TAHADHARI ya “Usipige Picha” nchini Tanzania na dunia ya leo

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,060
Wana Mtandao.

Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii.

Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.

Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH.

Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?

Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe.

Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.
 
Pole sana ndugu yangu, hii ndiyo BONGOland! Yaani siku hizi watu wanadhani picha ni mali. Nilikuwa nawaambia wale macurator wa huko Makumbusho kwamba wengine tumebahatika kufika katika museum kubwa tu za France na Italy na USA, na unapiga picha nje na katika baadhi ya maeneo uanweza ukaambiwa usipige picha kwa kutumia flash. Hata Last Supper ya Leonardo Da Vinci nilienda kuiangalia - the original one in Italy na tuliipiga picha bila tatizo ingawa bila flash! Sasa hapa ndo tunajifanya tunajua kuzuia picha, alafu uliza hizo pesa zinatumika vipi? Watapata kigugumizi.
 
Susuviri, utafikiri ulikuwepo. Sasa mie sikuwa na muda na nilitaka kupiga tu majengo kwa nje. Ni kweli kabisa jamaa huwa hawaruhusu FLASH. Hii hata uwe na pesa kiasi gani. Sasa kule kwetu ulimbukeni kweli unatisha. Wanafikiri kila mzungu ni tajiri na kumbe wengine ni jua kali tu kama sisi ila anahamu ya kuja Africa na akifika huko na mapenzi yake yote wanafikiri ni BUZI, basi hao wako tayari kuchuna. Niliwaambia MTAKUFA MASIKINI kwa mwendo huu. Hongera kwa kufika na kuona kazi ya Da Vinci. Mie si mpenzi sana ingawa pia nilishafika na kusikia hilo Tangazo la NO FLASH. Labda kuna viongozi wa juu watasoma hili na kulifanyia kazi maana kwa kweli hii njaa inatuvua sasa nguo.
 
duh!! wanachaji!!!this is terrible!! ila nna wasiwasi, hawakuwa watoto wa mjini kweli hao??? manake bongo bwana lolote linawezekana.hako kanchi ketu kuna vifisadi vidogovidogo kila kona
 
duh!! wanachaji!!!this is terrible!! ila nna wasiwasi, hawakuwa watoto wa mjini kweli hao??? manake bongo bwana lolote linawezekana.hako kanchi ketu kuna vifisadi vidogovidogo kila kona

Mzee wa jicho moja, habari za Izrael?
Hawa akina mama walikuwa wamesimama na ticket zao kwa watu wanaoingia ndani basi unalipia. Sasa sijui ukipiga picha unapata risiti gani. Sikuwa na muda kwani siku ya jumatano ndiyo nilikuwa naondoka na mvua iliyonyesha sikuwa na hamu ya kubishana na PUMBAVU, watu watashindwa kuona tofauti.
Next time ntawaingilia asubuhi na timu yangu ya matapeli. Tutasumbuana nao siku nzima hadi somo lieleweke. Ikibidi hadi kwa waziri tutafika siku hiyo huku tukiwa na waandishi wa habari kama wapambe na timu ya watu wa HAKI ZA BINADAMU. Upuuzi mwingine inabidi kuushambulia kwa juhudi zote.
 
habari za huku nzuri mkuu, a bit dry day at 66F.hao watu inabidi uwafate wakupe majibu mazuuuri.manake hai-make sense kabisa kuwachaji watu pesa kwa kupiga picha, kwanza hiyo ni moja ya njia ya kutangaza utalii.ukirudi ukawakomalie bwana
 
Kuna viwili hapa:
1) Kutokujua masuala ya biashara. Kuna idara za serikali bado wanauza fomu! Hii hapa kutoka Tanzania Investment Centre.

The Centre Will Require The Following Basic Documents In Order To Process Your Application:

1. 3 copies of the project’s Business Plan/Feasibility Study

(The intended project should aim at foreign exchange generation and savings, import substitution, creation of employment opportunities, linkage benefits, transfer of technology, expansion of production of goods and services etc)

We expect your feasibility study to contain the following information, clear statement of the project objective, information regarding the investor (profile), details of investment costs (foreign and local expected capital expenditure), how the proposed investment will be financed, specific sources(s) of finance for the project, terms and conditions of the loan if applicable, sources of technology if applicable, project financial and economic analysis, market study, project capacity, production process if applicable, environmental impact assessment, expected employment generation, proposed implementation schedule, etc

2. 3 dully filled copies of TIC application forms which are issued by the Centre at a fee of US$ 100
3. Incase of expansion/rehabilitation, a copy of audited account for the past three years.

4. A copy of the company’s Memorandum and Articles of Association.

5. A certified copy of the Certificate of company Incorporation

6. A brief profile of investors(s)

7. Evidence of sufficient finance capital available to implement the project

8. Evidence of land ownership for the location of the project

9. Company Board Resolution to register the project with TIC

10. Project implementation schedule

11. An overall covering letter to which all the above are attached.

**** All applications are officially submitted to TIC Registry Department, located in Tanzania Investment Centre’s Office, along Shaaban Robert Street, Plot No. A & B, Dar es Salaam

You are further advised to prepare yourself for a fee of US$ 750 for the Certificate of Incentives in the event that you have qualified and been informed that your project shall be granted the Certificate of Incentives.

Tunakamua hata pale ambapo hapana haja. Wenzao fomu zipo kwenye mtandao, una'download' kwa kadri unavyotaka. hawa jamaa wanataka dola 100 ingawa kwenye homepage wameonyesha kuna fomu za ku'download'.

Hapo makumbusho unaambiwa ukiwa na camera ya kawaida ni bure lakini digital wanataka mpango! Halafu wanalalamika watalii hawaji. Watakujaje kwa mpango huu? Watu wanaenda mahali mara nyingi kutokana na simulizi za wenzao na picha wanazoleta kutoka huko. Hili wenzetu hawalioni. Nyumba zinaanguka kwa kukosa matengenezo na akitokea mwenye mapenzi nazo wanaanza kumbughudhi!

2. Kuendelea kupigana vita na makaburu. Huu wakati wa Google Earth kweli unakaa kuzuia watu kupiga picha daraja la salenda! maaskari sasa wamefanya mradi. Kwa wenzetu hata airport wewe piga tu maana wanajua hamna cha ajabu utakachoweza kufanyia wakati picha zimejaa kwenye mtandao. kwa mtazamo huu, hilo ongezeko la utalii tutalisikia redioni.
 
Fundi, umenikumbusha ishu ya airport! Eti tulikuwa tunamwaga mtu na kupiga picha, askari akaja kutuambia eti haturuhusiwi kupiga picha na kwamba eti utawala lazima wapewe taarifa, blablah. Tulimtoa nduki huyo askari mpaka akaamua kupiga patroli kwingine. Yaani ujinga huu wa kuona picha ni mradi ni ujinga!

Suala la kuuza fomu ni vichekesho lakini nadhani itabidi tuanzishe mada nyingine maana tukianza kuangalia fomu zinazouzwa Bongo utacheka!
Lakini vitu vyoet hivi vinatokana na fikra za zamani na ujanja wa watoto wa mjini!
 
jamani kuna sheria ambazo bado ziko vitabuni ndio vimesababisha mambo haya. Miye nakumbuka pale Chuo cha Ualimu Korogwe miaka hiyo kulikuwa na bango kubwa ati "Hairuhusiwi kupiga Picha"! Sijui tulikuwa tunaficha vitu gani kwenye vyuo vya walimu.
 
Kuna viwili hapa:
2. Kuendelea kupigana vita na makaburu. Huu wakati wa Google Earth kweli unakaa kuzuia watu kupiga picha daraja la salenda! maaskari sasa wamefanya mradi. Kwa wenzetu hata airport wewe piga tu maana wanajua hamna cha ajabu utakachoweza kufanyia wakati picha zimejaa kwenye mtandao. kwa mtazamo huu, hilo ongezeko la utalii tutalisikia redioni.

Fundi mchundo mwenzangu,
Umesema juu ya DARAJA la Sarenda na kwa hasira nimeingia kwenye GOOGLE EARTH na kuliona. Tena mjinga mmoja ajiitaye Aman kawewa na picha Hihiiii :) Nafikiri mmesema kweli kuwa kuna mawili yaani moja ni ushamba na mbili ni watoto wa mjini. Anyway ni kutafuta uwezekano wa wahusika kuambiwa na kuondoa uhuni huu. Iwe imeandikwa kabisa kuwa kama sehemu haijaindikwa basi Tanzania kama nchi ya kitalii ni RUKSA.
 
Wana Mtandao.
Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii. Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.

Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH. Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?

Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe. Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.
Ndiyo maana Mlima Kilimanjaro unaaminika ni wa Kenya yote hii sababu yake ni UBUBU wetu. "NI SIRI" st....id philosophy.
 
Bubu Msemaovyo. Sitoshangaa kusikia kuna watalii wanatolewa upepo kwa kuupiga picha mlima Kilimanjaro bila kibali!
 
Bubu Msemaovyo. Sitoshangaa kusikia kuna watalii wanatolewa upepo kwa kuupiga picha mlima Kilimanjaro bila kibali!

Haswaaaa. Nimekuwa nafanya utafiti binafsi wa jinsi tulivyo butu katika kutoa MATANGAZO MAZURI YENYE KUVUTIA, iwe ni kupitia radio, magazeti ama TV. Ukilinganisha na wenzetu Wakenya na Waganda, sisi Watanzania tuko nyuma sana kutoa matangazo achilia mbali matangazo yenye kuvutia lakini pia ile nia ya kutangaza biashara. Hatujui. Mara nyingi matangazo yetu mathalani tunatangaza SABUNI huanza na nyimbo na huishia kibwagizo cha "...SABUNI HII NI KIBOKO CHA UCHAFU. Kama tutatangaza aina fulani ya KINYWAJI basi tutanza na wimbo na kibwagizo chake kitakuwa"....Kinywaji hiki ni KIBOKO cha KIU TANZANIA" HIVI KWANINI MATANGAZO YETU YANAKIBWAGIZO "KIBOKO" Je ina maana hatujui kujitangaza? sasa tunasomea nini katika masuala ya biashara katika kuzitangaza? Hadi nimechoka kusikia Hiki ni Kiboko cha...." TUBADILIKE JAMANI
 
Hao viongozi wetu hata ramani ya nchi yetu hawaijui vizuri, ndio maana hata wanapotaka kuitangaza, wanashindwa wafanye nini.
hakuna marashi ya kufunika harufu ya ushuzi uliooza
 
Haswaaaa. Nimekuwa nafanya utafiti binafsi wa jinsi tulivyo butu katika kutoa MATANGAZO MAZURI YENYE KUVUTIA, iwe ni kupitia radio, magazeti ama TV. Ukilinganisha na wenzetu Wakenya na Waganda, sisi Watanzania tuko nyuma sana kutoa matangazo achilia mbali matangazo yenye kuvutia lakini pia ile nia ya kutangaza biashara. Hatujui. Mara nyingi matangazo yetu mathalani tunatangaza SABUNI huanza na nyimbo na huishia kibwagizo cha "...SABUNI HII NI KIBOKO CHA UCHAFU. Kama tutatangaza aina fulani ya KINYWAJI basi tutanza na wimbo na kibwagizo chake kitakuwa"....Kinywaji hiki ni KIBOKO cha KIU TANZANIA" HIVI KWANINI MATANGAZO YETU YANAKIBWAGIZO "KIBOKO" Je ina maana hatujui kujitangaza? sasa tunasomea nini katika masuala ya biashara katika kuzitangaza? Hadi nimechoka kusikia Hiki ni Kiboko cha...." TUBADILIKE JAMANI

Lile Tangazo la Utalii la Tz kwenye CNN kwa kweli linasababisha mtu ubadili chanel. Tangazo hili linatakiwa liwe kwa Watanzania watembelee mbuga zao na si watalii. halina tofauti na matangazo ya India, Malesia true Asia, Thailand, nk. Ukija ya Tanzania ongeza neno BUREEE. Kila kitu wao ni BUREE.

Nafikiri kwenye level ya kimataifa inabidi tangazo lako liwe fupi na kali saana. kikubwa zaidi liwe na kitu kimoja cha ajabu ambacho hakuna watu wameshawahi kukitumia na kila atakayeona basi MILELE ATAKUMBUKA. Mie hapa huwa nina wazo langu zuri tu la kuitangaza Tz na kwa kweli hata BUSH akiliona atacheka saana. Anyway nimeliweka kichwani mwangu na siku moja nikja pata fursa watu walinunue basi ntaliuza na kuomba mwenyewe kucheza kwenye hili Tangazo. Ila nina uhakika kwa asilimia 95% kuwa kila atakayeona basi kuanzia siku hiyo atajua TANZANIA ni nini.

Nafikiri haya matangazo mengine watu wanapeana tu. Mtu anachukua pesa kwa kazi isiyoeleweka. Ndiyo maana watu wanasema watoto wa mjini. Kama watu wameipa RICHMOND ilete umeme, sembuse matangazo ya biashara? Huko itabidi ipite miaka.
 
poleni sana kwa nyusumbufu hizo, wakuu huenda wakawa weshasikia malalamiko haya au kupelekwa kwao tuombe mungu awawezeshe kufanya mabadiliko ya maana kwa maslahi ya taifa
 
Fundi, umenikumbusha ishu ya airport! Eti tulikuwa tunamwaga mtu na kupiga picha, askari akaja kutuambia eti haturuhusiwi kupiga picha na kwamba eti utawala lazima wapewe taarifa, blablah. Tulimtoa nduki huyo askari mpaka akaamua kupiga patroli kwingine. Yaani ujinga huu wa kuona picha ni mradi ni ujinga!

Lakini vitu vyoet hivi vinatokana na fikra za zamani na ujanja wa watoto wa mjini!

October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.
 
October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.

Mbalamwezi, naona hawa jamaa au kuna MJINGA fulani huko aliona aweke au wamekisahau tangu ule wakati wa UKOMINISTI hadi leo. Haingii akilini dunia ya leo kukataza watu wasipige picha wakati unaweza kununua picha yoyote na tena imepigwa unavyotaka kwa kutumia satelite. Anyway nafikiri ulitakiwa kumuuliza POLISI yeyote pale kama kile kibao kweli kina maana yoyote katika karne hii ya 21 au kipo ili KINYANYASE wasiojua kusoma.
 
October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.

Inawezekana. Wanakataza hata kupiga ndani?
Sasa sisi hata vibao hatuweki! Unamkataza mtu kupiga picha majengo ati ni ofisi za serikali unategemea nini? Sehemu kubwa ya mji ni majengo na yanayovutia ni yale ya kihistoria kwa hiyo ni lazima mtalii atataka kuyapiga. Ukikimkataza unaondoa sehemu kubwa ya furaha yake ambayo ni kuweka kumbukumbu safari yake.
 
Hili ni swali na jibu huko BUNGENI. Huyu Waziri wa ulinzi sijui kama alikuwa anajua nini anajibu katikamdunia hii ya leo. Hivi hilo daraja analosema wasipige watu picha si unaweza kuliona kwenye GOOGLE EARTH? Kama kuna mawaziri au wabunge watasoma hii mada basi waende na kusema BUNGENI kuwa hii kitu imepitwa na wakati. Wafikiri njia nyingine za kulinda na si kuandika USIPIGE PICHA....
Hon. Rosemary Kasimbi Kirigini [ CCM ]
Special Seat
Supplementary Question Number Sector Date Asked
PUBLIC SECURITY AND SAFETY Security 12 April 2007
Ahsante sana Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi. Nianze tu kwa kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa. Lakini ningependa tu Mheshimiwa Naibu Waziri aelewe kwamba tunapoleta maswali ndani ya Bunge hili tayari tunakuwa tumepata malalamiko kutoka kwa wananchi wetu na vile vile tumefanya uchunguzi kuhusiana na tatizo ambalo tumewasilishiwa na wananchi wetu. Pale darajani zipo nyumba mbili ambazo zilikuwa zinatumika wakati wa ujenzi wa daraja lile lakini nyumba zile zimeachwa na sasa hivi hazitumiki na kitu chochote. Kwa nini nyumba hizi zisitumike na kukarabatiwa na Wizara husika ili ziweze kutumika na polisi ili kupunguza ile adha ya polisi kutoka Musoma Mjini kuja kulinda daraja hilo au kutoka Tarime Mjini kuja kulinda daraja hilo?

Swali la pili, katika daraja hilo hilo kuna tangazo ambalo linasema kwamba hairuhusiwi kupiga picha darajani hapa. Lakini pale kumekuwa na watalii ambao wanatoka Kenya wakielekea mbuga za wanyama Serengeti, wamekuwa wakisimama darajani pale na kupiga picha. Je, Wizara husika haioni kwamba suala hilo ni hatari kwa nchi hususan Mkoa wa Mara na wananchi wake wanaoishi katika maeneo yale? Ahsante.
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #
Answer From Hon. Mohamed , Mohamed Aboud PUBLIC SECURITY AND SAFETY
NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA:

Mheshimiwa Spika, ni kweli upo umuhimu mkubwa wa kuimarisha ulinzi hasa katika maeneo nyeti yakiwemo madaraja. Lakini ni ukweli usiopingika katika nchi yetu yapo madaraja mengi sana. Kwa hiyo, tukiamua kila kwenye daraja kupeleka askari polisi sifikiri kama tutakuwa na uwezo wa askari hao kuweza kufanya kazi nyingine za kupambana na uhalifu.

Nafikiri Mheshimiwa Mbunge ungekubaliana na mimi kwamba hii mbinu inayotumika sasa ya kufanya doria na ulinzi shirikishi pamoja na mbinu zingine za kiaskari ziendelee kutumika. Hata ushauri wake kuhusiana na nyumba hizo tumeuchukua, tutautafakari ili tuone nini tunaweza kufanya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Kuhusu watalii wanaopiga picha pale darajani mahala ambapo pameandikwa si ruhusa kupiga picha, maana yake si ruhusa kupiga picha. Kwa hiyo, hatua na utaratibu wa kisheria utachukuliwa ili kukomesha jambo hilo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom