Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Nimefurahinkwelim kweli. Ati milango ya kioo nitauvunja!! Wadhani hicho lkioo ni laini tu kwamba ukipiga chafya tu tiyari kimevunjika?? Hapana. Kioo uzuri wake ni kuwa, wataalam wanawaona mpo wapi hivyo watafanya bidii kuwatoeni. Mlango wa lifti ni madhubuti saana kwa usalama wako pia.
Furaha na masikitiko ni huyo aliyebaki anamkumbatia mdada aliyeingiwa kifafa. Nadhani hata namba zake alikupa umpigie. Hapo ndio wamama mshike adabu mbele ya mwanamume
Mkuu maana yangu ni kwamba kukiwa na vioo watu wanawaona kwahiyo ni mizuri kwaajili ya usalama, endapo mtu anataka kukudhuru inakuwa rahisi kuonekana ndio usalama ninaouzungumzia mimi.
 
Sio kuonekana tu hata pressure inakaa sawa kama unawaona watu kwa nje na namna wanavyoshughulika kukutoa kuliko ile milango mizito hujui kama kelele zako zinasikika? Au watu wanakuona? Pressure inakua juu kwa hofu
 
Saa kama tatu hivi zilizopita nilikua Kariakoo kwenye jengo moja la ghorofa saba ambalo hutumika kama makazi ya watu na ofisi pia. Ofisi niliyokua naenda ipo ghorofa hiyo ya saba ambapo ilinilazimu nipande lift

Nilipobonyeza kitufe cha namba ya floor ninayoenda akawa amekuja dada ambaye kwa mavazi yake nikahisi alikua ametoka au anakwenda kwenye mazoezi (nadhani kwenye jengo lile ipo gym) hivyo ikanilazimu nibonyeze kitufe cha kumsubiria akapanda tukaondoka

Sekunde chache tu baada ya kuondoka tukiwa tunapita floor ya tatu taa zikazimika ndani ya ile lift, ikatoa mlio kama imegonga kitu halafu ikawa kama inarudi chini kisha ikasimama kabisaa! Yule dada akapiga yowe la ku panik. Nilipomwambia asiwe na wasiwasi tutatoka akanisogelea na kunikumbatia huku anaendelea kupiga kelele

Changamoto kubwa ni ile milango ya lift yenyewe ilivyokua mizito mpaka unahisi kabisa hata hizo kelele hazifiki popote. Nilinyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha emergency bila kuondoa mkono(continuously) lakini hatukuweza kupata msaada kwa haraka

Hali ilikua ya taharuki kubwa maana kile kichumba cha lift ni kdogo, milango ni minene sana na joto lilikua linaongezeka. Tulikaa mle kama dakika saba au nane ambazo zilikua kama mwaka ndipo zikasikika sauti za watu kwa nje wakiwa wanashughulika kutufungulia mlango na muda walipofanikiwa kutufungulia yule dada niliyekua nae alikua amelala chini kwenye sakafu ya lift na akawa kama anaeelekea kupoteza fahamu!!!

Namshukuru Mungu tulitoka salama ingawa yule dada ilibidi apelekwe hospitali kwa hali aliyokua nayo maana hata mambo yake mengine ya kiuanamke (tafsida imezingatiwa) yalimuharibikia na ukizingatia mavazi aliyokua amevaa hakutarajia pengine mambo yamtokee wakati huo!

Wito wangu kwa watengeneza elevators, watengeneze lifts za milango transparent ili mtu aweze kuona nje angalau pressure inapungua kuliko hizi lift zenye milango utadhani gereza au kaburi aisee! Mtu unapokua unawaona watu nje unajua muda wowote unatoka. Amakweli kifo kwa binadamu ni sekunde tu!
Huo muda ilitosha kabisa kumpiga mashine huyo mrembo..uliletewa mboga mezani ukaacha kula..bure kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepiga ramli nimeona kuna mtu.hapo mtaani kwenu anakuloga.Njoo pm nikupe dawa na kukuibia vijihela kidogo.I'm kidding!
 
Mkuu, ulibonyeza unapokwenda, halafu ukabonyeza kumsubiri mdada...hapo ndipo zali lilipoanzia. Maji ukiyavulia nguo, shurti uyaoge,,,
Nakushauri mfuatilie huyo mdada hadi hospitali ili muendelee kuwasiliana, yajayo yanafurahisha. Kumbuka kutujuza maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumsubiria aingie lilikua ni jambo la kibinadamu zaidi mkuu
 
Kiukweli hali ya usalama wa lift zenu bado serikali haijaweka utaratibu na kuzifuatilia lakini taarifa kama hizi itasaidia watupie jicho pia. Kuna jengo parking za magari ndani ya jengo unatumia lift na kuna siku nilishuhudia jamaa akipandishwa na lift alafu ghafla ile lift ikataka kubinuka ikiwa imeshapanda juu! Isingekuwa u sharp wa operator wa lift kuisimamisha leo tungekuwa tunasema mengine. Tanzania swala la lift kwenye majengo bado halina control zaidi ya kudra za Mungu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom