Tai: Ndege mchafu mwenye kuuokoa ulimwengu

Tai: Ndege mchafu mwenye kuuokoa ulimwengu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,403
Kwa baadhi ya ya tamaduni tai akitua juu ya paa lako...
Watu watakusanyika na kuanza kutoa maelezo mbalimbali
Wengine Watazomea na kupiga kelele, "Jamani eeh! Nuksi imetua!"😂
Wengine hata wataita waganga wa kienyeji
Na Wengine watafunga na kuomba.

Yote haya ni Kwa nini?
Kwa sababu kuna wazee waliwahi kusema tai ni wajumbe wa kifo.

Lakini ngoja nikuambie ....

Ndege yule yule anayeogopeka..
Huyo huyo tunayemuita mchafu na mwenye nuksi
Ndiye sababu ya sisi sote hatujafa kutokana na magonjwa mbalimbali

Iko hivi
TAI WANAKULA VITU VILIVYOFA… (mizoga) NA NDICHO KINACHOTUFANYA TUWE HAI.

Wanakula mizoga.
Nyama iliyooza.
Wanyama wanaooza.
Vitu ambavyo hakuna mnyama mwingine anayegusa.

Lakini ingekuwaje kama tai asingefanya hivyo?

Kama tai watatoweka leo-
Magonjwa kama vile kimeta, kichaa cha mbwa, nk yangeongezeka.

Kwa mfano yule mbwa aliyegongwa na kufa aliye kando ya barabara?
Nzi watakula.
Funza wataongezeka.
Bakteria watazidi ..Matokeo yake
Kifo kitaingia kwenye mnyororo wa chakula.
Kitaingia hewani.
Kitatuingia.

Lakini tai hutusaidia kuondoa huo uchafu bila kulalamika.. Na wala hatumpongezi
Wanakula kifo ili sisi tuishi.

Somo?
Wakati mwingine, wito wako utakupeleka kwenye maeneo machafu.Yasiyoonekana. na wengi na utaifanya, ili dunia dunia isioze

Sio kila shujaa huvaa manukato.
Wengine wananuka uvundo… ili wengine wapate harufu nzuri.😁
Inaendelea
 
Mshana Jr katika ubora wake
 
2.TUMBO LA TAI HUWEZA KUUA
VIMELEA VYA KIPINDUPINDU.

Mfumo wao wa mmeng'enyo wa chakula una asidi nyingi, ambayo Inaweza kuyeyusha bakteria ambazo zinaweza kuua wanadamu papo hapo.

Wanageuza sumu kuwa amani.

Somo?
Sio kila kitu kinachoingia kwenye maisha yako kinakusudiwa kukuangamiza.

Baadhi ya watu wamekua matumbo ya kiroho—
Hayo hugeuza usaliti kuwa hekima.
Maumivu ya ndani kuwa tumaini jipya
Waliokata tamaa kimaisha kupata faraja na tulizo

Mapito yako sio ulemavu wako maana yanaweza kuwa nguvu yako ya uponyaji iliyofichwa.

✅ TAI NI WAAMINIFU.

Wanaishi ndoa moja milele
Hawana michepuko
Wana kiapo cha milele cha upendo usio na kusalitiana

Hata kama mmoja akifa -
Hawana "kusonga mbele" (Ku move on) kana kwamba hakuna kilichotokea.
Wanaomboleza.
Wanajitenga.
Wanaishi kwenye ukiwa
Wanaelewa maana ya upendo wa kweli

Somo?
Uaminifu sio somo la kufundishwa shuleni, bali ni kitu cha kibinafsi cha kipekee, cha nadra na kilichojaa uchaji wa kiroho usafi na utakatifu

Katika ulimwengu wa hali mbaya na usaliti -
Kuwa mtu ambaye anakupenda kwa dhati, anakujali na asiyeweza kukusaliti
Kuwa mtu anayekupenda toka rohoni na anayekuheshimu sana

Inaendelea
 
Kwa baadhi ya ya tamaduni tai akitua juu ya paa lako...
Watu watakusanyika na kuanza kutoa maelezo mbalimbali
Wengine Watazomea na kupiga kelele, "Jamani eeh! Nuksi imetua!"😂
Wengine hata wataita waganga wa kienyeji
Na Wengine watafunga na kuomba.

Yote haya ni Kwa nini?
Kwa sababu kuna wazee waliwahi kusema tai ni wajumbe wa kifo.

Lakini ngoja nikuambie ....

Ndege yule yule anayeogopeka..
Huyo huyo tunayemuita mchafu na mwenye nuksi
Ndiye sababu ya sisi sote hatujafa kutokana na magonjwa mbalimbali

Iko hivi
TAI WANAKULA VITU VILIVYOFA… (mizoga) NA NDICHO KINACHOTUFANYA TUWE HAI.

Wanakula mizoga.
Nyama iliyooza.
Wanyama wanaooza.
Vitu ambavyo hakuna mnyama mwingine anayegusa.

Lakini ingekuwaje kama tai asingefanya hivyo?

Kama tai watatoweka leo-
Magonjwa kama vile kimeta, kichaa cha mbwa, nk yangeongezeka.

Kwa mfano yule mbwa aliyegongwa na kufa aliye kando ya barabara?
Nzi watakula.
Funza wataongezeka.
Bakteria watazidi ..Matokeo yake
Kifo kitaingia kwenye mnyororo wa chakula.
Kitaingia hewani.
Kitatuingia.

Lakini tai hutusaidia kuondoa huo uchafu bila kulalamika.. Na wala hatumpongezi
Wanakula kifo ili sisi tuishi.

Somo?
Wakati mwingine, wito wako utakupeleka kwenye maeneo machafu.Yasiyoonekana. na wengi na utaifanya, ili dunia dunia isioze

Sio kila shujaa huvaa manukato.
Wengine wananuka uvundo… ili wengine wapate harufu nzuri.😁
Inaendelea

Tai hana umuhimu huo kwa maisha yetu. Hapa mjini mara ya mwisho umemwona Tai ni lini? Mkoa gani kuna tai wengi kusema wanafanya hayo uyasemayo? Si bora hata ungesema chogo mzingwi, ndege john au kunguru.

Tai umuhimu wake si mkubwa hivyo kama ambavyo umetaka waaminisha watu. Wapo tai wachache sana kuliko kunguru au aina nyingine ya vultures. Tai kwenye jamii nyingi si ndege wa mkosi. Ungesema bundi labda. So kuna mambo umeandika hukufikiria kwa kina au hukupewa utafiti jadidi. Na ukasahau humu tupo watu mbalimbali
 
3.TANZI HURUKA BILA KELELE
Ni kati ndege wenye mabawa makubwa zaidi angani.lakini ni mara chache hupiga mbawa zao. Wao hucheza na upepo tuu Wakati ndege wengine wanatokwa na jasho kila kukicha…😂 wao Tai huteleza angani kimyakimya

Somo?
Sio lazima kuhangaika kama kuku asiye na kichwa ili uonekane.. Ili utambulike
Unaweza kusoma upepo na ukatembea na mkondo. Hatima yako itakuja bila kuhangaika kwingi
Harakati nyingi sio maendeleo kila wakati...Jifunze kusubiri upepo wako.

✅ TAI HAWANA SAUTI.
Hawawezi kutoa sauti
Hawawezi kulia.
Wanachoweza kufanya ni kupanua tu mdomo na kuguna.

Katika ulimwengu ambapo kasuku na ng'ombe, mbuzi nk wanapiga sana kelele....Tai hustawi kwa ukimya.

Somo?
Sio lazima uwe na sauti kubwa ili utambulike
Acha matendo yako yazungumze.
Acha matokeo yako yapige kelele.
Acha mwangwi wako ujirudie muda mrefu baada ya kuondoka kwenye chumba... Acha usikike mbali

✅ TINGI HAWAUI, WANAHIFADHI

Hawawindi
Wanasubiri kilichokufa.
Kisha wanakisafisha.
Huu ni wajibu muhimu wa mwisho wa asili. KUHIFADHI

Wakati simba wakinguruma na tai wakiwinda—
TAI hutulia na kuweka mazingira sawa yaliyochafuliwa na wenye kelele

Somo?
Sio lazima kuwa mkali ili kupata ufanisi.
Baadhi yetu si wapiganaji.
Sisi ni wapambanaji
Sisi ni tunajitoa sana
Sisi ndio tunaoingia baada ya wengine kuharibu
Na jukumu hilo...Ni takatifu vile vile.
Inaendelea
 
4.Mwisho wa tamati

KATIKA UTAMADUNI WA KIHINDU NA WABUDHA, TAI NI WATAKATIFU.

Huko Tibet, tai ni sehemu ya "mazishi ya angani."

Mtu anapokufa, mwili hutolewa kwa tai
Tendo takatifu la kurudi kwa asili.

Wanaamini kwamba tai huinua roho mbinguni.

Lakini katika ardhi yetu wenyewe?
Tunawapiga mawe ndege ambayo wengine wanaheshimu.

Somo?
Heshima sio kila wakati.
Lakini hiyo haimaanishi kuwa huna thamani.

Hata kama kuna watu wanakutendea mabaya wasamehe tu ... hawaelewi kusudi lako na umuhimu wako kwao

✅ TAII WANATOWEKA… NA NI DHARURA YA DUNIA.

Maendeleo ya kibinadamu yamewafanya tai Kupoteza makazi.
Tai wanakufa kwa wingi.

Na wanasayansi wanalia.

Kwa sababu wanajua nini kitatokeaIkiwa tai watatoweka

Magonjwa mabaya yataongezeka.
Dunia itateseka.

Somo?
Watu tunaowapuuza leo -
Huenda ndio watu hasa wanaoshikilia maisha yetu pamoja na hatima yetu

Heshimu wafanyaji usafi
Waheshimu wazee.
Thamini watu tulivu wanaotumikia bila malipo.

Wakati mwingine, kuishi kwa wengi ...
Inategemea nguvu za wachache.

Good morning Tanganyika
 
TAI HAWAUI, WANAHIFADHI

Hawawindi
Wanasubiri kilichokufa.
Kisha wanakisafisha.
Huu ni wajibu muhimu wa mwisho wa asili. KUHIFADHI.

Mkuu mshana, Tai wanaua wanyama kama sungura, digigi na hata watoto wa mbuzi na kondoo, wakitokeza kwenye eneo wazi, hasa maeneo ya pori lenye miti mirefu na mapango ya milima na mawe. ambapo ndipo makazi ya Tai.
 
nmesoma ila ulipofika kwenye ndoa na mchepuko naona hii ni chai, anyway tunywe tu na haka ka mvua ka asubuhi
JamiiForums-653783758.jpg
 
Mkuu, mbona kama umechanganya sifa za Tai na bundi?

Tai (TISS) wana sifa sawa na bundi?
 
Tai hajawahi kuwa na sifa hizoo, rudi tena ukapekue vizuri ulikotoa hili desaa
 
Leo Mshana jr umejichanganya.,.. ushauri tu kwenye neno Tai weka Bundi...... edit p'se
 
Kwa baadhi ya ya tamaduni tai akitua juu ya paa lako...
Watu watakusanyika na kuanza kutoa maelezo mbalimbali
Wengine Watazomea na kupiga kelele, "Jamani eeh! Nuksi imetua!"😂
Wengine hata wataita waganga wa kienyeji
Na Wengine watafunga na kuomba.

Yote haya ni Kwa nini?
Kwa sababu kuna wazee waliwahi kusema tai ni wajumbe wa kifo.

Lakini ngoja nikuambie ....

Ndege yule yule anayeogopeka..
Huyo huyo tunayemuita mchafu na mwenye nuksi
Ndiye sababu ya sisi sote hatujafa kutokana na magonjwa mbalimbali

Iko hivi
TAI WANAKULA VITU VILIVYOFA… (mizoga) NA NDICHO KINACHOTUFANYA TUWE HAI.

Wanakula mizoga.
Nyama iliyooza.
Wanyama wanaooza.
Vitu ambavyo hakuna mnyama mwingine anayegusa.

Lakini ingekuwaje kama tai asingefanya hivyo?

Kama tai watatoweka leo-
Magonjwa kama vile kimeta, kichaa cha mbwa, nk yangeongezeka.

Kwa mfano yule mbwa aliyegongwa na kufa aliye kando ya barabara?
Nzi watakula.
Funza wataongezeka.
Bakteria watazidi ..Matokeo yake
Kifo kitaingia kwenye mnyororo wa chakula.
Kitaingia hewani.
Kitatuingia.

Lakini tai hutusaidia kuondoa huo uchafu bila kulalamika.. Na wala hatumpongezi
Wanakula kifo ili sisi tuishi.

Somo?
Wakati mwingine, wito wako utakupeleka kwenye maeneo machafu.Yasiyoonekana. na wengi na utaifanya, ili dunia dunia isioze

Sio kila shujaa huvaa manukato.
Wengine wananuka uvundo… ili wengine wapate harufu nzuri.😁
Inaendelea
Hivi kuna tai makundi mangapi?
Je wote wanakula mizoga?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom