Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

kwanza pole. lkn unawezaje kumpa mtu simu yako atumie? shukuru Mungu alitaka kukuibia hiyo simu vinginevyo angeweza kukuset ktk staili ambayo ungejutia mpaka unatwaliwa na Mwenyez Mungu.
 
TATIZO NA NYIE MKIOMBWA SMARTPHONE KIDIPLOMASIA HAMTOI MDADA KACHOKA VITOCHI
BABY BABY HAIJAZAA MATUNDA
HALI hii diplomasia haifai kabisa.safi sana JPM.Kuna mdada alikuwa anagongwa na bosi mmoja hivi.basi kila wiki simu mpya.sasa hivi dah hali ngumu
 
Marufuku kutoa cm Kwa usimjua hapo ukiambiwa uisaidie police cm yako imetumika kwenye mawasiliano utafanyaje
 
Juzi nimeenda Mlimani City kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa Mary Brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na ya kwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!

Mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mimi simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu.

Nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu. Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
ungempa mbataa kidogo au kumpiga picha na kumtangaza social media
 
Ni muhimu hasa kwa wanaume wanaolainika kirahisi kwa wanawake, kila wakati kuwa na simu ya kitochi bei tshs 25,000. Hivyo basi akitokea mdada kama huyo badala ya kumpa simu smartphone, unampa simu kitochi ili kupunguza hasara in case akiamua kukuibia!!!
 
Be carefull jinsi ylivyoichukua simu yako, angeweza kugueuzia kibao kwamba wewe ndio mwizi, mpaka ukweli ujulikane ushachakaa au kufa
 
Njaa bora iishie tumboni....ikisha fika kichwani....ni balaa tupu......
Hilo tukio katika hali ya kawaida unaweza ukawa unajiuliza limetokeaje tokeaje.....!!??
 
Mimi niliwahi kupanda daladala ya Tegeta kufika Mwenge akapanda binti fulani....tukawa tumekaa sitimoja.....mimi nilikaa upande wa dirishani.....kwa muda mfupi akawa rafiki yangu tukiongelea masual mbali mbali ya kijamii.......

Kutokana kumzoea na kufurahishwa na ucheshi wake akawa kama rafiki yangu wa siku nyingi so sikuona ubaya wa kumlipia nauli.....nikatoa noti yangu ya elfu kumi nikampa yule binti ampe konda akate wawili.......konda akasema kwa muda ule hakuwa na chenji kwa hiyo tumvumilie kidogo....wakati tunaendelea na story yule binti akashukia tangi bovu.....akapitia kwa konda akachukua na ile chenji.....mimi sina hili wa lile nafika mwisho wa safari naulizia chenji.....naambiwa acha utapeli wa kizamani wewe.....kwani ulivyomuambia yule binti achukue chenji ulizani tumesahau....!??

Ikabidi niwe mpole....huku nikiwaza nitarudi vipi nyumbani......
 
Hahahahaa. Pole sana Field Marshall
 
Ha ha ha ha, mkuu kama vile nakuona unatoka nduki kumtimua dah hataaaaaaari sana.

Ana kila sababu ya kumshukuru Mungu mara mbili.Kwanza kufanikiwa kumpata akiwa na hiyo simu bado kwani angekuwa na bouncer wake nje akawahi kumkabidhi ingeikuwa ishu.Pili ashukuru huyo mrembo hakuwa na kundi la vijana wa kihuni nje angeweza kungolewa macho.Ni kweli kuwa msaada huo asingeweza kuutoa kwa mwanamme mwenzie ila funzo amelipata.
 
Juzi nimeenda Mlimani City kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa Mary Brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na ya kwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!

Mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mimi simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu.

Nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu. Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
Wee jamaa ni noma sana. Nimekukubali! Mimi pia nilishataka kuibiwa simu na mdada kwenye bus. Nikamdaka kimya kimya. Wadada wamekuwa wezi sana siku hizi, sijui tatizo ni nini hasa.
 
Mjombaa huyo anabahati kukutana na wewe na roho yako lakini angelengana na mimi angejuta kuzaliwa, mimi kuna kadada kaliniliza gauni shop nikakastukia nilikazima kwa pigo moja tu fahamu alizipatia hospitali, simu yake nikakwarua pesa na gauni yangu nikarudisha dukani.
 
Back
Top Bottom