Pole sana ndugu yangu, hii ndiyo BONGOland! Yaani siku hizi watu wanadhani picha ni mali. Nilikuwa nawaambia wale macurator wa huko Makumbusho kwamba wengine tumebahatika kufika katika museum kubwa tu za France na Italy na USA, na unapiga picha nje na katika baadhi ya maeneo uanweza ukaambiwa usipige picha kwa kutumia flash. Hata Last Supper ya Leonardo Da Vinci nilienda kuiangalia - the original one in Italy na tuliipiga picha bila tatizo ingawa bila flash! Sasa hapa ndo tunajifanya tunajua kuzuia picha, alafu uliza hizo pesa zinatumika vipi? Watapata kigugumizi.
duh!! wanachaji!!!this is terrible!! ila nna wasiwasi, hawakuwa watoto wa mjini kweli hao??? manake bongo bwana lolote linawezekana.hako kanchi ketu kuna vifisadi vidogovidogo kila kona
Mzee wa jicho moja, habari za Izrael?
Hawa akina mama walikuwa wamesimama na ticket zao kwa watu wanaoingia ndani basi unalipia. Sasa sijui ukipiga picha unapata risiti gani. Sikuwa na muda kwani siku ya jumatano ndiyo nilikuwa naondoka na mvua iliyonyesha sikuwa na hamu ya kubishana na PUMBAVU, watu watashindwa kuona tofauti.
Next time ntawaingilia asubuhi na timu yangu ya matapeli. Tutasumbuana nao siku nzima hadi somo lieleweke. Ikibidi hadi kwa waziri tutafika siku hiyo huku tukiwa na waandishi wa habari kama wapambe na timu ya watu wa HAKI ZA BINADAMU. Upuuzi mwingine inabidi kuushambulia kwa juhudi zote.
The Centre Will Require The Following Basic Documents In Order To Process Your Application:
1. 3 copies of the projects Business Plan/Feasibility Study
(The intended project should aim at foreign exchange generation and savings, import substitution, creation of employment opportunities, linkage benefits, transfer of technology, expansion of production of goods and services etc)
We expect your feasibility study to contain the following information, clear statement of the project objective, information regarding the investor (profile), details of investment costs (foreign and local expected capital expenditure), how the proposed investment will be financed, specific sources(s) of finance for the project, terms and conditions of the loan if applicable, sources of technology if applicable, project financial and economic analysis, market study, project capacity, production process if applicable, environmental impact assessment, expected employment generation, proposed implementation schedule, etc
2. 3 dully filled copies of TIC application forms which are issued by the Centre at a fee of US$ 100
3. Incase of expansion/rehabilitation, a copy of audited account for the past three years.
4. A copy of the companys Memorandum and Articles of Association.
5. A certified copy of the Certificate of company Incorporation
6. A brief profile of investors(s)
7. Evidence of sufficient finance capital available to implement the project
8. Evidence of land ownership for the location of the project
9. Company Board Resolution to register the project with TIC
10. Project implementation schedule
11. An overall covering letter to which all the above are attached.
**** All applications are officially submitted to TIC Registry Department, located in Tanzania Investment Centres Office, along Shaaban Robert Street, Plot No. A & B, Dar es Salaam
You are further advised to prepare yourself for a fee of US$ 750 for the Certificate of Incentives in the event that you have qualified and been informed that your project shall be granted the Certificate of Incentives.
Kuna viwili hapa:
2. Kuendelea kupigana vita na makaburu. Huu wakati wa Google Earth kweli unakaa kuzuia watu kupiga picha daraja la salenda! maaskari sasa wamefanya mradi. Kwa wenzetu hata airport wewe piga tu maana wanajua hamna cha ajabu utakachoweza kufanyia wakati picha zimejaa kwenye mtandao. kwa mtazamo huu, hilo ongezeko la utalii tutalisikia redioni.
Ndiyo maana Mlima Kilimanjaro unaaminika ni wa Kenya yote hii sababu yake ni UBUBU wetu. "NI SIRI" st....id philosophy.Wana Mtandao.
Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii. Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.
Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH. Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?
Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe. Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.
Bubu Msemaovyo. Sitoshangaa kusikia kuna watalii wanatolewa upepo kwa kuupiga picha mlima Kilimanjaro bila kibali!
hakuna marashi ya kufunika harufu ya ushuzi uliooza
Haswaaaa. Nimekuwa nafanya utafiti binafsi wa jinsi tulivyo butu katika kutoa MATANGAZO MAZURI YENYE KUVUTIA, iwe ni kupitia radio, magazeti ama TV. Ukilinganisha na wenzetu Wakenya na Waganda, sisi Watanzania tuko nyuma sana kutoa matangazo achilia mbali matangazo yenye kuvutia lakini pia ile nia ya kutangaza biashara. Hatujui. Mara nyingi matangazo yetu mathalani tunatangaza SABUNI huanza na nyimbo na huishia kibwagizo cha "...SABUNI HII NI KIBOKO CHA UCHAFU. Kama tutatangaza aina fulani ya KINYWAJI basi tutanza na wimbo na kibwagizo chake kitakuwa"....Kinywaji hiki ni KIBOKO cha KIU TANZANIA" HIVI KWANINI MATANGAZO YETU YANAKIBWAGIZO "KIBOKO" Je ina maana hatujui kujitangaza? sasa tunasomea nini katika masuala ya biashara katika kuzitangaza? Hadi nimechoka kusikia Hiki ni Kiboko cha...." TUBADILIKE JAMANI
Fundi, umenikumbusha ishu ya airport! Eti tulikuwa tunamwaga mtu na kupiga picha, askari akaja kutuambia eti haturuhusiwi kupiga picha na kwamba eti utawala lazima wapewe taarifa, blablah. Tulimtoa nduki huyo askari mpaka akaamua kupiga patroli kwingine. Yaani ujinga huu wa kuona picha ni mradi ni ujinga!
Lakini vitu vyoet hivi vinatokana na fikra za zamani na ujanja wa watoto wa mjini!
October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.
October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.