Rais Samia: Nawasihi Viongozi wa Kanisa na Viongozi wengine wa Dini nchini kuendelea kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu, tusiyumbishwe!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,980
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Kanisa la Anglikana na Viongozi wengine wa Dini kuzidi kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu na kuilinda Amani Yetu na tusikubali Kuyumbishwa na mtu yoyote asiyelitakia mema Taifa letu

Rais Samia amesema hayo Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma

Jengo hilo la kisasa kabisa jijini Dodoma linaitwa NMB Safina House

Mlale unono 😀😀

---

1692128444508.png
Rais Samia leo Agosti 15, 2023 Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma amesema:

“Serikali inatambua na kuthamini mchago mkubwa unaotolewa na taasisi pamoja na mashirika ya kidini nchini, mbali na kutoa huduma za kiroho ambazo zinachangia sana kujenga taifa la watu wenye uadilifu na uchaji Mungu, taasisi hizi zinasaidia sana Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi hususani afya, elimu, maji na hata kilimo.”

“Nawasihi viongozi wa kanisa hili [Anglikana] na viongozi wote wa dini nchini kuendelea kuliweka taifa letu katika mikono salama ya Mwenyezi Mungu ili lidumu katika amani, umoja na mshikamano. Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mtu yeyote yule asiyelitakia taifa letu mema.”

Nataka kuhimiza kazi ya kulinda maadili na kukemea maovu. [Viongozi wa dini] Muwafundishe vijana, lakini mbali na vijana hata wakubwa wale ambao wanalitumia kanisa kufanya mambo ya hovyo, naomba kemeaneni.”

Source: Swahili Times
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Kanisa la Anglikana na Viongozi wengine wa Dini kuzidi kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu na kuilinda Amani Yetu na tusikubali Kuyumbishwa na mtu yoyote asiyelitakia mema Taifa letu

Rais Samia amesema hayo Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma

Jengo hilo la kisasa kabisa jijini Dodoma linaitwa NMB Safina House

Source: Swahili Times

Mlale unono 😀😀
Amani+Haki ✔️
 
Wakati misukule yake inatunga maneno ya uongo dhidi ya Dr. Slaa ili kumfunika kwa udhaifu wake, kumbe ameshajua utawala wake unayumba, sasa asimlaumu yeyote mwingine, isipokuwa yeye mwenyewe.

Dharau zake kwa watanganyika ndio chanzo cha yote, huwezi kutoa bure bandari zetu zote kwa waarabu halafu ugome kusikiliza malalamiko yetu.
 
Wananchi tunaiombea serikali yetu kila siku ila viongozi wetu wanatuona wajinga. Sasa Bora tuwashtaki kwa Mungu afanye yake. Tumewachoka viongozi wala rushwa! Nchi inadumaa kila uchao! Tumeochoka serikali,hatuitaki Tena! Tumechokaaaaa!
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Kanisa la Anglikana na Viongozi wengine wa Dini kuzidi kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu na kuilinda Amani Yetu na tusikubali Kuyumbishwa na mtu yoyote asiyelitakia mema Taifa letu

Rais Samia amesema hayo Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma

Jengo hilo la kisasa kabisa jijini Dodoma linaitwa NMB Safina House

Source: Swahili Times

Mlale unono 😀😀
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Kanisa la Anglikana na Viongozi wengine wa Dini kuzidi kuliweka Taifa letu katika Mikono salama ya Mungu na kuilinda Amani Yetu na tusikubali Kuyumbishwa na mtu yoyote asiyelitakia mema Taifa letu

Rais Samia amesema hayo Wakati akifungua Jengo la Kitega Uchumi la Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma

Jengo hilo la kisasa kabisa jijini Dodoma linaitwa NMB Safina House

Source: Swahili Times

Mlale unono 😀😀
Nimemskiliza vizuri. Ila maneno hayo hakuna aliyeshangilia hadi yeye kajistukia.

Samia ana hoja nyepesi kama Nyasi
 
Back
Top Bottom