TAHADHARI ya “Usipige Picha” nchini Tanzania na dunia ya leo

Ha haa!
Ukiwakuta wako bize na kugongelea vile vibao vyao eti, 'Usipige picha hapa'! Utadhani wamefanya kikuubwa.... Ila sasa kwa vile teknolojia imebadilika, kupitia google Earth unaweza ukaona inside out jinsi mazingira yao yalivyo...
Mimi nawashauri waaachane na mambo ya kizamani, waruhushu tu watu waje na vidio camera zao wajiachie maana hakuna kilichofichika.
La sivyo wawafuate google earth wawatie virungu... Samahani lakini!

Picha kwa hisani ya google earth...
View attachment 431049
Usichojua usiku Wa Giza na sio kila ukionacho ukiamini
 
Ukiwa nchi kama Russia kama wewe ni black skin/white ukiwa unapiga picha hovyo unalambwa shaba fasta/unasweka lupango! Wanasema unaipeleleza nchi yao
 
Zamani si lazima usogee upige palepale siku hizi lens 100 - 400mm unapiga uko mbali kabisa lakini picha kali.
 
Wana Mtandao.

Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii.

Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.

Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH.

Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?

Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe.

Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.

Kwa Jumba la Makumbusho naomba nitofautiane nawe,ukitoa kiingilio unaruhusiwa kupiga picha ,mimi mwenyewe nimepiga picha kibao pale Jumba la Makumbusho ,kama huamini njoo inbox uone hizo picha,laikni pia nakubaliana nao kuwa kuna sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam wenyewe hukataza kupiga picha ,unaambiwa ruksa kupiga kwa simu lakini sio camera,hata ukiwa ndani ya pantoni la Kigamboni huruhusiwi kupiga picha,tofauti na Zanzibar wenzetu kule hupiga picha bila tatizo lolote,pia hapa akiwa mzungu haulizwi sijui labda ni shida ya kuzungumza Kiingereza.Ila kwa teknolojia ilivyo siku hizi vizuizi vya usipige picha hapa naona vimepitwa na wakati.Hebu nikuulize mwenzetu huko majuu sheria za kupiga picha zinasemaje inaweza kutusaidia kidogo watu wa dunia ya tatu
 
Vituo vya mwendokasi picha marufuku
Kwenye pantoni ya kuvuka kigamboni picha maarufuku napo

Ova
 
jamani kuna sheria ambazo bado ziko vitabuni ndio vimesababisha mambo haya. Miye nakumbuka pale Chuo cha Ualimu Korogwe miaka hiyo kulikuwa na bango kubwa ati "Hairuhusiwi kupiga Picha"! Sijui tulikuwa tunaficha vitu gani kwenye vyuo vya walimu.
Hata kwenye mabwawa ya nguvu za umeme kama Mtera na Kidatu pamedandikwa usipige picha hapa,na hata stesheni za TAZARA wameandika hivyo,nilitaka kufanya documentary ya majengo ya kale hasa ya relwe na nikaambiwa sijui kwanza niandike barua halafu kama nitapata kibali itabidi nilipie,nikaona isiwe tabu nikasepa
 
Wana Mtandao.

Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii.

Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.

Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH.

Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?

Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe.

Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.

Nilishawahi kuandika kitu cha aina hii kwenye post inayoonyesha elimu yetu ilivyokuwa outdated.
 
Pole sana ndugu yangu, hii ndiyo BONGOland! Yaani siku hizi watu wanadhani picha ni mali. Nilikuwa nawaambia wale macurator wa huko Makumbusho kwamba wengine tumebahatika kufika katika museum kubwa tu za France na Italy na USA, na unapiga picha nje na katika baadhi ya maeneo uanweza ukaambiwa usipige picha kwa kutumia flash. Hata Last Supper ya Leonardo Da Vinci nilienda kuiangalia - the original one in Italy na tuliipiga picha bila tatizo ingawa bila flash! Sasa hapa ndo tunajifanya tunajua kuzuia picha, alafu uliza hizo pesa zinatumika vipi? Watapata kigugumizi.

Bila shaka ni kina muta nyie mikogo mingiiiii
 
Sina cha kucomment... Ila nimekuja ili kumjua huyu mtu aliyeitwa "Mdau" katika social network fulani ni nani...
 
Yaani hii ni POST ya zamani sana hadi nilisha sahau.

Sehemu nilipokuwa ilikuwa NYUMBA za Makumbukusho Kijitonyama. Hadi leo sijarudi tena pamoja na kuwa muda mwingi nipo Dar.

Nilichokuwa nalilia ni kuwa kama sehemu hawataki upite, upige picha au usimame nk, basi waweke kibao. Sipendi kuvunja sheria na pia sipendi kuviziana kwa watu ambao tunakuwa wageni sehemu fulani. Na kama ni sehemu ya JESHI au USALAMA basi ikae mbali na watu na wajenge uzio kuzungusha. Mie huko ndani ya uzio kwa kweli sintaonekana.

Kuna majengo ya zamani yenye PAINT huwa wanakataza kupiga picha kwa mwanga kwani mwanga unaharibu hizo PAINT. Ila unajulishwa kawaida kabisa. Mtu akinijulisha mapema sina shida hata kama jambo napingana nalo. Sipendi pale ambapo sijajulishwa na mtu anakuja kuniambia nimevunja sheria.

Kuna Hotel niliambiwa nisipige picha kwa Camera ila kwa simu sawa. Simu nyingine zinapiga picha nzuri kama Camera tu sasa sijui tofauti ni ipi. Anyway, kama nilivyosemwa, kama kibao kipo sina shida. Mara nyingi nakuwa mwangalifu kusoma vibao ili kutovunja sheria. Ila kwa nchi ya kitalii, mijini na mbugani tungelilegeza kamba kidogo na kuacha watu wapige picha.

Back
Top Bottom