TAKUKURU Ilala yaokoa Tsh. Bilioni 1.1 zilizokusanywa bila kuwasilishwa Benki

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1690976729103.png

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ilala, imefanikiwa kuokoa Sh1.13 bilioni ikishirikiana na taasisi nyingine.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini hapa, Mkuu wa Takukuru Ilala, Sosthenes Kibwengo amesema fedha hizo ni za umma ambazo zilikusanywa bila kuwasilishwa benki kwa muda mrefu na nyingine ni kodi iliyokwepwa kwa kutoa taarifa za uongo.

"Tunawakumbusha wote wenye majukumu ya kukusanya mapato mbalimbali ya Serikali, kuyawasilisha benki kwa wakati na kujiepusha na matumizi ya fedha mbichi (ambazo hazijaidhinishwa)," amesema Kibwengo katika taarifa ya robo mwaka, Aprili hadi Juni.

Pia taasisi hiyo imebaini kasoro za ujenzi, usimamizi na manunuzi katika ukaguzi wa miradi 13 ya maendeleo katika sekta za afya, ujenzi, elimu na huduma za jamii ambapo imesimamia kurekebishwa kwa kasoro hizo.

"Tumeanzisha uchunguzi kuhusu mradi mmoja wa ujenzi katika bustani ya kupumzikia ya Mnazi Mmoja, wenye thamani ya Sh690 milioni ili kujiridhisha iwapo gharama zilizotumika zinarandana na kazi iliyofanyika," amesema.

Aidha mafanikio katika kupanua wigo wa washiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa yameelezwa kupatikana kupitia programu ya Takukuru Rafiki katika kata Mnyamani, Kinyerezi, Buguruni, Segerea na Mchafukoge.

"Tunapenda kuwashukuru madiwani wa kata hizo, watendaji wa kata, wadau Na wananchi walioshiriki kuibua kero na pia tunazishukuru taasisi za umma Kwa kufanyia kazi kero zilizoibuliwa na kushiriki kutoa mrejesho kwa wananchi," amesema.

Kibwengo ameeleza mikakati ya taasisi hiyo katika mkoa huo kwa robo mwaka ya Julai hadi Septemba kwamba imejikita katika miradi ya maendeleo na uelimishaji wa makundi yasiyo rasmi kupitia mikusanyiko na vipindi vya redio.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom