Taifa letu la kesho linaandaliwa hapa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
WANAFUNZI12.jpg


mwalimu wao, hayupo katika picha, huku Jengo la darasa lao likiwa katika hali mbaya inayohatarisha maisha yao kama linavyoonekana katika picha hii. Darasa hilo hutumiwa na wanafunzi 45. (Picha na Mashaka Mhando).
 
Waungwana nilishindwa kuiweka hiyo picha ya kusikitisha hapa, lakini ukiclick kwenye hiyo link utaliona darasa ambalo halistahili kupewa hata hadhi ya kuwa choo wachilia mbali darasa.
 
Watoto wao wanasoma katika shule zilizo bora kabisa, kuanzia mazingira mpaka Waalimu. Hawana haja kuboresha shule za Wananchi manake hawana uchungu wowote, na wanajua watatawala kwa muda watakao.
 
Mwanafunzi akifanikiwa kufaulu toka kwenye darasa hilo ni genius!

Hii inatuumiza sisi ambao tumepata bahati ya kuishi sehemu ambapo mambo hayoko hivyo. Bahati mbaya hawa watoto, maisha ya nyumbani kwao hayana tofauti na darasa lao! sio ajabu wazazi wao wanasifia kuwa darasa pia limeezekwa kwa bati. Kitu wengi wasicholielewa ambacho ndicho serikali isichotaka wengi waelewe ni "NINI NI HAKI YA RAIA WA TANZANIA". Likiweza kufahamika hilo, na haya yatakwisha, vinginevyo kura wataendelea kupata kwa kishindo kwani siku hizi wanakimbia maeneo kama haya kwa kuwa hawaulizwi maswali mengi na magumu!

Inasikitisha kiasi cha kutosha.
 
Mwanafunzi akifanikiwa kufaulu toka kwenye darasa hilo ni genius!

Kumbe mimi ni genius maana nimesoma shule dizaini hizo, na waalimu walikuwa hawatoshi, nikiwa darasa la saba nilikuwa nafundisha wenzangu madarasa ya chini 6 na 5! Leo napeta na watoto wa mafisadi walisomea st.....Academy!
 
Darasa ndilo hilo, hospitali dripu zinatundikwa kwenye miti, wananchi utapiamlo kwa sana, maralia usiseme, maji ya matope yanachotwa kilomita tano, vyuo vya elimu ya juu mikopo haitolewi, halafu tunaandamana eti sera zimetekelezwa!!!!!!! jamani tukoje sie.

Wakati shule,hospitali, huduma za Afya na maji ziko hivyo ona contradictions: snacks bilioni 9 kwa mwaka, shangingi kila mkuu wa wilaya na all other extravagancies, where do we think we are heading.
 
Hapa silaumu mafisadi.

Yaani wameshindwa kwenda kukata fito na miti kadhaa na kuja kujenga hizo kuta?

Sehemu za madirisha zingeachwa wazi ila vijana wawe ndani. Yaani hata udongo na fito nayo ni kazi? Hicho kijiji ni cha kuchapa viboko. Hiki ni kilema cha kutegemea serikali ije itufanyie kila kitu. Kijiji kizima kingelifanya hiyo kazi siku moja tu.

Inabidi kupata jina la Mbunge wa eneo hilo, mkuu wa wilya, mkoa, katibu kata, katibu tarafa, mwenyekiti wa kijiji....... Huu ni ukiwete mbaya kabisa duniani --KILEMA CHA MAWAZO.

Ningelaani kama kusingelikuwa na madawati na mabati juu. Hii shule ni BOMBA sana sana ukilinganisha na wengine tulizosomea. Masanilo, kama umetembea Sikonge nafikiri ulijionea mwenyewe shule za huku kwetu kama Iyombakuzova, Mibono, Pangale, Ipole, Tumbili, Utawambogo nk.

Hebu tuache kulaani kila kitu MAFISADI. Wananchi inabidi tubebe lawama ya asilimia 40 ya hali hii kwa ujumla. Yaani hakuna MWALIMU Juma wa kutibu magonjwa ya namna hii? Ningelimpeleka huko akatibu UTINDIA UBONGO wa Kijiji kizima. Mengine nakubali lawama ila hili mwenzenu SINUNUI.
 
WANAFUNZI12.jpg


Haya na endeleeni kubisha kuwa Miafrika Sivyo Tulivyo! Watu wenye akili na ubunifu wangetumia akili na ubunifu wao kuboresha hayo mazingira ya kujifunzia. But guess what...wanasubiri lidude liitwalo serikali kuja na kuwaboreshea mazingira yao. Wanachosahau ni kwamba hata hilo lidude liitwalo serikali limejaa mijitu mijinga isiyo na akili kama wao. I guess unapokuwa mjinga hata kumtambua mjinga mwenzako inakuwa kaaazi kweli kweli.
 
Lakini ieleweke kuwa Taifa letu bado ni changa ,Rais wetu anafanya jitihada za hali ya juu kuondowa matatizo yanayotukabili ,tuwe wenye ustahamilivu kwa kipindi hiki kigumu ,tumpeni muda angalau inatia moyo hao wanafunzi wapo juu ya mabenchi na kupatiwa elimu.
 
Lakini ieleweke kuwa Taifa letu bado ni changa ,Rais wetu anafanya jitihada za hali ya juu kuondowa matatizo yanayotukabili ,tuwe wenye ustahamilivu tumpeni muda angalau inatia moyo hao wanafunzi wapo juu ya mabenchina kupatiwa elimu.

Hali hii inavunja moyo zaidi ya kutia moyo. Eti inatia moyo wako juu ya mabenchi kupatiwa elimu. Babylon please.....

Hii hali haina excuse. Na ukiingiza kwenye equation hiyo misaada tunayopata kutoka kwa wahisani tokea enzi na enzi ndio unanyong'onyea kabisa.

Sitashangaa kama wakiwepo wale watakaosingizia hali hii na ukoloni kana kwamba kabla ya ukoloni mambo yalikuwa mswano zaidi.

Miafrika Miafrika Miafrika....
 
Inatisha! lakini sio kwa sababu serikali haijafanya kitu, bali wananchi hawajafanya kitu. Hata Mwalimu mkuu angeweza kubadili mazingira yale kwa kutumia nguvu kazi, udongo na maji kuweka kuta vizuri. Mbona madesk ni mazuri tu, imeshindakana nini. Na hapa nadhani ndio tunahitaji kisomo kwa wananchi wetu, wajikusanye wasisubiri serikali. Serikali ni wao wenyewe. Kama serikali Kuu itahusishwa basi ni kwa yale yahusiyo walimu na mishahara yao. Naunga mkono suluhisho sio ufisadi, ni sisi wenyewe kujikakamua na kufanya kazi. Pengine wenzetu wa Kilimanjaro walilitambua hili mapema zaidi na ndio maana wana shule nyingi tena bora, na kwa kawaida majengo ya shule yakiwa mazuri na mazingira yatapendeza; uwezo wa kumshawishi mwalimu abaki kufundisha unakuwa mkubwa. Shule kama hizi za mbavu ya mbwa hukimbiwa na walimu bora. NI AIBU KUKUBALIA WATOTO WETU WATESEKA HIVI KUPATA ELIMU
 
pamoja na hali hii Meneja wa TRA analipwa 18,000,000Tsh kwa mwezi akale yeye na awapandao, pia Meneja wa TBC, Meneja wa Tanroads, Wabunge, Waziri wa elimu nk .

Yani mkuu, at times huwezi kuelewa kuwa wote hawa wanaishi nchi moja. Na cha kuudhi zaidi ni mmoja anakula pesa ya mwenzake. Kweli Mungu awalipe mara 100.
 
Lakini hata hivyo si unacheki matofali hapo!?? watu wako shughulini kwa hiyo kimsingi kwa upande wao naona wanataka ku upgrade kutoka miti na tope kuwa matofali tena naona ya kuchoma hayo.
Anyway lets see 2010 is so closer
 
Back
Top Bottom