kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,613
Haya niambie!!! Taifa stars kwa ku fluke ikawa hiyooo hadi Qatar. Hebu tuseme ukweli ingekuwaje?
Taifa lengepata aibu inayoweza kuuangusha chini hata mlima wa Kilimanjaro. Timu hii ya akina Samatta na Kibu ingemwaibisha Waziri mkuu na kila mtu nchini.
Kilichoipata Zaire 1974 ambacho dunia inakumbuka hadi kesho ingekuwa cha mtoto.
MwenyeziMungu katunusuri na balaa zito.
Tunaomba serikali yetu sikivu ianze Sasa kutengeneza kikosi Cha kwenda USA na Mexico kuanzia Leo. Serikali iwekeze kwenye timu ya taifa kuanzia Sasa kwa kumwanga pesa kwenye soka la watoto na vijana.
TFF hakikisheni kuwa wachezaji wetu wote wanakuwa na maumbo makubwa wenye vipaji. Mikoa yenye wachezaji wenye maumbo makubwa inafahamika, nendeni huko mkachague watoto wenye vipaji na kuwaweka pamoja kuanzia utotoni.
Tusingojee kuwajaza pressure wachezaji kwa maneno na ahadi ya fedha siku ya mechi.