Tahadhari - Road Barrier ya Vibaka Mandela Rd na Shida ya Emmergency No. ya Police | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari - Road Barrier ya Vibaka Mandela Rd na Shida ya Emmergency No. ya Police

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sanctus Mtsimbe, Jun 2, 2009.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Wazalendo;

  Asalaam Aleykhum.

  Napenda kutoa tahadahri kwa watumiaje wa barabara ya Mandela wakati wa Usiku.

  Siku ya Ijumaa iliyopita nilikuwa naendesha gari along Mandela Road nikiwa natokea katika tafrija ya harusi Mbezi. Ilikuwa yapata saa nane za usiku/alfajiri. Tulikuwa Wanne katika gari.

  Mara baada ya kupita Landmark Hotel (Nikielekea upande wa Buguruni)karibu na njia panda ya kwenda Mabibo Hostel; tuliwaona vijana kama kumi wakiwa wamefunga barabara kwa mawe makubwa na gogo. Kwa haraka, tulishauriana kuwa haikuwa salama na tukaanza kurudisha gari reverse na kusubiri. Baada ya muda vijana wale walitoa mawe yale na gogo, nikaendesha gari kwa speed sana mithili ya mtu anayetaka kuwagonga, wakatupisha.

  Baada ya kupita salama, nilijaribu kupiga simu ya Emmergency 112 Kuomba msaada kwa Wanausalama wetu kuja kuwadhibiti wale waharifu, lakini automatic reply inilijulisha nisubiri dakika 17 kupata huduma ya kusikilizwa. Nilijaribu mara kadhaa lakini majibu yalikuwa yale yale.

  Nilipojaribu Simu ya Kamanda Kova ilikuwa imezimwa.

  Naomba sana Wazalendo mnaotumia barabara ile wakati wa usiku muwe makini sana.
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Poleni sana. Hiyo ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo.

  Vipi website ya TPN bado mazee?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ndugu Eneo hilo kuna kituo cha Polisi cha karibu kwanza ni External karibu na Jengo la TFDA na mbele kidogo kuna Kituo cha Tabata Relini kote huko kuna vituo na askari wale wako Macho masaa 24 ulishindwa nini kwenda kutuo chako cha karibu kupata huduma hiyo ? mfano ungekuwa umeumizwa ungetaka kova aje ? Hata ungempigia kova angeongea na kituo chako cha karibu cha Polisi labda kama ulikuwa unamtaka yeye Binafsi -- Tusidhalilishe Jeshi letu la Polisi kiasi hichi Jamani Tena kwa Mwelewa kama wewe , Msomi

  Au njia nyingine Mfano kama wewe ni mteja Wa Zain Piga hiyo no 100 Huduma kwa wateja wakati mwingine Unaweza kuongea na Mtoa huduma akakusaidia Kupeleka Taaarifa Mbali zaidi , sijui kwa mitandao mengine , mimi nakumbuka tu kuna siku nilikuwa nashida nikapiga hiyo 100 nikaongea na mtu wa Huduma kwa Wateja Nikampa Maelezo ya kutosha Wanausalama wakafika eneo Husika wa kituo cha Karibu
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu jamaa si ametoa tahadhari na ametoa ushauri .Vituo ulivyovitaja havina magari na sina uhakika kama askari pale wana silaha au mawasiliano-kawaida ya Police -posts.
  Ni mtu mgeni tu DSM asiyejua kuwa vituo vya post wakati wa emergency havina msaada wowote wa maana.
   
 5. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Sasa kama Polisi hawawezihimili emergencies then wawaeleze watu badala ya mtu kujikuta uko katika songombingo na polisi hawawezi kukusave. Maana ukijua there is no Polisi then akili itafanya kazi ya ziada ya kujisave.
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  baada ya kuzidiwa na majukumu ya kila siku polisi waliruhusu PRIVATE SECURITY GROUPS....!
  HOW DO WE SEE BAADHI YA MAJUKUMU AMBAYO DHAHIRI SHAHIRI YANAONEKANA NI HAWAYAWEZI KUOMBA PRIVATE POLICE?
  USALAMA BARABARANI, UDHIBITI UHALIFU(QUICK RESPONSE), UENDESHAJI KESI
  (TRAFFICK CASE), ETC
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,307
  Likes Received: 5,641
  Trophy Points: 280
  Ndugu hayo yamenikuta daraja la kawe na pale usithubutu kupita ujalock milango.....watakufanya kitu mbaya na wanajeshi shost...kazi kwetu....
   
 8. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #8
  Jun 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160

  Pole sana Mama Mia.

  Bila shaka tuna kazi ya ziada ya kuandaa mfumo madhubuti wa kudhibiti uhalifu.
   
Loading...