nasnay
JF-Expert Member
- Mar 28, 2015
- 599
- 911
Nitajitahidi mkuu na Mungu AniwepesishieHapo kwenye kutoa ahadi kedekede umejaribiwa. Ni muhimu utimize hizo ahadi.
Saa kama tatu hivi zilizopita nilikua Kariakoo kwenye jengo moja la ghorofa saba ambalo hutumika kama makazi ya watu na ofisi pia. Ofisi niliyokua naenda ipo ghorofa hiyo ya saba ambapo ilinilazimu nipande lift
Nilipobonyeza kitufe cha namba ya floor ninayoenda akawa amekuja dada ambaye kwa mavazi yake nikahisi alikua ametoka au anakwenda kwenye mazoezi (nadhani kwenye jengo lile ipo gym) hivyo ikanilazimu nibonyeze kitufe cha kumsubiria akapanda tukaondoka
Sekunde chache tu baada ya kuondoka tukiwa tunapita floor ya tatu taa zikazimika ndani ya ile lift, ikatoa mlio kama imegonga kitu halafu ikawa kama inarudi chini kisha ikasimama kabisaa! Yule dada akapiga yowe la ku panik. Nilipomwambia asiwe na wasiwasi tutatoka akanisogelea na kunikumbatia huku anaendelea kupiga kelele
Changamoto kubwa ni ile milango ya lift yenyewe ilivyokua mizito mpaka unahisi kabisa hata hizo kelele hazifiki popote. Nilinyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha emergency bila kuondoa mkono(continuously) lakini hatukuweza kupata msaada kwa haraka
Hali ilikua ya taharuki kubwa maana kile kichumba cha lift ni kdogo, milango ni minene sana na joto lilikua linaongezeka. Tulikaa mle kama dakika saba au nane ambazo zilikua kama mwaka ndipo zikasikika sauti za watu kwa nje wakiwa wanashughulika kutufungulia mlango na muda walipofanikiwa kutufungulia yule dada niliyekua nae alikua amelala chini kwenye sakafu ya lift na akawa kama anaeelekea kupoteza fahamu!!!
Namshukuru Mungu tulitoka salama ingawa yule dada ilibidi apelekwe hospitali kwa hali aliyokua nayo maana hata mambo yake mengine ya kiuanamke (tafsida imezingatiwa) yalimuharibikia na ukizingatia mavazi aliyokua amevaa hakutarajia pengine mambo yamtokee wakati huo!
Wito wangu kwa watengeneza elevators, watengeneze lifts za milango transparent ili mtu aweze kuona nje angalau pressure inapungua kuliko hizi lift zenye milango utadhani gereza au kaburi aisee! Mtu unapokua unawaona watu nje unajua muda wowote unatoka. Amakweli kifo kwa binadamu ni sekunde tu!
Yap huyohuyo, kwa bahati mbaya hadithi ya mkimbizi sikuwahi kuimalizaUnamzungumzia yule BINGWA WA TAHARUKI TANZANIA, Hussein issa Tuwa wa Mkimbizi ya Tiga Mumba?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo elevator ni bongo tu ila ulaya wameshaupdate na wanatumia za Vioo
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeniuliza kama ninawajua.Nimejibu kama wangekuwa na faida ya kuweka ugali mezani binti yangu Wakuru akala ningewajua.They have got nothing aside maandishi yao.
Asante mkuu, nimeshapoa lakini sijui yule abiria mwenzangu anaendeleaje huko aliko
Jamaa ni fundi wa kizazi hiki. Uliishia wapi labda nikumegee ka utam kidogo. Msome pia kwenye Sniper, Wimbo wa gaidi, Mtuhumiwa, Utata wa 9/12 1&2. Kwa uchache,Ila kwa sasa yupo on fire na Mtafiti.Yap huyohuyo, kwa bahati mbaya hadithi ya mkimbizi sikuwahi kuimaliza
Sent using Jamii Forums mobile app
And,I repeat, jamaa ananakili vitabu vya mabeberu.Jamaa ni fundi wa kizazi hiki. Uliishia wapi labda nikumegee ka utam kidogo. Msome pia kwenye Sniper, Wimbo wa gaidi, Mtuhumiwa, Utata wa 9/12 1&2. Kwa uchache,Ila kwa sasa yupo on fire na Mtafiti.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo elevator ni bongo tu ila ulaya wameshaupdate na wanatumia za Vioo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hadly Chase ipi umeshaipitia mkuu?And,I repeat, jamaa ananakili vitabu vya mabeberu.
Mkuu kuna watu hawaruhusiwa kupanda mipando na Dr mfano waliovunjika miguuNdio tuache uvivu sasa maana hilo ni bonge la zoezi! Kama hapo ghorofa ya 8 ni ofisini kwako huna tena haja ya kua unaenda mazoezini kwenye viwanja vya mpira😀😀😀
Ni vema na haki. Kuendelea kuwasiliana ndio ubinadamu wenyewe.Kumsubiria aingie lilikua ni jambo la kibinadamu zaidi mkuu
Kupitia maandishi ndipo tulipojifunza ustaarabu tulionao sasa. Haijalishi andiko linakuvutia wewe au la, ila elewa kila andiko liwe la kipuuzi au la hekima lina impact kwenye jamii yoyote. Wengine wanavutiwa na maandiko matakatifu na wanayafuata ila wanajishuhulisha na shuhuli za kuzalisha kipato, maandiko yana sehem yake na umuhimu wake. Wengine hayajui na wala hawana mpango wa kuyajua maandiko yako uyaonayo bora na yanakuletea kipato na rizki mezani na wanaishi vyema pengine hata kukushinda wewe.Umeniuliza kama ninawajua.Nimejibu kama wangekuwa na faida ya kuweka ugali mezani binti yangu Wakuru akala ningewajua.They have got nothing aside maandishi yao.
Yaani hata sikumbuki vizuri best, niliishia pale mchumba wake anamsisitiza aende akatibiwe sina hakika kama niliendelea zaidi ya paleJamaa ni fundi wa kizazi hiki. Uliishia wapi labda nikumegee ka utam kidogo. Msome pia kwenye Sniper, Wimbo wa gaidi, Mtuhumiwa, Utata wa 9/12 1&2. Kwa uchache,Ila kwa sasa yupo on fire na Mtafiti.
Sent using Jamii Forums mobile app
Lift nao si usafiri mkuu?SUMATRA WANAHUSIKAJE NA ELEVATORS MKUU?

Waonaje twende kule jukwaa husika ili tuwachambue wawili hawa kwa pamoja. Usisahau Japhet Nyang'oro Sudi wapo wanaosema anamuiga Bingwa Ben R Mtobwa na Joram Kiango wake. Tafadhal, twende eneo husika tukapeane ma ujuzi.And,I repeat, jamaa ananakili vitabu vya mabeberu.
A lot of them.Mia sita salasini na sita kasarobo to mention!Hadly Chase ipi umeshaipitia mkuu?