Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

Kuna rafiki yangu aliibiwa kwa style hiyo, tena sio mdada ni mbibi yuko na kinokia Torch chake anajidai kimezima na nataka kuongea akampa, bibi akatokomea kusikojulikana. Kuanzia siku hiyo stakag mazoea ya kuwapa SIM mastranger
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Yaan kumuacha ndio umefanya makosa aisee ungempeleka kwa wale maaskari na picha ungempga kabisa maana ni upuuz huo
 
pole sana ila ulitakiwa kujiongeza, kama alikuwa nacheza na simu iweje muda huo huo tena akwambie ya kwake imeisha chaji?
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Najaribu kupiga picha ulivyotoka nduki baada ya kugundua umeshaibiwa kama nakuona vile[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Pole sana kiongozi
 
Ungeombwa na mwanaume mwenzako usingempa ungejidai haina hela ila kwa Dada ukasema kama Dr love pimbi kajileta mwenyewe
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kupatwa kwa mdada sasa unaiba sim mpaka uiuze ni lin huyo sio mtanzania wadada wa Tanzania wanaiba kwa akili sana mpaka ustuke ushakuwa moja
 
Umenifurahisha sana ni kumyanganya simu yako na kurudi kupata msosi wako, asante kwa alert !
 
Ha ha ha ha, mkuu kama vile nakuona unatoka nduki kumtimua dah hataaaaaaari sana.
 
Utamuachia vp aende nayo counter hyo simu ase unampa aongee nayo hapohapo jirani ukimuona anazuga kwenda sehemu nyingine unamstua hapohapo aongee

Huyo mwenye bodaboda atakuwa mtu wake bila shaka
 
Unasemea hilo la simu ? Kuna hii style ya kinyoko kama hapo Mlimani City unakuta wamepaki gari yao kwenye parking mbali kidogo na mall karibia na hili Gate linatokea kwenye barabara ya Sam Nujoma basi mdada anavutwa kwenye gari sijui wanampulizia nini wanaondoka nae wanacho mfanya wanajua wenyewe ila fahamu zikimrudi mdada anajikuta kwenye mtaro

Na wanapenda sana kupasua vioo vya gari kuiba Laptop
 
Me Simu sikupi yani umevaa Nguo za Gucci Bag la Louis Viutton Gaun la Dolce Gabanna halafu una Samsung ya Laki, 5 eti huna vocha Ma Sista Duu wezi ndo mana staki Shobo Nao
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Juzi nimeenda Mlimani city kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa mary brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na yakwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!!! mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mm simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu, nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu.
Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
Don't do it again.. Mana hapo ulivokwara hyo cm yy angeweza kukuitia mwiz tuwe Makin ndugu zangu dada zetu WANANJAA sana
 
Juzi nimeenda Mlimani city kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa mary brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na yakwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!!!

mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mm simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu,

nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu.
Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
sio lulu huyu?
 
Back
Top Bottom