Taifa liadhimishe Komba day

Taifa liadhimishe Komba day

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,845
Reaction score
4,775
Salam wakuu,

Baada ya Msiba mzito wa Capt J Komba, niliamua kusikiliza kazi mbalimbali alizozifanya. Nimegundua jamaa alikuwa na uwezo mkubwa sana, Yaani alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo na kurekodi ndani ya nusu saa. Pia tofauti na nyimbo za akina Diamond, Nyimbo za capt Komba hazichuji kabisa. Halafu zina ushawishi sana.

Kwa kweli kuna kila sababu ya kumuenzi. Tuteue siku 1 ya mapumziko tuwe tunasikiliza track zake. Japo mimi sio CCM, ila kuna wimbo unaitwa Arambee ulikuwa unanishawishi sana, hasa kwenye yale maneno "Wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupee" dah... huyu jamaa alikuwa hatare sana.

Komba day ni muhimu aisee.
 
Hizi ni akili za watu wavivu,, badala ya kuja na mada ya kukwamua tanzania kwenye umaskini unazungumzia kuendelea kulala lala tu. Mtu akishakufa amekufa tu.

Pia aliwakosea sana Watanzania na magamba wengine kwa kutukosesha kuwa na Katiba nzuri, sioni kama yeye na hao wengine wanahadhi ya heshima kwa walichokifanya.

Ukichanganya na uhuni wanaondelea kuwafanyia Watanzania wajue watu wana hasira nao sana.
 
Ikumbukwe kwamba kifo cha maccm ni faraja sana kwa watanzania.komba day watafanya huko huko waliko tangulia...
 
Nakuunga mkono mdau,captein alikuwa ni hazina ya utunzi ndani ya taifa letu.Si vibaya kuwa na Komba day ili kumuenzi kipenzi chetu huyu!!.
 
Salasm wakuu... baada ya msiba nzito wa Capt J Komba... niliamua kusikiliza kazi mbalimbali alizo zifanya. Nimegundua jamaa alikuwa na uwezo mkubwa sana..... Yani alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo na kurekodi ndani ya nusu saa.. Pia tofauti na nyimbo za akina Diamond, Nyimbo za capt Komba hazichuji kbs. Halafu zina ushawishi sana. Kwakweli kuna kila sababu ya kumuenzi.... tuteue cku 1 ya mapumziko tuwe tunackiliza track zake. Japo mimi sio ccm ila kuna wimbo unaitwa Arambee ulikuwa unanishawishi sana..... hasa kwenye yale maneno "wapinzani tuwalete tuwachanechane tuwatupee" dah... huyu jamaa alikuwa hatare sana. Komba day ni muhimu aisee.

Nakuunga mkono mdau,captein alikuwa ni hazina ya utunzi ndani ya taifa letu.Si vibaya kuwa na Komba day ili kumuenzi kipenzi chetu huyu!!.

Pathetic....!!!
 
Nakuunga mkono mdau,captein alikuwa ni hazina ya utunzi ndani ya taifa letu.Si vibaya kuwa na Komba day ili kumuenzi kipenzi chetu huyu!!.

Alikuwa akiimbia taifa au Chama? Nyimbo zake zilisaidia nini ktk level ya Taifa? Je, South Africa watasemaje kuhusu kina Lucky Dube na michango yao ktk kuhamasisha uhuru wa taifa lake? Michael Jackson wa USA asihadhimishwe hata nusu siku iwe Komba?
 
huyu alikuwa mchafuzi Wa taifa hili alitangaza kuingia msituni...Mungu kaliokoa taifa

Ila kiukweli tutazimis tungo zake.
Fikiria leo tupate msiba mkubwa wa kitaifa(Mungu na apishilie mbali),nani atahanikiza kwa nyimbo zenye hisia kali za majonzi kama ilivyokuwa enzi za Capteiiiin!!.
 
Labda za n

Labda zile za maombolezo ya nyerere lkn hizi nyingine labda unazielewa wewe tu.
 
Labda za n

Labda zile za maombolezo ya nyerere lkn hizi nyingine labda unazielewa wewe tu.

Vipi kuhusu ile free style aliyoimba pale bungeni "Tunaimaniii na katiiiba" haija kugusa hata kama huungi mkono katiba?
 
Nikweli alikua na kipaji lakini kuwa na siku ya komba day labda ccm wanapaswa kufanya hivyo kwakua kunapengo limebaki kwao
 
Mwaka 2005 pale Dodoma kwenye mkutano mkuu wa ccm,captein nusura amtoe machozi JK.
Ni pale JK alipotangazwa mshindi mbele ya Dk Salim na Prof mwandosya katika uchaguzi wa ndani wa chama,ndio hapo Captain akaporomosha lile songi maaaarufu kabisa la...."Jakaya Kikwete amechukua ameweka waaa...ccm jama shangilia ushindi unakuja...".
Pale jukwa kuu nilikua namuona JK macho yanamchonyota kwa jinsi captain alivyokuwa anaimba kwa hisia kali!!.
 
Tungo za Komba noma sanaaaaa😀😕😛
 
Tungo za Komba noma sanaaaaa😀😕😛

Sana tu mkuu,ni vile watu hawataki kujipa muda wa kusikiliza tungo za captaiiiiin!!
Wao wanang'ang'ania oooh katuharibia katiba mara ooh anatembea na Lulu....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom