Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,580
- 6,119
Wana Mtandao.
Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii.
Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.
Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH.
Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?
Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe.
Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.