umenikumbusha 2016 ilikuwa siku ya harusi ya mdogo wangu, kwenye hoteli flani pale ubungo tulikuwa watatu tunashuka kwenye lift tumpeleke bibi harusi salom. umeme ukakatika tena ule wa mgao wa kukatika asubuhi kurudi jioni. sitasahau jamani tulikaa kwenye lift karibu nusu saa ilikuwa hekaheka mpaka kugundulika tumekwamia wapi, kumbe bahati nzuri tumekwama ground flour yani tulishafika chini, ndio ikaletwa chepe ikaingizwa kwenye mlango ukaanza kufunguliwa kwa lazima kukapatikana tu kaupenyo cha kuingiza hewa, wenzangu wawili niliokuwa nao walisha faint chini nguvu zimewaisha wanaswet balaa, mimi nimekazana na maombi jamani dah. tunasikia tu nje wanasema generator automatic ni bovu sijui na fundi hapokei simu jamani dah! sijui alitokea wapi msamaria mwema akachokonoa generetaro likawaka ndio mlango ufunguke tukatoka. sikuamini kama tumetoka salama kutokana na story za lift ambazo nishazisikiaga. kweli Mungu alitusaidia