Tahrir Square ya Tanzania

Tahrir Square ya Tanzania

Naona Watanzania tumechoka na amani.

Upinzani walijenga hoja nzuri sana ya kuutokomeza UFISADI ambayo karibuni iing'oe CCM. Lakini walifanya kosa kubwa la kiufundi kwa kumleta Lowassa kama kinara wao.

Kuanzia pale upinzani wamejaribu sana kuisambaratisha serikali ya Magufuli kwa kutumia kila mbinu za kisiasa lakini wanaona wameshindwa kabisa. Hii ni dhahiri ukiangalia wananchi wa kawaida walivyorudi kuipenda CCM kwa kura wanazowapa.

HATARI
Sasa upinzani, wakiongozwa na CDM (na namshangaa Zitto nae pia yumo) wameamua kuwatumia wananchi (mithili ya UKUTA) kuleta vurugu nchi nzima kwa migomo na maandamano. Wanataka kutumia fujo hizi ili nchi isitawalike. Hiki kitu ni hatari sana.

Ni matumaini yangu kuwa Watanzania watayapuuza matakwa yao haya, kama walivyowapuuza kwa kuwakataa wagombea wao katika chaguzi hizi ndogo.

Hivi watu wana akili za kivipi? Mange yupo Marekani full-kiyoyozi anawashakiza muingie mitaani kupinga serikali na nyie kweli mnaitikia. Atakaelambwa virungu, maji ya washawasha, mabomu ya machozi, na risasi za moto ni nyie na watoto wenu.

Kwa kipi lakini?
Kwa sababu Mbowe na genge lake la wahuni wameishiwa na mbinu halali za kisiasa za kuchukua dola?
Au ni kwa sababu Mbowe na upinzani kwa ujumla wamekwishabaini kuwa, kwa mwendo huu ifikapo 2020 hawatapata wabunge wala madiwani na ndio itakuwa mwisho wa ruzuku?

Vijana msikubali kutumiwa na watu, hasa walioko nje ya nchi, kuvunjisha amani. Wenzenu wamekaa ndani na wanaangalia kinachoendelea mitaani kama sinema vile. Mwisho wa siku sio Mbowe, Zitto, au Mange atakaeumia au kufa. Ni wewe unaeshakizwa kama mbwa ukaumie ili waone machafuko.

Kuandamana ni hiari yako. Lakini kabla hujatoka nyumbani na kuingia mitaani jiulize, NINAPIGANIA KITU GANI HASA. Kama ukijiridhisha kuwa kuna maslahi yako ya kupigania basi endelea la sivyo ujue unatumiwa.
 
Nakumbuka Kenya waliweza kukutana mpaka kumwapisha Raila pamoja na ubabe wa polisi wao japo haikua na umaana sembuse wangekuwa wanadai katiba!! Kunanchi watu hawataki ujinga kabisa.
 
Waishaongea mangapi?
Kila maandamano na malengo yake kulikuwa na maandamano ya kudai cost sharing, ya kudai kuachiwa kwa mashehe, ya kudai kudhulumiwa viwanja, ya wamachinga kudai maeneo ya kufanyia biashara zao nk nk, Ila haya ni maandamano ya kuung'oa udikteta na dikteta mwenyewe.
 
Nakumbuka Kenya waliweza kukutana mpaka kumwapisha Raila pamoja na ubabe wa polisi wao japo haikua na umaana sembuse wangekuwa wanadai katiba!! Kunanchi watu hawataki ujinga kabisa.
"Our first option is Uhuru Park, second option Uhuru Park and third option Uhuru Park...," he said during an interview on KTN.

"If all options are not possible, then our last option will be Uhuru Park .. the swearing-in is a fight that we are willing to take. We have no intention of changing the venue for the ceremony."
 
Kudhihirisha maandamano ya Mange kimambi hayawezekani hata huu Uzi wachangiaji wachache

Sasa kama , watuamiaji ID fake wanakuwa waoga kuchangia Je maandamano halisi wataweza
 
Hata wakati wa mapinduzi ya Libya mitandaoni walikuwepo watu kama wewe, nikukumbushe tu kauli ya Membe aliyekuwa waziri wa mambo ya nje naye alikuwa akibeza kuwa 'nchi haiwezi kupinduliwa kwa pickup', kilichotokea ni historia.
Jeshi la nchi za kiarabu walicheka na ngedere,Ngedere wanaingia shamba La tahrir Square serikali inawakodolea macho tu .Hadi watu walikuwa wakipanda vifaru vya jeshi na kutukana serikali

Hapa ukisema unaandamana labda uandamane porini kwenye barabara lazima uwe na kibali kwa sheria za usalama barabarani .Huwezi kuibuka TU BIN VUU uko barabarani unatakiwa utii sheria bila shuruti haraka kwa spidi ya umeme UACHIE BARABARA.Huwezi zuia watu kufanya shughuli zao za kiuchumi kisa makalio yako yanaandamana.Sheria tu ya usalama barabarani inatosha kukuvurumishia makombora kukuondoa barabarani kama unaingia kinguvu.Barabara ipi utaingia bila kibali ya waarabu usiyalete Tanzania.Kule polisi anabembeleza waandamaji sweet ,my love nawasihi msiandamane ,I love you.Nyooo sio Tanzania hii nchi nyingine
 
Mtu yuko JF au insta kwa Mange ndo anajua Tanzania nzima iko hapo. Tanzania ni nchi inayoongozwa na matukio na huwa na tension kubwa mno lkn haipiti wiki watu wanaendelea na story mpya
 
Pale pembezoni mwa bahari ya hindi nyuma ya ikulu wanapofanyiaga gwaride.
 
Hivi kabisa inamaana hujaona wizi wa kura katika uchaguzi huu uliopira juzi? hujaona makada wa ccm wakisimamia uchaguzi? hujaona watu wakipogwa na wengine kuuwawa? shame be upon you.
 
Waacheni watu waandamane kwa amani na kutoa hisia zao kama wale wa Kenya pale Uhuru park walio kusanyika zaidi ya milioni na hakuna aliyerudi nyumbani na jeraha
Hamia kenya basi, Kenya na Tanzania ni nchi tofauti zenye majina tofauti na mambo tofauti. Tanzania is not a Copy cat of Kenya
 
Hata mkianza kuuwa hawatazidi mia au miambili wengine watapona na mtakuwa mmeshakimbia. Watakaobaki wataishi kwa amani na uhuru
 
Sehemu moja kwa Dar si nzuri.
Several places simultaneously will work wonders if at all it happens.
 
Pale pembezoni mwa bahari ya hindi nyuma ya ikulu wanapofanyiaga gwaride.
Karibu sana mpendwa
performance-with-crocodiles-at-samphran-elephant-ground-near-bangkok-bg6pmg.jpg
 

Attachments

  • upload_2018-2-19_17-42-41.jpeg
    upload_2018-2-19_17-42-41.jpeg
    8.8 KB · Views: 29
Back
Top Bottom