Tajiri la Kimarekani na Papa

Mtanzanika

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
2,389
1,131
Tajiri mmoja wa Kimarekani alienda likizo kutalii mjini Rome, na alitamani sana kumwona Papa.Alisimama katika mlolongo mrefu wa watu akiwa na suti yake moja ya bei mbaya mno akiamini kuwa Papa angelimwona kwa umaridadi wake wa mavazi na labda angechati nae kidogo.

Papa alipomkaribia, alimpitia karibu kabisa lakini wala hakumtupia jicho kana kwamba Tajiri huyo hakuwa kitu chochote bali ni Mlingoti tu..

Papa akasimama kwa kijana mmoja masikini choka mbaya kwa mavazi yake, kasha akamnong’oneza kitu halafu akaendelea na safari.

Kitendo kile kilmuuma sana Tajri yule. Baadae alimfuata Yule kijana masikini na akazinunua nguo zake kwa dola 1500 akiamini Papa angelimwona na kuzungumza naye kesho yake.

Kesho yake Tajiri Yule aliposimam katika mlolongo kama kawaida akiamini safari hii ni uhakika kuchat japo kidogo na Papa. Papa alipofika kwa Tajiri aliinama kwa upole kabisa na akamnong’oneza sikioni...

"I thought I told you yesterday to get the f**k out of here."
 
Back
Top Bottom