TAKUKURU kutoa elimu ya rushwa ya ngono mtaa kwa mtaa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kitengo cha Kupambana na Rushwa ya Ngono, imesema imejipanga kuanza kutoa elimu mtaa kwa mtaa ili kuhakikisha inawafikia watu wa rika zote.

Mkurugenzi wa Idara hiyo, Janeth Mawinza, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipofungua kikao cha mgawanyo wa majukumu na wadau mbalimbali katika taasisi hiyo pindi watakapoanza kutoa elimu hiyo.

"Leo (jana) tumeitana hapa na ninyi wadau katika taasisi hii ya kupambana na rushwa ya ngono ili kupeana mikakati ya kuanza kutoa elimu hii mtaa kwa mtaa, tutaanzia Wilaya ya Ilala siku ya Ijumaa," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema rushwa ya ngono ni hatari zaidi ya rushwa ya kawaida kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwa mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kifo.

"Tumejitoa kukomboa hiki kizazi ambacho kinaonekana kuanza kupotea kwa sababu ya rushwa ya ngono, rushwa hii ni hatari na inaua, ukiachana na kuua, pia inamweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa hatarishi kama kaswende, na gono sambamba na kumharibu mtendwa kisaikolojia.

"Kikubwa tunaomba ushirikiano wa kutosha pindi mtakapoona tunapita mtaani kutoa elimu, tuna mambo mengi ambayo tunatamani jamii ijue juu ya hii rushwa ya ngono hasa kwa hawa wanafunzi na watoto wa kike ambao ndiyo wahanga wenyewe," alisema.

Ofisa kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi Ilala, Christina Onyango, alisema wako bega kwa bega na taasisi hiyo kuzuia rushwa ya ngono.

"Sisi Jeshi la Polisi kitengo hiki cha kupambana na hii rushwa, tunalo dawati letu la kushughulika na watu wanaokumbwa na adha ya rushwa ya ngono sambamba na kuwashughulikia watu wanojihusisha kuomba rushwa ya ngono," alisema

IPP MEDIA
 
Maisha haya, ndugu zangu, balaa! Jambo linakuzwa ili kitengo kiendelea kupiga manoti ya kodi za walalahoi.
 
Ukifanya utafiti ktk maofisi mbalimbali lazima utakutana wasichana kadhaa walio pata KAZI au kupandishwa cheo Kwa rushwa ya ngono. Wana wake wengi wana nyanyaswa kingono na mabosi wao lkn wamekaa kimya ili waendelee kunufaika na matunda ya kazi.
TAKUKURU toeni elimu lkn pia fanyeni uchunguzi ktk maofisini wana wake wana nyanyasika sana
 
Kuna kitu wanakosea sana, hasa kimtizamo!

Rushwa ya ngono ni kama rushwa ya pesa, huombwa na kutolewa na jinsia zote.

Hapa naona kama wanaoonekana ni wanufaika wa rushwa hii ni wanaume pekee, wakati mimi mwenyewe nimepokea sana rushwa za ngono, lakini sijawahi kuomba hata siku1 nilikuwaga nashawishiwa!

Sasa ninapoletewa rushwa ya aina hiyo kwa kushawishiwa, hapo mnufaika si mimi ni yule aliyeileta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wengi maofisini ndio wahanga wa rushwa ya NGONO......hawasemi lkn ukweli ndio huo.....wanawake walio wengi wameajiriwa au wamepandishwa vyeo baada ya kufanya ngono Na boss, yamo kila ofisi Na wanajulikana, kila boss ana mzigo wake ofisini.
 
Fanyeni uchumguzi kwenye taasisi ZA serikali Na mashirika binafsi lkn haswa taasisi ZA ser
 
Back
Top Bottom