Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Umenikumbusha miaka kadhaa iliyopita, kwenye lift za IFM daaah kuna wadada wawili walivua t-shirts live joto lilivyokolea tulikwama kama dakika 10 tu.
 
Pole sana mkuu, si lile jengo pale karibu na NMB na CRDB?
Hapana ni lile la pale makaburi ya mjerumani mkabala na ofisi za nhif kama unaenda ofisi za Tanga Fresh za Zamani.

Ilikua hivii.

Tulipanda lifti na jamaa yangu (ni jf member), tukiwa tunaenda floor ya kwanza tu , japo niligoma ila jamaa akalazimisha tupande.

Mlango ukafunguka tukaingia, ghafla kuna jamaa wakawahi tukawa watu 4.

Ile lift ni zile za kizamani sana. Chumba kipo sealed. No taa, hewa ya kubembeleza.

Ndani tukakuta wamebandika namba za Emergency.

Tukapress 1, jamaa wengine wakapress 4 (nakumbuka vizuri)

Lift ikaanza kwenda juu kidogo. Alaf ikagota ikaanza kurudi chini, ikagota ikaanza tena kurudi juu, ikagota ikawa inarudi chini, alaf ndio ikakwama hapo hapo chini. Tukawa tumestack.

Hapo hapo nikapata panic attack (mana ndio ilikua shida yangu kubwa), niliwahi tokewa na tatizo kama hilo hapo nyuma kidogo.

Jamaa wakaanza kubonyeza button ya kufungua mlango, wapiii chenga?, lift ikaanza kuwa kaburi, joto na hewa inakata huku na mimi panic ndio ipo kwa peak.

Mmoja akapiga simu ya mafundi (namba zilizokua ndani ya lift) simu zikawa hazitoki.
.katika bonyeza bonyeza nikiwa miguu haina nguvu nimekaa chini nasubir kifo changu ama msaada , mlango ukafunguka.

Aisee niliruka kama mshale, sijui nguvu zilitoka wapi.

Tangu siku hiyo kitu kinaitwa lift sitaki na sikitaki maishani mwangu. Shubhaamit


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee niliruka kama mshale, sijui nguvu zilitoka wapi.

Tangu siku hiyo kitu kinaitwa lift sitaki na sikitaki maishani mwangu. Shubhaamit
emoji4.png
Umenichekesha sana mkuu, ila kwakweli serikali ingeweka viwango vya aina ya lift na technology salama na ifuatwe na watu wote
 
yeah nimezipenda sana lift za rock city mall Mwanza ni transparent kwa nyuma ukikwama unaweza kuwave na fulana yako ukasaidiwa
 
Mimi pia ni mhanga, jengo la Mega complex Arusha, floor ya tano Kenyatta University.
Tulikuwa watatu vidume wote, jamaa yangu akaanza kulipiga ngumi, mlango mgumu balaa, Dakika kama Tano, Jenereta likawashwa hapo tushaanza onja joto ya jiwe kijasho.
Ni ombea mtu tu akusimulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usije ukarudia tena kulazimisha mlango wa lift kufunguka
 
Kiukweli binafsi kuanzia ghorofa ya kwanza - tatu huwa sipandi lift kabisaaa napiga zangu mdogo mdogo,naogopa mnoo na ikinilazimu kupanda hadi nifike niendako huwa nahisi presha kabisaa, sizipendi kabisaaaa.
 
Back
Top Bottom