Taifa linalishwa uongo, sio Trump wala Magufuli

Taifa linalishwa uongo, sio Trump wala Magufuli

CCM watakubali kunguza wajumbe? Wajumbe watakula wapi?
 
UFIPANI HAWALALI WAKISIKIA MAGUFULI AKISIFIWWAAA.
ETI WANAPINGA TRUMP HAJAMSIFIA MAGUFULI. SIJUI AKILI ZENU ZIKOJE
 
naombeni kuona hizo taarifa maana hili jitu linaloongoza nchi flani ya samawati silipendi [emoji111][emoji111]
 
Sasa wewe mpuuzi YERIKO unaeshindwa kuhoji ALIPO SAANANE unajifanya kuja huku kutetea lichacjma lisilo jali na kuthamini michango ya watu wanao kipigania CHAMA....HIVI kipi kinachokuuma IWAPO TRUMP akimsifia MAGUFULI?????.....tatzo lenu hapa mnataka kusikia MABAYA tuu juu ya MAGUFULI......Let me remind you this.....KWA SASA HAKUNA RAIS BORA AFRIKA aliye kwenye midomo ya WAAFRIKA kama MAGUFULI na hili nyie hmataki kabsa kulisikia...
Na hakuna CHAMA KICHAFU kwa propaganda chafu za mitandaoni kama CHAMA CHENU.....
Refer uchaguzi wa 2015 mlivyokuwa walaghai kwa mipicha picha ya mafuriko YA VYUMBANI KWENU
Achana na hizo story za February mwaka Jana wakati ndiyo kwanza ana miezi minne (4) tangu kuchaguliwa.
 
Kuna upuuzi unaendelea mitandaoni na wabana pua kwamba oooho Trump ampongeza rais wetu kipenzi. Ikulu ya Marekani ndio inaandika kiingereza kibovu vile na inatumia wasapu siku hizi badala ya njia sahihi toka White House Kiingereza kile kina sura na mfanano kabisa wa mwandiko wa ndugu yangu Humphrey Polepole, labda siku hizi amekuwa mwandishi na msemaji wa Donald Trump wa Chamwino pale Dodoma...Lakini Trump yule wa Marekani sijui kama anajua kuwa kuna Tanzania ya Magufuli, ninachofahamu anajua kuna Afrika ya Nyerere, Nkurumah, Mandela, Lumumba, Mugabe, Museven nk.....

Hotuba ya Donald Trump wakati akisaini sheria ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini mwake hakuna mahali alipotamka neno Magufuli, wala hakuna alipomsifu... Nilifuatilia hotuba ile, lakini mtandao wa radio ya Ufaransa ya kiswahili umechomekea maneno hayo nakufanya habari kuwa tofauti kamia propagsnda za aona hii bisa, Ukweli Rais wetu tutamsifu wenywe kwa mazuri yake sio kwakutumia propaganda za aina hii, Bahati mbaya vyombo vya habari vya kimataifa vinavyotumia lugha ya kiswahili vingi vimejaa watanzania wenye ushabiki wa vyama (makada) ambao muda mwingi wanatumika vibaya.

Rais asifiwe kwa mazuri yake mfano mimi namuunga mkono kwa 100% Zanzibar ibebe msalaba wake, Muda wa kubebwa Zanzibar umekwisha ilipe deni la tanesco ili shirika letu liweze kujiendesha... Tumewabeba kwenye bajeti ya Masuala ya Muungano ambapo Bajeti huwa kati ya trilion 2-2.5 lakini Zanzibar huchangia sifuri katika Mfuko huo wa Muungano uitwao JVC committee. Wakati huo bajeti ya Zanzibar ni kati ya 500b hadi 550b lakini pato la Zanzibar ni 150b, hivyo kiasi cha zaidi ya 350b huwa tunawachangia sisi tani kodi zetu zinakwenda kuwahudumia wao kule... Baada ya hapo katika baje ya Muungano hutengwa 34b kwaajili ya Rais wa Zanzibar, hii huitwa pesa maalumu ikitumika kwa shughuli maalumu za kiusalama na mengineyo... Hii inatoka pia kwa walipa kodi wa Tanganyika, Je Zanzibar inachangia nini kwa Tanganyika? Jibu ni sifuri..... Zaidi ni ulinzi wa Bahari na UDUGU.
Hili ndilo linanifanya nimuunge mkono rais wangu kipenzi...

Tukirejea kwenye siasa zetu chafu, Mahangaiko ya vijana wa Lumumba ni makubwa na yanasikitisha sana, Chama kimepasuka mapande matatu hapo Dodoma ambayo hayana refa kabisa,

Ipo ccm ya JPM hawa wanaangalia ugali unapotoka tu (wafanya biashara), Ipo ccm ya JK hawa wanalia kuumizwa baada ya JMP kufunga mirija yao, na Ipo ccm ya The Don hii ndio inayoendesha nchi...

Nyie parulaneni huko Dom, badilisheni katiba kwamba mnajenga ccm imara kumbe mnaivunja cm, lakini sisi ni timing tu, furaha yetu ni kuona uchaguzi ujao katiba inazuia mwanaccm kumpinga rais aliyepo madarakani.

Taarifa zote zinazomhusu Rais Trump hata akipiga chafya tu hutolewa kupitia hapa Statements and Releases. Nje ya hapa hizo ni kahawa za vibarazani TBCccm.

Twendeni....twendeniii tukamkabe Bashite....
Kama wewe ulivyolilisha taifa uongo kuwa Lowasa ni fisadi.

Shame on you
 
hivi kwa nini rais wa nchi ya kiafrika akisifiwa na rais wa marekani inakuwa ni big deal? mbona huko US kwenyewe kila uchao wanaandamana kumpinga huyo Trump?
huu ukoloni mamboleo wa kutawaliwa kifikra utatuishia lini? eti kiongozi bora ni yule anayesifiwa na rais wa US? tumefilisika akili zetu kiasi hicho kweli?
aibu.aibu.aibu.
tujitambue.
 
ufipa ni hatari kama viroba..chuki imetamalaki usoni hadi nyoyoni..
 
Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuwa mfano mzuri wa viongozi wa Afrika.

Wakati akisaini sheria ambayo itakuwa ikizuia waafrika kutoka nchi ambazo marais wake hawafanyi lolote na wale ambao wamegoma kuondoka madarakani, Trump amesema rais Magufuli ni mfano wa viongozi bora wa Afrika na nchi yake inastahili kutendewa kipekee.

Trump ameongeza kuwa sheria hiyo itaziathiri nchi kama Zimbabwe, Uganda na nyingine za Afrika ambazo marais wake wamekataa kuondoka madarakani wakiwa hawafanyi lolote na kusema kuwa Tanzania si miongoni mwazo kwa kuwa wajina wake rais John Pome Magufuli anafanya kazi nzuri.

Kwa mujibu wa Rais Trump , Watanzania hawatazuiwa kwenda Marekani na watapewa upendeleo maalum kwa hisani ya rais Magufuli.

Trump amehitimisha kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake akisema "Hongera wajina wangu John Magufuli, wewe ni shujaa wa Afrika".

Rais wa Marekani ampongeza rais Magufuli wa Tanzania
 
Back
Top Bottom