TAHADHARI ya “Usipige Picha” nchini Tanzania na dunia ya leo

Je tahadhari hii ina umuhimu wowote enzi ya Google maps?

Google maps inakupa detailed aerial view ya eneo linaonyesha Nyumba, barabara na location co ordinates details zaidi ya picha za kupiga ardhini i.e. ground photos.

Tahadhari ya Usipige picha hapa imepitwa na maendeleo ya teknologia.
 
Je serikali inaweza kuamuru google kufifisha picha za setilati zinaonesha maeneo nyeti kwa usalama wa taifa?
 
Kwa nchi za ulimwengu wa kwanza nafikiri maeneo mengine nyeti hayapigiki picha hata na hao google! Kama wanaweza kutatiza simu kwanini isiwe picha!
 
HURUHUSIWI KUPIGA PICHA ENEO HILI.

Labda wanamaanisha zile za insta, ila si zile za matumizi.
 
HURUHUSIWI KUPIGA PICHA ENEO HILI.

Labda wanamaanisha zile za insta, ila si zile za matumizi.

Hayo makatazo yapo...mwaka jana tulikuwa safarini toka Dodoma kwenda Iringa kupitia Mtera...kuna jamaa safari yao iliishia pale getini (bwawa la mtera) baada ya kutumia simu zao kupiga picha
 
kwa kweli tangazo la aina hiyo halina maana kwa technology ya sasa. maana with Google Earth unaona picha of any location on earth including important information of like coordinates, elevations, topography, and distances to deferent references. Kimsingi ina wabughudhi au kuonea watu wasiotaka au wasiojua kutumia technology za kisasa.
 
Google map unaweza kuona hadi pentagon na white house. Ila makatazo bado yapo mfano ni hapo us Embassy Dsm.
 
Ha haa!
Ukiwakuta wako bize na kugongelea vile vibao vyao eti, 'Usipige picha hapa'! Utadhani wamefanya kikuubwa.... Ila sasa kwa vile teknolojia imebadilika, kupitia google Earth unaweza ukaona inside out jinsi mazingira yao yalivyo...
Mimi nawashauri waaachane na mambo ya kizamani, waruhushu tu watu waje na vidio camera zao wajiachie maana hakuna kilichofichika.
La sivyo wawafuate google earth wawatie virungu... Samahani lakini!

Picha kwa hisani ya google earth...
live picture.png
 
Mnanikumbusha vile vibao kule chuo cha polisi moshi. Ccp. "Usipige picha hapa" ukienda mbele mbele kidogo unakuta kingine, hili ni eneo la jeshi la polisi 'tembea kikakamavu"
 
Hata uzinzi pia umekatazwa mbona watu wanaufanya sana na wanaupenda sana, na laiti bao lingekuwa na mlio kama risasi je usiku tungelala, si ingekuwa kama vita?
 
nakumbuka mwaka 2012 nilipiga picha mlimani city mlinzi alinifata nduki sikujua ni nini bali alinipokonya kamera yangu. nilichofanya ni kuongea Kimombo na hapo jamaa alijing'atang'ata sana akanipa kamera nikaondoka. Huu ni upuuzi yani watu wanapiga picha kwenye malls Dubai halafu hicho kimlimani city eti usipige picha. Sijui kama bado hako katabia kapo
 
Back
Top Bottom