Kafia Gheto ya Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi

Feb 6, 2024
40
51
HUSENI MACHOZI

Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi . Alizaliwa mwaka 1986 katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

HUSENI MACHOZI ni moja Kati ya wasanii ama list ya wasanii ambao walipita kwenye mikono ya radio presenter/ producer "kid BWAY"
Hii ni
List ya baadhi ya wasanii ambao wamepita kwa producer kid BWAY .

Sajna
Baraka da prince
Star madini

Nk...

KWA maelezo ya producer kid BWAY anadai kwenye list ya wasanii ambao wamepita kwenye mikono yake kwa upande wa msaniii husen machozi kid bway ameplay party kubwa sana kumsaidia HUSENI MACHOZI katika safari yake ya Muziki.

Hapo nyuma husen machozi alikuwa anaishi Mkoani kagera na for the first time producer kid BWAY kuonana na msaniii husen machozi , ni pale msaniii HUSENI MACHOZI alipokuja kurekodi wimbo wake wa kwanza unaitwa" promise"

Producer kid bway alimueleza huseni kuwa anaona kibaji chake kuwa ni kikubwa sana lakini maneno yake yalitimia pale alipoenda kutoa wimbo wake wa pili unaitwa " kafia ghetto"

Enzi hizo promise ikiwa kama single song kabla ya wimbo huu kubeba jina la Album..

Msaniii huseni machozi aliteka sana Hisia za producer kid BWAY na kupelekea producer kid bway kumpa nafasi nyingine huseni machozi kwenda kurekodi nyimbo for free ( Bure)

nyimbo yake ya pili iliyojulikana kwa jina la "kafia ghetto "..

Kutokana na chemistry ya huseni machozi na producer kid BWAY kushika atamu ilimlazimu producer kid bway kumueleza huseni machozi inampindi atoke Mkoani kagera na arudi jijini Mwanza ili kusiwepo na ugumu tena likija suala nzima la uandaji wa kazi nyingine kutokana na ubali wa kutoka Mkoani kagera hadi jijini Mwanza na msanii huseni aliishia KWA producer kid BWAY kwa muda wa mwaka 1 na Nusu.


Kama uliwahi kuusikia wimbo unaoitwa Kafia Ghetto unaozungumzia story ya jamaa mmoja ambaye alimfukuzia au kumtaka urafiki wa mapenzi binti mmoja kwa muda mrefu sana. Baada ya muda huo mrefu, siku moja binti huyo akaamua kwenda “ghetto” kwa ajili ya huyo jamaa ili kumpa taarifa kwamba amekubali ombi lake. Kijana akafurahi sana na kisha kumuacha binti ghetto na kuelekea dukani kumnunulia soda. Aliporejea alitahamaki kukuta binti amejilaza kitandani kwake. Alipojaribu kumgusa akagundua kwamba binti amekata roho. Jamaa akachanganyikiwa asijue la kufanya. Kwa ufupi hiyo ndiyo story iliyomo ndani ya wimbo Kafia Ghetto. Mwisho wa wimbo Hussein anauliza ungekuwa ni wewe hali hiyo imekutokea ungefanya nini? Je walimwengu watakuelewa kwamba hukumuua binti? Je ungemtoa vipi humo ndani mwako?.

Wimbo huu ulizindi kuziirisha uwezo wa msaniii husen machozi kwa producer kid BWAY na wadau wengine wa Muziki kutokana na ubora wa huseni machozi .

Na kubwa zaidi before huseni machozi kujiita huseni machozi
alikuwa anatumia jina lake halisi "huseni" lakini radio presenter "frederick Bundala a.k.a sky walker alipomsikiliza kazi za jamaa ( husen machozi) akadai kutokana na msaniii huseni machozi kuimba nyimbo zenye Hisia kali kuhusu mapenzi ndio radio presenter sky walker akadai si vyema jina lake liishie tu "huseni" maana kuna kina huseni wengi" Tanzania
ndipo hapo akapindi kuongezea neno " machozi"

Tangu hapo huseni akabadili jina akawa anaitwa " huseni machozi" mpaka leo ..

Naimani kuna kitu umejifunza hapa

#funguka

Hussein Machozi hakuishia hapo. Aliendelea kudhihirisha ukali wake kwa kutoa wimbo mwingine uliokwenda kwa jina Full Shangwe akimshirikisha AY. Nyimbo hizo pamoja na zingine kama vile Maji Yakimwagika, Niambie zinapatikana katika albamu yake ya kwanza inayoitwa PROMISE aliyoitoa mwaka 2008.

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
images.jpeg
images (1).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom