TAKUKURU, Bila Kuchunguza hii Rushwa ya Bunge, bora ivunjwe

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.

Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.

Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.

Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.

Kufuta aibu hii ya kitaifa TAKUKURU watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.

Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe?

Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?

TAKUKURU ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo

=====

Tuhuma nzito Wabunge CCM wapewa Bil 2.7 kuweka mambo sawa​


Mtanzania Digital | November 4, 2016 | Na Bakari Kimwanga, DODOMA

TUHUMA nzito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kudai wabunge wote CCM) wamehongwa kila mmoja Sh milioni 10.

Amesema mgawo wa fedha hizo, uliratibiwa vyema na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kushirikiana na Katibu Msaidizi wa wabunge wa CCM, Abdallah Ulega.

Alisema lengo na kutoa fedha hizo ni kutaka kuwalainisha wabunge hao ili wapitishe Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni leo.

Hoja hiyo aliibuka jana bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.
Mbowe alikuwa mbunge wa kwanza kupewa nafasi ya kumwuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa lakini Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alikataa lisijibiwe kwa madai si swali la kisera.

Baada ya kuzuiwa swali hilo, uliibuka mvutano mkali kati ya Mbowe na Dk. Tulia kumpa nafasi mbunge mwingine ili aendelee kuuliza swali jingine.

“Mheshimiwa Naibu Spika, wabunge na mawaziri ni viongozi wa umma kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995.

Kuna taarifa ya kwamba siku ya Jumanne Oktoba 25, mwaka huu saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM na wewe ukiwa mwenyekiti (Waziri Mkuu Majaliwa), katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

“Pamoja na mambo mengine Muswada ambao unatarajiwa kuletwa bungeni kesho (leo) wa mambo ya habari na Mpango wa Taifa ambao tunaendelea kuujadili ulijadiliwa pamoja na mambo mengine yote kikao kile kiliamua kutoa zawadi kwa wabunge wa CCM,wakiwamo mawaziri kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa kila mbunge wa CCM wakiwamo mawaziri.

“…zimetolewa kwa viongozi ambao wanabanwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na vilevile mgao huu umeendelea kutolewa ofisi za CCM makao makao, ukiratibiwa na Naibu Katibu wa wabunge wa CCM ambaye pia ni mbunge, Waziri Mkuu taarifa hizi ni za kweli?,” alihoji Mbowe.

Hata hivyo, swali hilo liligonga mwamba, baada ya Dk.Tulia kumzuia Waziri Mkuu kujibu akisema swali hilo lilikuwa kinyume na maudhui ya kipindi hicho.

“Maswali kwa Waziri Mkuu ni maswali yanayohusu sera, waheshimiwa wabunge tukumbushane tu vizuri mheshimiwa Mbowe naomba swali lako liwe linahusu sera.

“Mheshimiwa Mbowe, mimi nitamruhusu kujibu maswali yanayohusu sera kama ambavyo nitamzuia mtu mwingine yoyote kwa hiyo, wewe ndiyo maana nimekupa nafasi tena ili uulize swali linalohusu sera ndivyo kanuni zetu zinavyosema,” alisema.

Licha ya hali hiyo, Mbowe aliendelea kushikilia msimamo wake na kutaka swali hilo lijibiwe kwa kuwa linahusu sera.

“Sijasema tuhuma hizi ni za kweli ila nimeuliza Waziri Mkuu atujibu ni za kweli au si za kweli Naibu Spika unalinda nini?,” alihoji.

Mnyukano kati ya Mbowe na Dk. Tulia, ulimfanya kiongozi huyo wa Bunge kulizuia swali hilo.

“Mheshimiwa Mbowe nadhani hapa tulipofika kama wewe unaona hili swali ni la sera, kanuni hizi ndiyo zinaniongoza mimi kwa maana hiyo nitaendelea na maswali mengine. Mheshimiwa Munde Tambwe Abdallah atauliza swali kwa Waziri Mkuu,” alisema Dk. Tulia.

Hata hivyo, swali hilo lilibuka na kuombewa mwongozo na Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), ambaye alitaka kujua hatua ya swali hilo kuzuiwa na kama Bunge litakuwa linaona haliwezi iridhiwe ili iundwe Tume ya Kimahakama ili kuchunguza swala hilo.

Mbali na Silinde, pia Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), alimtaka Mbowe athibitishe madai hayo kwani ni masuala yanayohusu vyama na si Bunge huku akisistiza hakuna fedha iliyogawiwa na chama.

Mbowe na wanahabari

Baada ya kipindi cha maswali na majibu Mbowe, alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Rais Dk. John Magufuli, amtumbue Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa kama anavyowatumbua watendaji wengine.

Alisema taarifa walizonazo katika kikao cha wabunge wa CCM Oktoba 25, mwaka huu, baada ya Serikali kuona hasira za wabunge wao dhidi ya kudorora kwa uchumi, Kinana na Majaliwa walikubaliana kuwapa fedha wabunge.

Alisema tuhuma hizo ni nzito na Bunge haliwezi kujichunguza lenyewe hivyo ni lazima iundwe tume huru ya kimahakama kuchunguza jambo hilo.

“Kwa nchi zilizoendelea jambo hili lingefanya Serikali ijiuzulu leo rushwa ya Shilingi bilioni 2.7 inatolewa kwa malekezo ya kiongozi mkuu wa nchi?…hii ni hatari na inaonyesha tusivyo na utawala bora,” alisema .
 
Poleni kwa hasira. Mimi nawashangaa nyie kushangaa hili leo. Tanzania sheria zetu hulala na kuamshwa kutegemea ni nani mlengwa. Kama uko kenye chama tawala zitaamshwa ukihamia upinzani au hata ukiushabikia. Hilo limeonekana sana awamu hii tena bila aibu. Kuna watu waliadhibiwa kwa sababu tu maeneo yao ya simamizi walishinda wapinzani.
 
Hivi zile tuhuma za Mbowe kupokea Bilioni 10 kutoka kwa Lowasa ili aruhusiwe kugombea Urais uchunguzi ulishafanyika?
 
Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.
Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa ccm kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.
Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.
Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.
Kufuta aibu hii ya kitaifa Takukuru watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.
Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe? Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?
Takukuru ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo

Takukuru huwa wanafuatilia tuhuma zenye ushahidi.Mbowe alitakiwa apeleke hizo tuhuma na ushahidi wote TAKUKURU sio kubwabwaja tu bungeni maneno matupu yasiyo na ushahidi wowote kama maneno ya mlevi kwenye kilabu cha mbege.
 
Serikali ya Magufuli haina mambo ya kuhongana. Akina Bashe wangepiga kelele mchana kweupe
Kweli eeh...kwaio kilichomfanya spika amzuie mbowe kuongea ni nini...
Subirin mtayatapika na mengine yatawatokea puani siku za karibuni
 
Hivi kwani sheria zinasemaje hapa, au wanaweza tu kuchunguza pale wakiambiwa na Waziri Mkuu!
 
Hiyo ndio Tanzania bwana.Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba utuondolee hili joka kubwa na lenye sumu kali inayoangamiza nchi.Ni aina ya Koboko mwenye rangi mbili za KIJANI na NJANO na weusi kwa mbali.Tunakuomba utunusuru wanyonge wanaangamia.
 
Achana propaganda na siasa za kibunge hizo
Wewe kweli kwa akili ya kawaida tu
Kweli unaweza amini kuwa serikali
Inaweza kuhonga mil 10 kila mbunge
Kwa kupitisha muswada wa habari?
Sasa nini kitafanya hili lisiwezekane?na wewe unatuletea kioja mbona?
 
Back
Top Bottom