Tajiri wa Pi Network anaomba nimrudishe kazini

Ponjoro wa Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
3,536
Reaction score
9,611
Huyu kijana aliyekuwa anafanya kazi hapa kama operator wa forklift, aliacha ghafla kuja kazini wiki chache zilizopita. Nikafanya jitihada kumtafuta akawa hapokei simu.

Baada ya siku kadhaa akanipigia akaniambia anakaribia kuuza coin zake hivyo hafanyi kazi za kimaskini nitafute mtu mwingine.

Ukweli ni kuwa nilimpa muda wa kutafakari, baada ya ukimya kutawala ikabidi tutafute kijana mwingine.

Sasa leo kaja nyumbani na mjomba wake anaomba sana arudi kazini hata kwa kazi za kusaidia mafundi maana yakwake imeshachukuliwa.

Sasa naogopa kumwajiri tena huyu tajiri wa Pi - Network maana aliniambia yeye ni bilionea.

Niliwahi kuona uzi wa Pi hapa JF sijui matajiri wa hapa JF walifanikiwa au vipi? Nataka niwaunganishe na tajiri mwenzenu mpeane mbinu za kivita.
 
Coins zilikuwa na airdrops kamq njugu halafu eti ziwalipe ni utani🤣🤣🤣Hawa walioanza kufuatilia cryptocurrency hivi karibuni wana tabu sana..

Muache apauke kwanza akili ikae sawa
 
Huyu kijana aliyekuwa anafanya kazi hapa kama operator wa forklift, aliacha ghafla kuja kazini wiki chache zilizopita. Nikafanya jitihada kumtafuta akawa hapokei simu.

Baada ya siku kadhaa akanipigia akaniambia anakaribia kuuza coin zake hivyo hafanyi kazi za kimaskini nitafute mtu mwingine.

Ukweli ni kuwa nilimpa muda wa kutafakari, baada ya ukimya kutawala ikabidi tutafute kijana mwingine.

Sasa leo kaja nyumbani na mjomba wake anaomba sana arudi kazini hata kwa kazi za kusaidia mafundi maana yakwake imeshachukuliwa.

Sasa naogopa kumwajiri tena huyu tajiri wa Pi - Network maana aliniambia yeye ni bilionea.

Niliwahi kuona uzi wa Pi hapa JF sijui matajiri wa hapa JF walifanikiwa au vipi? Nataka niwaunganishe na tajiri mwenzenu mpeane mbinu za kivita.
Hahaha Kuna mwamba tukonae,daily wimbo wa pai namna atakavyokuwa "young bilioner " tunasubiria Pi iteme na ana mpango wa kuacha kazi baada ya Pi kutema
 
Sasa leo kaja nyumbani na mjomba wake anaomba sana arudi kazini hata kwa kazi za kusaidia mafundi maana yakwake imeshachukuliwa.
Hadi kaja na mjomba wake mtakuwa mnafamiana/ndugu. Mpe hiyo nafasi anayoitaka atakuwa amejifunza.
 
Back
Top Bottom