Kisa cha mtoto kuliwa na Tai kilivyopelekea mpiga picha wa tukio kujiua kwa sumu kali

NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
917
1,198
Mwaka 1993 mwezi March Mpiga picha maarufu wa Africa kusini (PhotoJournalist) Kevin Carter alitembelea Nchi ya Sudan kwa ajili ya kupiga picha za habari kuhusiana na baa la njaa lililoikabili nchi hiyo.

Ni kipindi ambacho nchi ya Sudan ilikumbwa na baa kubwa sana la njaa hal iliyopelekea watu wengi kufa njaa na wengine wakihangaika kuokoa uhai wao kwa kula Magome ya miti, nyasi na mizizi.

Ni kipindi kibaya sana katika Historia ya Sudan kwa sababu Jumuiya ya kimataifa ilisita kupeleka msaada wa chakula kutokana na hali mbaya ya kisiasa iliyokuwepo Sudan (vita vya wenyewe kwa wenyewe).

Japo baadae umoja wa Mataifa (UN) ulikubali kupeleka msaada wa Chakula lakini watu wengi walikua wameshapoteza maisha kutokana na ba la njaa.

Ni kipindi hiki ndipo Kevin Carter alienda nchini Sudan akifuatana na Mwandishi mwenzie wa kireno João Silva kuripoti ju ya baa la njaa lililoikumba nchi hiyo.

Katika kutekeleza wajibu wake wa kikazi Kevin alifanikiwa kupiga picha ya mtoto mmoja mdogo aliyeshindwa kuendelea na safari ya kuwafuata walezi wake waliokuwa wameenda kupokea chakula cha msaada toka UN. Mtoto huyo alipew jina la Ken.

Ndege za UN zilikua zikidondosha msaada wa chakula kwa wanakijiji wa eneo hilo. Wazazi wa Ken walifariki kwa njaa na yeye kulelewa na jamaa wa karibu.

Siku hiyo walezi wa Ken walienda kuokota chakula cha msaada kilichokuw kikidondoshwa na ndege za UN. Ken alijaribu kuwafuata walezi wake lakini aliishindwa kuendelea na safari katikali y pori kutokana na uchovu, njaa kali, kiu, n mwili kukosa nguvu. Akiwa peke yake porini alianguka.

Akajaribu kuficha kichwa chake ardhini kutokana na jua kali lililokua likiwaka (zaidi ya nyuzijoto 40°C). Hapakuwa na mti wa kujikinga maana miti ilikauka kwa ukame, mingine watu walikula magome wakiwa katika jitihada za kujiokoa na njaa.

Ken hakujua kuwa nyuma yake kulikua n ndege aina ya "tai" ambaye hula mizoga na alikua akimnyemelea. Akiwa pale chi alivamiwa na ndege huyo ambsye alimdonoa sehemu ya utosi na kumuua kabla ya kuanza kula nyama yake kwa kudonoa kama adonoavyo mizoga.

Wakati Ndege huyo akimkaribia Ken, mwandishi wa Habari Kevin Carter alikua na Camera yake akipiga picha. Baadae akachukuliwa na ndege za UN na kumuacha mtoto huyo akiliwa na "tai" bila msaada wowote.

Picha hiyo ilichapishwa kwenye gazeti la New York Times tar.26 March 1993 na kuibua mjadala mkubwa juu ya maadili y taaluma ya upigaji picha za habari (Ethic of Photojournalism).

Wengi walilaumu kitendo cha Kevin Carter kupiga picha na kuacha kuokoa maisha ya mtoto yule. Katika utetezi wake Carter alisema hakujua kama tai yule angemshambulia Ken.

Aliongeza kuwa alisubiri kwa muda wa dakika 20 kuona kama tai yule angerush mbawa zake kumsogelea Ken. Alipoona tai huyo hamsogelei mtoto huyo aliamua kuondoka kwa ndege maalum za UN zilizokua zikitoa msaada eneo hilo na kumuacha mtoto Ken peke yake. Lakini baadae akaambiwa kuwa mtoto huyo alidonolewa na tai hadi kufa.

Taarifa nyingine zinadai kuwa Carter alikua akitekeleza kazi aliyopewa na muajiri wake, kwamba akifika Sudan afanye kazi moja tu ya kupiga picha na alizuiwa kufanya kazi ya uokoaji kwa sababu hakwenda Sudan kwa kazi hiyo.

Pamoja na hayo yote Carter alitunukiwa tuzo kwa Picha hii, mnamo mwezi April mwaka 1994 kwenye tuzo maarufu za Pulitzer. Picha hii ilipewa tuzo ya kuwa picha bora ya makala (Feature Phoyograph).

Lakini Carter hakuifurahia tuzo hiyo kutokana na kukosa utu ambao ulipeleke kifo cha mtoto Ken. Aliishi maisha ya masononeko na kujilaumu kila mara kwa kushindwa kuokoa maisha ya mtoto yule

Aliomba radhi kwa kusema ''kwakweli naomba msamaha kwa kutomuondoa mtoto huyo katika mazingira ya hatari (“I’m really, really sorry I didn’t pick the child up,”).

Tar.27 mwezi July mwaka 1994 (miezi minne tu baada ya kupokea tuzo) Kevin Carter aliamua kujiua kwa sumu ya Carbon Monoxide (Carbon monoxide poisoning) kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na historia ya Sudan ya kifo cha mtoto Ken.

Kevin Carter alilipwa fedha nyingi sana na gazeti la New York Times kwa picha ile. Hali kadhalika alipewa tuzo ya heshima kwa upigaji picha bora, lakini baadae akaona vyote havina thamani kwa kitendo alichokifanya kwa kukosa utu.
Kabla ya kujiua Carter aliandika ujumbe kwenye kipande cha karatasi akisema "Maumivu ya moyo yanazidi furaha ya fedha" (The pain of heart overweigh the joy of getting money)...

.... Najisikia vibaya sana, kumbukumbu za mauaji, njaa na mateso ya mtoto Ken zinanijia kila mara. Naenda kumfuata na kumuomba msamaha kama nitapata bahati ya kufanya hivyo... ( I am so depressed ... I am haunted by the vivid memories of killing, anger and pain of starving child Ken... I have gone to join him and ask for forgiveness if that opportunity arrise.)

Kevin%2BCarter's%2BPulitzer%2BPrize-winning%2Bphotograph.jpg
 
inasikitisha sana wanadamu tunapta kwenye vpindi vigumu sana
 
Picha hiyo nimekuwa nikiiona mara nyingi ila sikuwa na taarifa ya kutosha juu yake. Asante sana. Umetupa somo muhimu.
 
Hiyo picha inaonyesha kabla Tai ajafanya kitendo cha kumuua. Kwann huyo mpiga picha asinge mfukuza?
 
Hiyo picha inaonyesha kabla Tai ajafanya kitendo cha kumuua. Kwann huyo mpiga picha asinge mfukuza?
Anadai alidhani Tai hatamdhuru mtoto...kitendo hicho kilimfanya akose amani moyoni mwake kila alipokumbuka,,,,,,,pamoja na kupewa tuzo ya picha bora lakini aliona bora ajiue..
 
Hiyo picha inaonyesha kabla Tai ajafanya kitendo cha kumuua. Kwann huyo mpiga picha asinge mfukuza?
Hiyi picha hua inapotoshwa sana, kwa kifupi huyo mtoto hakuliwa na tai, ingekua ni uwendawazimu kwa mwandishi kupiga picha huku mtoto akiendelea kuliwa. ukitaka maelezo zaidi jaribu kujisomea hata wikipedia
 
Pulitzer Prize photograph in Sudan
Main article: The vulture and the little girl
Carter shot an image of what appeared to be a little girl, fallen to the ground from hunger, while a vulture lurked on the ground nearby. He told Silva he was shocked by the situation he had just photographed, and had chased the vulture away. A few minutes later, Carter and Silva boarded a small UN plane and left Ayod for Kongor.

Sold to The New York Times, the photograph first appeared on 26 March 1993, and syndicated worldwide. Hundreds of people contacted the newspaper to ask the fate of the girl. The paper said that according to Carter, "she recovered enough to resume her trek after the vulture was chased away" but that it was unknown whether she reached the UN food center." In April 1994, the photograph won the Pulitzer Prize for Feature Photography.

In 2011, the child's father revealed the child was actually a boy, Kong Nyong, and had been taken care of by the UN food aid station. Nyong had died four years prior, c. 2007, of "fevers", according to his family.
 
Back
Top Bottom