha hii kampeni hii ya Utatu na Wadau waliofika23 Oct 2019 Katika Bwalo la Polisi Oysterbay katika kujadiliana juu ya huu utatu.

Tunafurahishwa na dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya tano ya kupambana na rushwa ambayo ni moja ya ahadi ya CCM kwenye kampeni za 2015.

Rais Magufuli amepambana na rushwa hadi kuwezesha Kuondoa wenye vyeti feki, watumishi hewa elimu bure, ununuzi wa ndege, upanuzi wa bandari, Viwanja vya ndegenk, haya ni baadhi ya mambo aliyo yasimamia Maghufuli. Hii miradi inaendeshwa na fedha za ndani.

Rushwa inaweza ikafanya nchi isifike Uchumi wa kati wa viwanda. Ulemavu, upotevu wa nguvu kazi nk.

Taasisi mbalimbali za kitaifa zimetoa taarifa zao na kuonesha Tanzania inafanya vizuri katika kupambana na rushwa. Na CPI imeonesha kuwa 2015 hadi 2018 imepanda hatua 18 katika kupambana na rushwa

Utafiti wa Twaweza wa mwaka 2017 pia ulionesha rushwa imepungua.

Katika Afrika Mashariki, Tanzania ni ya pili katika kupambana na rushwa ya kwanza ni Rwanda.

Vitendo vya rushwa vimekuwa vikichafua taswira ya nchi yetu. Tushirikiane kuitokomeza.

Nakukaribisha rasmi utuzindulie kampeni hii ya utatu. Karibu sana.

11:09hrs: Mkuchika anasema.
IMG_20191101_111039_3.jpg

Leo nmesimama hapa kusoma hotuba ya Waziri mkuu. Anakusalimuni sana. Taasisi ya kupambana na Rushwa ipo katika Wizara yangu. Amemkaribisha Mbunge Rwekiza ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya utawala Serikali za mtaa asalimie.

Pia amemkaribisha Mbunge Mwanne Ismail Makamu mwenyekiti wa kamati ya Utawala bora Serikali za mitaa.

Anasoma hotuba ya Waziri mkuu,

* Kampeni hii itakuwa na mchango mkubwa katika kutoa taarifa na kuzuia rushwa barabarani.

* Tunawashukuru wadau wetu wa maendeleo kwa kukubali kufadhili mradi huu na wadau wengine wote. Dhamila hiyo ya ushirikiano katika kuandaa kampeni umeonesha kila mmoja anavyokerwa na rushwa za barabarani. Ajali za barabarani zinasababishwa na mambo mbalimbali na ni swala mtambuka ambalo kila mmoja wetu anapaswa kushiriki.

* Kisheria jukumu la kuzuia na kumbambana rushwa ni la takukuru lakini hili jukumu kila mmoja anapaswa kubeba jukumu hili. Vitendo vya rushwa vinafanyika sehemu tulipo, tunapofanyia kazi, barabarani na popote tulipo. Maswala ya rushwa pale ajali inapotokea haibagui nani anahusika na nani hahusiki.

Tangu kuingia madaraka 2015 serikali ya awamu ya tano imejipambanua katika kupambana narushwa. Rushwa ni adui wa maendeleo, rushwa ni adui wa haki.

Rushwa ikikithiri, Serikali haikusanyi mapato ya kutosha. Hivyo huduma kama za maji na hospitali zinakosekana.

Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kugharamia wahanga wa ajali na kurekebisha miundo mbinu iliyoharibiwa.
Inakadiliwa kwa upande wa afrika inapunguza 1% ya pato la taifa kila mwaka.

Kwa mjibu wa takwimu ajali za barabarani zimeanza kupungua kwa mwaka 2018/2019.

Kampeni hii inaenda kuboresha kuzuia ajali za barabarani. Serikali itaendelea kutekeleza ilani ya CCM ya 2015 kwa kuendelea kuimarisha TAKUKURU. Hivyo wananchi endeleeni kuwa na imani na Serikali yenu.

Tanzania imeendelea kuwa mfano wa kuigwa katika kupambana na Rushwa na Ufisadi. Benki ya dunia ilitamka wazi kwamba wanatambua jinsi tanzania inavyopambana na rushwa. Mafanikio hayo ni ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.

Vitendo vya rushwa barabarani vianchafua taswira ya Nchi yetu.

Tumefanikiwa kuongeza kwa kodi, uwajibikaji na uwajibishwaji kwa watumishi wa umma. Matumizi mazuri ya fedha za maendeleo.

Bado tunayo mapungufu katika Sheria na matumizi sahihi ya barabara. Serilali itaendelea kuyafanyia kazi mapungufu hayo. Tukicheka na wala rushwa tutarudishwa nyuma.

Sasa watu wanajua umuhimu wa kudai risiti na kutoa risiti pale unapouza au kununua kitu.

Nawashauri TAKUKURU kufanyia kazi kwa haraka taarifa watakazo kuwa wanapokea. Na wananchi tusitumie fursa hii kukomoana na kutoa taarifa za uongo za rushwa. Ila tuwe wajasiri kwa kutoa taarifa za rushwa barabarani tunapokutana nazo.

Tarehe 24 anov 2019 kutakuwa na upigaji kura wa Viongozi wa Serikali za mitaa 19, 681, 259, 000 asilimia 89 ya matarajio. Uwandikishaji wa mwaka huu umekuwa wa mafanikio. 29 Oct hadi 04 Nov 2019 ni siku zankuchukua na kurudisha fomu kutoka vyama mbalimbali.

Nawaomba watanzania mkajitokeze kupiga kura.

Natoa rai kwa wadau wetu kusaidia gharama au fursa za matangazo na machspisho kuhusu elimu ya rushwa na madhara yake. Muweke ujumbe unaokemea ajali za barabarani kama mchango wenu katika kutokomeza ajali.

Uzinduzi huu unaambatana na kuzindua mfumo wa kutoa taarifa kwa simu za mkononi kupitia App ya TAKUKURU. Tuendee kuishi na kauri mbiu ya kampeni.

Sasa natamka kampeni hii sasaimezinduliwa rasmi, asante sana kwa kunisikiliza. Amemaliza kuisoma hotuba ya Waziri mkuu 1140hrs
 
Hilo tamasha usishangae wakisema ni mafanikio katika kupambana na rushwa. Sidhani kama kunahitajika tamasha katika kupambana na rushwa iliyo wazi, zaidi ya kuamua kupambana nayo kwa dhati.
 
... kipi bora? Kulipa 30,000 au kutoa hela ya brush 5,000 au 10,000 ukasepa zako? Hivi unatoka Dar kwenda Mbeya, Arusha, Mwanza, n.k. utatoa elfu thelathini ngapi? Tena makosa mengine wala hayastahili kuitwa makosa!

Waache kutumia nguvu nyingi bila sababu; wakitaka tatizo la rushwa liishe kabisa kwanza sio kila kosa ni la kulipisha faini; mengine ni ya kuonywa au kuelekezwa tu na ndio kazi ya trafiki. Umeonywa au kuelekezwa mara kadhaa hutaki kubadilika ndipo hatua ya faini ifuate - TEHAMA inaweza kusaidia kwenye hili; mfano dereva ndani ya wiki moja ana maonyo 5 say, automatically aingiziwe bili ya 100,000 kwenye akaunti yake.

Faini; kama nilivyotangulia kusema ni wachache wata-opt kulipa 30,000 badala ya 5,000 kumalizana na trafiki. Kuondoa tatizo hili, faini zipunguzwe - ziwe 5,000 kwa mfano hapo hutokaa usikie rushwa barabarani. TEHAMA inaweza kusaidia pia kwenye hili kwamba kwa mfano, ukionekana wewe ni sugu wa faini say ndani ya wiki moja umepigwa elfu tano tano mara 5 then automatically kwenye akaunti yako unaingiziwa bili ya 150,000 (mfano). Kwa utaratibu huu rushwa za barabarani kwisha badala ya kutumia nguvu nyiingi unnecessarily.
 
Naona wanataka traffick wakabet. Kha jamani vyakufutia viatu tu si mbaya
 
Wewe inaelekea ni dereva mvunja sheria sugu. Siku zote lengo la faini ni ku-discourage mkosaji kutenda makosa. Ikiwa watashusha kiwango ina maana madereva watakuwa hawaogopi kutenda makosa. Kwanza jambo la kwanza la kukubali ni kuwa uendashaji wa magari barabarani wa Tanzania ni mbovu sana. Madereva hawajali kufuata sheria. Polisi wanatumia hii loophole ya uendeshaji mbaya kuchuma fedha. Tukirudi kwenye sheria za barabarani, ni kweli, kuna sheria nyingine zinakera. Jambo ambalo wanatakiwa kulifanya sambamba na huu uzinduzi ni kusikiliza maoni ya madereva na polisi ili kubadili sheria baadhi ya sheria. Watilie mkazo kwenye speed na vitu vinavyosababisha ajali mara kwa mara.
 
Pia wakumbushe wasisahau kumpa support CAG ili kutokomeza rushwa serikalini.
Nalog off
 
Sidhani kama traffic wataacha kupokea rushwa katika nchi hii. Hasa kwa traffic wa Iringa na Mbeya.
Kibwengo Alishaambia Wachukue Kwa Kuwa Ni "Pesa Wanazochukua Traffic Ni Pesa Za Kubrush Viatu"
 
Wewe inaelekea ni dereva mvunja sheria sugu. Siku zote lengo la faini ni ku-discourage mkosaji kutenda makosa. Ikiwa watashusha kiwango ina maana madereva watakuwa hawaogopi kutenda makosa. Kwanza jambo la kwanza la kukubali ni kuwa uendashaji wa magari barabarani wa Tanzania ni mbovu sana. Madereva hawajali kufuata sheria. Polisi wanatumia hii loophole ya uendeshaji mbaya kuchuma fedha. Tukirudi kwenye sheria za barabarani, ni kweli, kuna sheria nyingine zinakera. Jambo ambalo wanatakiwa kulifanya sambamba na huu uzinduzi ni kusikiliza maoni ya madereva na polisi ili kubadili sheria baadhi ya sheria. Watilie mkazo kwenye speed na vitu vinavyosababisha ajali mara kwa mara.
Lengo La Ile Faini Ni Kukusanya Pesa.

Na Ndio Maana Imewekewa Mazingira Ya Kulipwa.

Kama Kweli Gari Lina Tatizo Kwanini Traffic Waliache Liendelee Na Kazi Ya Kuwatafutia Hiyo Tsh 30,000 Ndani Ya Wiki Badala Ya Kulipark Mpaka Lifanyiwe Marekebisho Au Dereva Awe Huru ?
 
Narudia tena tena. Lengo kuu la adhabu yoyote inayotolewa kwa mkosaji popote duniani siyo faida. Lengo lake ni kuwafanya watu wasitende makosa. Ukishapigwa faini ni juu yako kuamua kulipaki gari mpaka litengemae au kuendelea kuwa kichwa ngumu ukumbwe tena na mkono wa sheria. Najua ni vigumu sana kubadili mind set za madereva wa Bongo wakubali kuwa unaweza kuendesha gari kistaarabu bila kufanya makosa. NB: Sipingi kuwa polisi nao wana share yao ya lawama.
 
Wakiweza huko wahamie kwa Hawa watu wanaokamata magari eti "wrong parking"
 
Narudia tena tena. Lengo kuu la adhabu yoyote inayotolewa kwa mkosaji popote duniani siyo faida. Lengo lake ni kuwafanya watu wasitende makosa. Ukishapigwa faini ni juu yako kuamua kulipaki gari mpaka litengemae au kuendelea kuwa kichwa ngumu ukumbwe tena na mkono wa sheria. Najua ni vigumu sana kubadili mind set za madereva wa Bongo wakubali kuwa unaweza kuendesha gari kistaarabu bila kufanya makosa. NB: Sipingi kuwa polisi nao wana share yao ya lawama.
Kaka mkubwa,unatumia nguvu nyingi kuelezea kazi ya fine.Ma-Trafic Police wameruhusiwa kupata hela ya ku-brush viatu na Mkubwa,hamuoni mnapoteza mda na fedha?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom